Karibu kwenye Tovuti Rasmi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same na hapa utaweza kupata taarifa mbalimbali zinazohusu Wilaya ya Same.
Wilaya ya Same ni miongoni mwa Wilaya 6 zinazounda Mkoa wa Kilimanjaro na ilianzishwa mwaka 1962. Wilaya iko kilomita 105 kutoka Moshi ambapo ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro.
Wilaya hii inachukua eneo la kilomita za mraba 5,186 sawa na 39% ya eneo lote la Mkoa (13309km2).
Muundo wa Utawala
Wilaya ya Same ina Majibo mawili ya Uchaguzi ambayo ni Same Magharibi na Same Mashariki, Wilaya hii imegawanywa katika tarafa 6, kata 34, vijiji 100 na vitongoji vilivyosajiliwa 503 kati ya hivyo kuna vitongoji 16 vinavyofanya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Same. Wilaya pia ina majimbo mawili ya ubunge ambayo ni Same Mashariki inayoundwa.
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Wilaya ya Same ina jumla ya watu 300,303 wakiwemo Wanaume ni 147,293 na Wanawake 153,010. Msongamano wa watu ni watu 53 kwa Km2, Ukuaji kwa mwaka ni 2.4% na jumla ya Kaya katika Wilaya 76,272. Ukubwa wa wastani wa kaya ni 4.5.
Wakazi wa Same
Wakazi wengi wa Same ni wa kabila la Wapare na wahamiaji wachache kutoka Usambara na Wachaga kutoka Moshi, kabila la Wamasai wametawanyika kwenye Kata za Ruvu, Kisiwani, Maore, Ndungu, Makanya, Kata ya Kihurio na kata ya Hedaru hasa wakiishi kama wafugaji.
Shughuli za Kiuchumi
Takriban 90% ya wakazi wa Wilaya ya Same wapo vijijini na wanategemea sana kilimo na ufugaji kwa maisha yao. Mbali na shughuli za kilimo baadhi ya wananchi wachache hutegemea biashara kuendesha maisha yao.
Katika miaka ya hivi karibuni Wilaya imekuwa ikiuza mazao ya chakula na biashara nje ya nchi.
Mazao ya chakula yanayolimwa hasa ni mahindi, mpunga, mtama wa maharagwe, mihogo, kunde, fiwi,viazi vitamu, ulezi na ndizi. Mazao makuu ya biashara ni kahawa, na tangawizi, mpunga na mahindi .
Maeneo ya Uwekezaji
Wilaya ya Same ina maeneo mbalimbali ya Uwekezaji ikiwemo uwekezaji kwenye kilimo cha umwagiliagi kwenye Kata za Maore,Ndungu,Ruvu na Kihurio.
Uwekezaji mwingine ni wa viwanda vya Saruji na Gypsum maana Wilaya ya Same ni tajiri kwa madini yanayotumika kwenye utengenezaji wa Saruji kama Gypsum, Magnesite ,pia Wilaya ya Same ina dhahabu kwa kiasi kidogo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.