Jumla ya wagombea tisa wameteuliwa kugombea ubunge katika majimbo ya Same Mashariki na Same Magharibi kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 Mwaka huu.
Akitoa taarifa hiyo Msimamizi wa uchaguzi wa majimbo hayo Bi.Nice Ngasala, amesema kwenye Jimbo la Same Magharibi waliochukua fomu ya Ubunge walikuwa Saba lakini walioteuliwa ni watano ambao ni Dkt. Mathayo David (CCM) Dkt Kidagho Mohamed (AAFP) Bw.Elisante Majid (ACT- Wazalendo) Bi. Ester Maregesi (Chama cha MAKINI) na Gervas Mgonja (CHAUMA ) ambapo Abdul Mkongo (NCCR -Mageuzi) hakurejesha fomu huku Sidra Katanga ( N.R.A) akiwekewa pingamizi.
Kwa upande wa Jimbo la Same Mashariki walioteuliwa kugombea Ubunge ni Deogratias Kweyamba (N.R.A), Bi.Anne Kilango (CCM) Nagy Kaboyoka (ACT-Wazalendo) Bi. Zaina Nampoto ( Chama cha MAKINI) ambapo Allan Alson wa CHAUMMA alichelewa kurejesha fomu hivyo kukosa uteuzi.
Kwa upande wa nafasi za udiwani jumla ya wagombea 39 wameteuliwa kugombea udiwani Jimbo la Same Magharibi lenye Kata 20 huku wagombea 25 wakipitishwa kugombea udiwani Jimbo la Same Mashariki ambalo lina Kata 14.Wagombea udiwani waliopitishwa wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT Wazalendo na CHAUMMA.
Bi.Ngasala amewapongeza wote walioteuliwa kugombea nafasi ya ubunge na udiwani na kuwasihi kufanya kampeni zao kwa kufuata sheria taratibu na kanuni kama ilivyoelekezwa kwenye kanuni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2025.
Amewataka pia wananchi kujitokeza katika kampeni hizo ili kusikiliza sera za wagombea na kuweza kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga Kura.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.