Halmashauri ya Wilaya ya Same imetoa pikipiki 10 kwa vikundi vya vijana wajasiriamali kupitia mkopo wa asilimia kumi unaotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akizungumzia Mkopo huo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Same Bw.Charles Anatoly amesema Pikipiki hizo zilizotolewa zina thamani ya Shilingi Milioni 30 na zinatarajiwa kutumika kibiashara kama bodaboda.
Vikundi vilivyonufaika na Mkopo huo ambao ni sehemu ya Mkopo wa asilimia 10 uliitolewa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026 ni Kikundi cha Vijana Bodaboda Ndungu naKikundi cha Vijana Bodaboda Same.
"Katika robo hii ya kwanza tumetoa Mkopo wa Shilingi Milioni 184.5 na hizi Pikipiki tulizokabidhi leo ni sehemu ya Mkopo huo"Alisema Bw. Charles
Hata hivyo amewataka vijana hao kuhakikisha kuwa wanatumia Pikipiki hizo kwa malengo tarajiwa ili waweze kurejesha mkopo huo.
Bw.Charles pia amewakaribisha waombaji wengine wa Mkopo kuanza kuwasilisha maombi yao ya Mkopo kwani tayari dirisha la maombi limefunguliwa Novemba 05,2025 na litafungwa Desemba 20,2025.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.