HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME
HISTORIA YA WILAYA YA SAME.
UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Same ilianzishwa rasmi kwa Sheria ya Bunge Sura ya 287 (Mamlaka za Wilaya) ya Sheria za Tanzania na ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 01 Januari 1984. Aidha Halmashauri ina Idara 13 na vitengo 6 ambavyo vinatekeleza majukumu mbalimbali kama ambavyo imeanishwa hapo chini:-
1.0 IDARA YA AFYA
1.1 Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Asilimia 30.6 ya kaya za Wilaya ya Same zimejiunga na CHF. Kwa Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Same ni ya 3 Kati ya Wilaya saba za Mkoa.
1.1.1 Mipango/Mikakati Iliyopo kufikisha 80%
Jedwali 1.1: Vituo Vya Kutolea Huduma Za Afya Wilayani
S/No |
AINA YA KITUO |
IDADI |
|||
|
|
SERIKALI |
MASHIRIKA YA DINI |
BINAFSI |
JUMLA |
1 |
Hospitali |
1 |
1 |
- |
2 |
2 |
Vituo vya Afya |
6 |
1 |
1 |
8 |
3 |
Zahanati |
39 |
15 |
9 |
62 |
|
Jumla |
46 |
17 |
10 |
72 |
Chanzo: Idara ya Afya
1.3 Hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma ni wa wastani, hii imesababishwa na upungufu wa dawa na vifaa tiba kutoka bohari ya dawa (msd), pia msd kutotoa ruhusa ya kununua dawa na vifaa tiba mapema kutoka kwa wazabuni wengine. Vifaa vilivyopo kwenye Hospitali ya Wilaya ni X-ray, Ultrasound, Anaesthetic machine, Autoclave, Washing mashine, Generator, Microscope, Votex, Diathermy na Pima Machine.
1.4 Mkakati makini wa zoezi la usafi na Mipango ya kuwafanya watu wajenge tabia ya usafi
1. Kila kitongoji kuwa na siku moja ya usafi itakayoshirikisha kila mwananchi tofauti na siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi ya usafi kitaifa
2. Kuunnda/kuwa na vikundi kazi kwa kila kata vitakavyotokana na jamii , vitakavyohusika kusimamia usafi kwa kila kata na watakao kaidi watatozwa faini. Aidha asilimia kadhaa ya faini itakuwa ya vikundi/kikundi kutegemeana na makubaliano
3. Kila kata kuwa na Afisa afya atakayeshirikiana na wataalamu wengine waliopo kwenye kata. Kata ambayo haina Afisa afya ateuliwe afisa maendeleo ya jamii kukaimu nafasi ya Afisa afya
4. Kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani wote watakaokiuka sheria na kanuni za afya ya mazingira
5. Kuwa na dampo la taka ngumu na taka maji katika Halmashauri
6. Kuwa na vitendea kazi, gari rasmi la kusomba taka na ada za uzoaji taka zitumike kwa makusudi ya uzoaji taka
7. Kuwezesha walezi wa kata siku 5 kila robo mwaka kwa ajili ya kutembelea kata na kuhamasisha jamii juu ya usafi wa mazingira
8. Kila biashara/ kaya kuwa na chombo/vyombo vya kuhifadhia taka
9. Kushinadanisha kitongoji au mtaa, kata na kata ili kuleta ushindani na kuboresha usafi
10. Kujenga vizimba vya taka katika maeneo yatakayo ainishwa Elimu ya usafi na mazingira ikaziwe shuleni (shule za msingi, sekondari na vyuo) mahali pa kazi yao.
1.5 Idadi ya Watumishi waliopo, Ikama na Pungufu ndani ya Idara
Idara ya afya inahitaji jumla ya watumishi 1114 waliopo ni 462, idara ina upungufu wa watumishi 689. Sawa na 61.8%. Hospitali ya Wilaya inahitaji Watumishi kwa kada kama ifuatavyo:-
Jedwali 1.1: Idadi ya Watumishi waliopo, Ikama na Pungufu ndani ya Idara
FANI YA MTUMISHI |
HITAJIKA |
WALIYOPO |
PUNGUFU |
|
Medical Doctor |
23 |
4 |
19 |
|
Assistant Medical officer |
39 |
3 |
36 |
|
Assistant Dental officer |
1 |
- |
1 |
|
Dental therapist |
2 |
1 |
1 |
|
Pharmacist |
2 |
1 |
1 |
|
Pharmaceutical Technologist |
|
5 |
|
|
AssistantPharmaceutical Technologist |
8 |
- |
8 |
|
Social welfare |
3 |
- |
3 |
|
Environmental officer Health officer |
2 |
1 |
1 |
|
Wauguzi |
99 |
71 |
28 |
|
Laboratory scientist |
1 |
1 |
- |
|
Health laboratory technologist |
4 |
4 |
- |
|
AssistantHealth laboratory technologist |
4 |
1 |
3 |
|
Occupational therapist |
2 |
1 |
1 |
|
Physiotherapist |
2 |
2 |
- |
|
Medicall attendants |
59 |
44 |
15 |
|
Health secretary |
1 |
1 |
- |
|
Medical recoder |
5 |
1 |
4 |
|
Radiology scientist |
1 |
- |
1 |
|
Radiographer technologist |
3 |
- |
3 |
|
Nutritionist |
1 |
1 |
- |
|
Ophthalmologist |
1 |
1 |
- |
|
Optometrist |
3 |
- |
3 |
|
Economist |
1 |
- |
1 |
|
Biomedical technologist |
4 |
- |
4 |
|
Motury attendants |
5 |
- |
5 |
|
Computer system analysit |
1 |
- |
1 |
|
Computer operator |
1 |
- |
1 |
|
Accountant |
1 |
- |
1 |
|
Assistant Accountants |
2 |
- |
2 |
|
Supplier officer |
1 |
- |
1 |
|
Assistant supplier officer |
1 |
1 |
- |
|
Electrical Technician |
4 |
- |
4 |
|
Personal secretary |
1 |
1 |
- |
|
Plumber |
1 |
- |
1 |
|
Security guard |
4 |
2 |
2 |
|
Cooker |
4 |
- |
4 |
|
Dhobi |
4 |
- |
4 |
|
Driver |
5 |
2 |
3 |
|
|
|
|
|
|
Chanzo: Idara ya Afya
Kwa upande wa Hospitali ya Wilaya, kutokana na staffing level 2014-2018 Hospitali ya wilaya ina upungufu wa watumishi 97.
1.6 Magonjwa Kumi yanayoongoza kwa Idara ya Wagonjwa wa Nje ni:
Magonjwa ya njia ya hewa, Nimonia, Malaria, Magonjwa ya kuhara, Minyoo ya tumbo, Magonjwa ya ngozi, Magonjwa mengine, Upasuaji wa dharura, Upungufu wa damu na Magonjwa ya macho.
1.7 Magonjwa Kumi yanayoongoza kwa Idara ya Wagonjwa wa Ndani ni: Nimonia, Magonjwa ya njia ya hewa, Magonjwa mengine, Malaria kali, Upungufu wa damu, Magonjwa ya kuhara, Watoto waliozaliwa na uzito mdogo, Upasuaji wa dharura, Ukimwi na Majeraha mbalimbali.
1.8 Vifo Vya Watoto Umri Chini Ya Siku 28
Mwaka 2015 vilitokea vifo 5 katika vizazi hai 1000
1.9 Vifo Vya Watoto Chini Ya Miaka 5
Mwaka 2015 vilitokea vifo 8 katika vizazi hai 1000
1.10 Hali Ya Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI
Kiwango cha maambukizi ni 1.4%, Watu wanaoishi na VVU ni 6,181, wanaotumia dawa ni WAVIU 4, 688, vituo vinavyotoa huduma kwa WAVIU ni 8, na huduma kwa njia ya kliniki ya mkoba ziko 9.
1.11 Changamoto
Idara ya afya inapambana na Changamoto zifuatazo: -
1. Upungufu wa watumishi wenye taaluma mbalimbali kwa asilimia 61.4%
2. Kuchelewa kupokea fedha za mfuko wa pamoja na kutokupokea kabisa fedha za kutokana na kutokupata fedha za matumizi mengineyo (OC) ruzuku kutoka serikali kuu tangu mwezi Januari 2016
3. Wodi zilizopo ni ndogo hazikidhi mahitaji.
4. Upungufu na uchakavu wa nyumba za watumishi katika ngazi zote za vituo vya huduma.
5. Maabara ya Hospitali ya wilaya ni ndogo, Halmashauri imeanza funya mawasiliano na marafiki wake wa Tillburg Partnership Uholanzi ili kupata fedha za ujenzi wa Maabara mpya.
6. Kutokupokea fedha ya kulipa watumishi walioitwa kazini (on call allowance) tangu mwezi Janauri 2016.
1.12 Mikakati ya kupambana na Changamoto
Ili kupambana na changamoto hizo, idara imeweka mikakati ifuatayo:
i. Kuomba vibali vya ajira na kuweka vivutio kwa waajiriwa wapya na watumishi kwa ujumla (Staff attraction and Retention strategies)
ii. Kushirikiana na Bohari ya dawa (MSD) kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kwa kuhakikisha kwamba kila kituo kinaandaa na kutuma taarifa na maombi ya dawa na vifaa – tiba kwa wakati kwenda MSD, na Idara kufuatilia maombi hayo ili yafanyiwe kazi na makasha kusambazwa vituoni kwa wakati muafaka.
iii. Halmashauri tayari imeomba mkopo wa dawa kutoka Mfuko wa Taifya wa Bima ya Afya na inakarabati chumba kwa ajili ya duka la dawa ndani ya hospitali ya Wilaya ili kukabiliana na changamoto ya wagonjwa kununua dawa na vifaa tiba nje ya hospitali.
iv. Kushirikisha wadau wengine wa sekta ya Afya katika upatikanaji wa Vifaa tiba na vitendea kazi Muhimu vya kutolea huduma bora za afya. Hadi sasa Idara imewashirikisha Tillburg Partnership (Uholanzi), PSPF, CRDB na NMB. Bado Idara inatafuta wadau wengine.
v. Kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kupata fedha za kujengea jengo la kusubiria wajawazito na wodi za wagonjwa katika Hospitali ya wilaya.
vi. Kuendelea kuomba fedha serikali kuu kwa ajili ya ruzuku, posho za kuitwa kazini na posho ya kujikimu kwa waajiriwa wapya.
2.0 IDARA YA ELIMU MSINGI
2.1 Utangulizi
Halmashauri ina jumla ya shule za Msingi 192 kati ya hizo shule 185 ni za Serikali na 7 ni za binafsi. Shule hizi ziko katika Kata za Kiutawala 34 na Kata 1 ya Kielimu.. Shule hizi zina jumla ya wanafunzi 59833 kati yao wasichana ni 30613 na wavulana ni 2920.
2.2 Ufaulu wa Wanafunzi
Kiwango cha kufaulu kwa Mtihani wa Taifa darasa la Saba Kimkoa na Kitaifa ni kama ifuatavyo:-
Jedwali 2.1: Ufaulu wa Mtihani wa Taifa darasa la Saba Kimkoa na Kitaifa
MWAKA |
KIWANGO CHA UFAULU (%) |
NAFASI KIMKOA |
NAFASI TAIFA |
2014 |
63.48 |
7 |
52 |
2015 |
75.94 |
6 |
51 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
2.3 Malengo Ya Kuongeza Ufaulu
Ili kufikia malengo ya asilimia themanini na tano ya ufaulu (85%), Halmashauri kupitia idara ya Elimu Msingi imeweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la ufaulu duni katika mitihani ya ndani na ya kitaifa kama ifuatavyo:
o Kufuatiliaji utendaji kazi wa walimu katika Uongozi na Utawala na Utekelzaji wa Mtaala. Zoezi lilianza kwa kufuatilia shule 35 zilizofanya vibaya zaidi
o Kuomba walimu toka TAMISEMI ili tuweze kupunguza upungufu mkubwa wa walimu.
o Kuhamashisha wazazi na walezi kuchangia chakula cha mchana ili wanafunzi wapate chakula cha mchana shuleni.
o Shule zote zimepewa maagizo ya kutekeleza Ratiba ya ufundishaji wa muda wa ziada ili kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kipindi kilichopita.
o Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa elimu itaendelea kutoa mafunzo ya mbinu za ufundishaji kwa walimu mfano semina ya somo la Lugha na Hisabati.
o Idara inaendelea na mpango wa kusoma na kutafisiri mpango wa kuinua taaluma ya Mkoa wa Katavi ujulikanao kama “ Katavi model” ili uweze kuhawilishwa na kutumika katika wilaya ya Same kwa lengo la kuinua na kuboresha taaluma.
o Kuhimiza na kusimamia mazoezi ya mwisho wa wiki, mwezi, mitihani ya utamirifu na ile ya Mwisho wa mihula ili kuchochea ushindani katika ngazi ya darasa, shule, Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa.
o Kupitia na kutekeleza Ushauri na Mapendekezo Mthibiti Ubora wa Elimu shuleni.
o Kutoa motisha chanya kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya utamirifu Wilaya, Mkoa na Mitihani ya Kitaifa.
Jedwali 2.2: Miundo Mbinu Ya Shule: Samani Na Majengo
SAMANI |
MAHITAJI |
VILIVYOPO |
UPUNGUFU |
MADAWATI |
26389 |
32775 |
6387 |
MEZA |
2914 |
1719 |
1195 |
VITI |
3211 |
1692 |
1519 |
KABATI |
1714 |
523 |
1191 |
MAJENGO |
|
|
|
NYUMBA ZA WALIMU |
1463 |
368 |
1095 |
MADARASA |
1551 |
1298 |
253 |
VYOO |
2602 |
1599 |
1003 |
STOO |
370 |
93 |
277 |
OFISI |
372 |
295 |
77 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
2.4 Hali Ya Walimu Katika Shule Za Msingi:
Hali ya walimu ni kama ifuatavyo:-
Jedwali 2.3: Walimu wa Shule Za Msingi Kwa Madaraja
SIFA |
MAHITAJI |
WALIOPO |
PUNGUFU |
||
ME |
KE |
JML |
|||
DARAJA IIIA |
1999 |
558 |
846 |
1404 |
581 |
STASHAHADA |
7 |
7 |
14 |
||
SHAHADA |
0 |
0 |
0 |
||
JUMLA |
565 |
853 |
1418 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
Jedwali 2.4: Idadi Ya Walimu Katika Shule Za Msingi (Angalia Kiambatisho)
MAHITAJI |
WALIOPO |
ASILIMIA |
UPUNGUFU |
ASILIMIA |
1999 |
1418 |
70.9 |
581 |
29.1 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
2.5 Utoaji wa Chakula Shuleni
Idadi ya shule zinazotoa chakula katika wilaya Same ni 17 kati ya 185 shule hizo Nasuro, Daghaseta, Mughungani, Mkanyeni, Mwembe, Mshewa, Kafingiro, Goma, Kwizu Mrindi, Manka, Kweresha ,Kiomande, Parane, Ivuga, Mpinji na Tae.
2.6 Hali Ya Mimba
Hakuna taarifa ya mwanafunzi aliyepata mimba toka mwezi Januari hadi sasa
2.7 Changamoto Mbalimbambali Zilizopo
Shule za Msingi Wilaya ya Same zinakumbana na changamoto mbali mbali, ambazo zinasababisha ufaulu wa wanafunzi kuwa wa kiwango cha chini. Baadhi ya changamoto hizo ni :
o Uhaba wa nyumba za walimu katika maeneo ya shule.
o Kukosekana kwa chakula cha mchana kwa wanafunzi shuleni.
o Upungufu mkubwa wa Walimu.
o Upungufu wa rasilimali fedha na vifaa kwa ajili ya ufuatiliji utendaji kazi wa walimu
3.0 IDARA YA ELIMU SEKONDARI
3.1 Utangulizi
Halmashauri ya Wilaya ya Same ina jumla shule 51 za sekondari, kati ya shule hizo 36 ni za serikali na 15 ni za binafsi. Mwaka 2015 shule 47 za sekondari ndizo zilikuwa na watahiniwa wa shule wa Mtihani Taifa kidato cha nne. Shule moja ya Hedaru Sekondari haikufanikiwa kupata matokeo mpaka tathmini hii inafanyika kutokana na kutokuwasilisha nyaraka muhimu Baraza kwa wakati.
3.2 Idadi ya Wanafunzi, kabla na baada ya Uhakiki
Idadi ya Wanafunzi, kabla na baada ya Uhakiki ni kama ilivyoainishwa katika Majedwali hapa chini;
Jedwali 3.1: Idadi ya Wanafunzi kabla ya Uhakiki
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
Jedwali 3.2: Idadi ya Wanafunzi baada ya Uhakiki
IDADI YA WANAFUNZI ILIVYO MWEZI AGOSTI, 2016 BAADA YA UHAKIKI |
|
||||||||||||||||||||
KID I |
KID II |
KID III |
KID IV |
KID V |
KID VI |
JUMLA KUU |
|
||||||||||||||
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
|
2133 |
2553 |
4686 |
1748 |
2142 |
3890 |
1162 |
1293 |
2455 |
1568 |
1865 |
3433 |
438 |
0 |
438 |
459 |
0 |
459 |
7508 |
7853 |
15361 |
|
|
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
3.3 Hali ya Ufaulu Katika Mitihani ya Kitaifa
Watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 5044, kati yao wasichana ni 2816 na wavulana ni 2228.watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa ni 4958 na waliopata daraja la ufaulu kuanzia daraja I-IV ni 2809 sawa na asilimia 56.6 ya waliofanya mtihani huo, ambapo watahiniwa 2149 walifeli, sawa na asilimia 43.4. Aidha, ufaulu huu umeshuka kwa asilimia 1.6 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2014 ambapo ulikuwa ni asilimia 58.2.
Aidha, matokeo ya kidato cha pili, 2015, Watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa upimaji walikuwa 4977, kati yao watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 4720 sawa na aslimia 94.8 ya waliosajiliwa. Kati ya Watahiniwa 4720 waliofanya Mtihani wa upimaji wa Taifa kidato cha pili, Watahiniwa waliopata madaraja ya ufaulu walikuwa 3856 sawa na asilimia 82 ya waliofanya mtihani. Watahiniwa waliofeli walikuwa 864 sawa na asilimia 18 ya waliofanya mtihani.
3.2.1 Mchanganuo wa Ufaulu Kidato cha Nne
Kufuatia utaratibu ambao Baraza la Mitihani la Tanzania limetumia kutunuku matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne 2015 kwa kutumia madaraja ya ufaulu kama ilivyokuwa mwaka 2013 na kurudi nyuma, matokeo ya kila shule yameainishwa katika madaraja matano ambayo ni “daraja la kwanza, pili, tatu, nne na waliofeli. Ufaulu huo kimadaraja ni kama ifuatavyo;
Jedwali 3.3: Hali ya ufaulu kimadaraja
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
3. 2.2 Nafasi Ya Wilaya Kimkoa Na Kitaifa
Katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE) mwaka 2014 wilaya ilishika nafasi ya 96. Kwa mwaka 2015 wilaya imeshika nafasi 7 kati ya wilaya 7 kimkoa na nafasi ya 102 kitaifa. Aidha, katika mtihani wa upimaji wa kidato cha pili (FTNA) kwa mwaka 2014, wilaya ilishika nafasi ya 47, na mwaka 2015 wilaya imeshika nafasi ya 57.
3.3 Mikakati ya Kuinua Taaluma Kiwilaya
vi. Wakuu wa shule wameagizwa kushirikiana na waratibu Elimu Kata kudhibiti utoro wa wanafunzi ambao hawahudhurii masomo badala yake wanakuja siku za mitihani tu.
3.4 Hali ya Madarasa/ Vyoo/ Nyumba za Walimu/Maabara na Mikakati ya ukamilishaji
Kwa upande wa hali ya Madarasa, Vyoo na Nyumba za Walimu ni kama ilivyoainishwa katika jedwali lifuatalo;
Jedwali 3.4: Madarasa, Vyoo, Nyumba za Walimu
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
3.5 Idadi ya Walimu ukilinganisha na Ikama
Kwa upande wa Idati ya Walimu, tuna uhaba mkubwa kwa upande wa Walimu wa Masomo ya Sayansi ukilinganisha na Walimu wa Masomo ya sanaa ambao wapo wakutosha na baadhi ya masomo wamezidi. Mfano katika somo la Kiswahili kuna zidio la Walimu 32 na somo la Kingereza kuna zidio la Walimu 13 kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini;
Jedwali 3.5: Idadi ya Walimu Wanaohitajika, Waliopo na Pungufu kwa kila somo
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
3.6 Ukamilishaji wa Maabara
Idara imejitahidi kusimamia ujenzi wa maabara katika shule zote 36, kama ambavyo iliagizwa na Mh. Rais wa awamu iliyopita. Ambapo jumla ya vyumba vya maabara vilivyotakiwa ni 108. Kwa sasa vyumba ambavyo havijakamilika ni vinne (04), vyumba vilivyokamilika ni 104. Ambayo havijakamilika ni katika shule za sekondari Lugulu na Masheko ambazo zote ni shule mpya. Aidha katika baadhi ya shule samani za maabara hazijakamili pia bado kuna upungufu wa vifaa vya ufundishiaji na ujifunzaji kwa masomo ya sayansi.
3.7 Mikakati ya Ukamilishaji
Mikakati iliyopo katika kukamilisha ujenzi wa maabara hizo ni;
3.8 Utoaji Wa Chakula Cha Mchana Kwa Wanafunzi wa Kutwa
Hali ya utoaji chakula katika shule za kutwa za serikali kwa sasa siyo nzuri, baada ya tangazo la Elimu bila malipo ambapo shule zote za sekondari zilikuwa zinatoa chakula cha mchana. Aidha, kwasasa idadi ya wanafunzi wanaopata chakula cha mchana ni kama ifuatavyo; wanafunzi 8445 wanapata chakula na ambao hawapati chakula ni 6916.
Aidha, ofisi imepokea waraka wa Elimu Na. 3 wa mwaka 2016, ambao unawataka wajumbe wa bodi na wazazi kuhakikisha wanafunzi wote wa shule za sekondari za kutwa wanapata chakula cha mchana. Waraka huu umeshapelekwa shuleni kwa ajili ya utekelezaji. Kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 3.7 kamati / bodi za shule za serikali (iii) kushirikiana na wazazi/jamii kuweka utaratibu wa chakula cha mchana au chakula na huduma za hosteli katika shule za kutwa kulingana na mazingira yao, na kutuma mapendekezo kwa MkurugenziMtendaji wa Halmashauri.
3.9 Mikakati Ya Kudhibiti Utoro Na Mimba Shuleni
Hali ya utoro limekuwa tatizo sugu kwa baadhi ya wanafunzi, hii ni kutokana na baadhi ya wanafunzi kushiriki katika biashara za kuendesha boda boda na shughuli nyingine zinazofanywa na wazazi / walezi.
Kupitia vikao vya bodi, wazazi /walezi, jamii kutoa malezi mfungamano, basipo kuangalia na kubagua watoto ili kuboresha nidhamu na kuwajengea uwezo wa kujitambua kama sehemu ya jamii wanayoishi.
Jedwali 3.6: Taarifa za Wanafunzi Watoro, Waliopata Mimba, Waliohama Na Kuhamia pamoja na Wanaopata na Wasiopata Chakula
S/N |
SHULE |
MIMBA |
WATORO |
WALIOHAMA |
WALIOHAMIA |
WANAOPATA CHAKULA |
WASIOPATA CHAKULA |
|
||||||
|
||||||||||||||
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
|
|||||
1 |
BANGALALA |
4 |
6 |
7 |
13 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
106 |
81 |
|
2 |
BEMKO |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
408 |
0 |
|
3 |
BOMBO |
2 |
3 |
4 |
7 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
46 |
310 |
|
4 |
CHALAO |
3 |
3 |
2 |
5 |
2 |
3 |
|
3 |
0 |
3 |
539 |
0 |
|
5 |
CHANJAGAA |
1 |
3 |
5 |
8 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
100 |
112 |
|
6 |
GONJA |
3 |
27 |
9 |
36 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
835 |
|
7 |
KASEMPOMBE |
2 |
10 |
8 |
18 |
4 |
2 |
0 |
0 |
0 |
0 |
180 |
171 |
|
8 |
KAZITA |
3 |
3 |
2 |
5 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
183 |
0 |
|
9 |
KIBACHA |
2 |
13 |
15 |
28 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
765 |
0 |
|
10 |
KIGANGO |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
160 |
0 |
|
11 |
KIHURIO |
2 |
2 |
4 |
6 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
193 |
349 |
|
12 |
KIMALA |
1 |
7 |
9 |
16 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
491 |
0 |
|
13 |
KIRANGARE |
1 |
4 |
2 |
6 |
4 |
1 |
0 |
0 |
6 |
0 |
50 |
363 |
|
14 |
KISIWANI |
4 |
2 |
0 |
2 |
2 |
0 |
0 |
3 |
3 |
6 |
730 |
0 |
|
15 |
KWAKOKO |
4 |
7 |
10 |
17 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
405 |
0 |
|
16 |
KWIZU |
0 |
0 |
0 |
0 |
1 |
0 |
1 |
1 |
0 |
1 |
375 |
0 |
|
17 |
LUGULU |
3 |
2 |
2 |
4 |
13 |
26 |
39 |
11 |
18 |
29 |
78 |
124 |
|
18 |
MABILIONI |
1 |
2 |
1 |
3 |
2 |
7 |
9 |
2 |
16 |
18 |
140 |
306 |
|
19 |
MADIVENI |
1 |
11 |
18 |
29 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
300 |
0 |
|
20 |
MAKANYA |
1 |
13 |
6 |
19 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
497 |
0 |
|
21 |
MALINDI |
0 |
2 |
0 |
2 |
1 |
1 |
2 |
2 |
0 |
2 |
153 |
117 |
|
22 |
MASHEKO |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
130 |
75 |
|
23 |
MKOMBOZI |
3 |
22 |
0 |
22 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
48 |
1091 |
|
24 |
MOIPO |
1 |
23 |
12 |
35 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
219 |
143 |
|
25 |
MTII |
3 |
3 |
2 |
5 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
100 |
213 |
|
26 |
MVUREKONGEI |
4 |
2 |
3 |
5 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
184 |
|
27 |
MYAMBA |
0 |
1 |
0 |
1 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
245 |
321 |
|
28 |
NDUNGU |
3 |
4 |
0 |
4 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
687 |
|
29 |
NTENGA |
2 |
2 |
4 |
6 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
618 |
|
30 |
PARENI |
2 |
1 |
2 |
3 |
3 |
4 |
7 |
0 |
0 |
|
274 |
0 |
|
31 |
SAME |
0 |
2 |
0 |
2 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
756 |
0 |
|
32 |
SAWENI |
0 |
6 |
12 |
18 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
252 |
0 |
|
33 |
TAE |
0 |
6 |
8 |
14 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
145 |
72 |
|
34 |
VUDEE |
1 |
6 |
4 |
10 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
198 |
58 |
|
35 |
VUMARI |
0 |
7 |
8 |
15 |
6 |
4 |
10 |
4 |
5 |
9 |
96 |
459 |
|
36 |
VUNTA |
0 |
9 |
5 |
14 |
0 |
2 |
2 |
0 |
0 |
0 |
83 |
227 |
|
|
JUMLA |
57 |
214 |
164 |
378 |
38 |
50 |
88 |
26 |
48 |
68 |
8445 |
6916 |
|
4.0 IDARA YA MAJI
4.1 Upatikanaji wa Huduma ya maji
Upatikanaji wa maji vijijini ni 70% na Vijiji vyenye maji ni 75
4.2 Mpango uliopo kwa mji wa Same
Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe unalenga kuhudumia watu 456,931 ifikapo mwaka 2038 katika Wilaya za Same (watu 264,793), Mwanga (watu 177,085) na watu 15,053 katika Wilaya ya Korogwe, kwenye vijiji 38 na miji ya Same na Mwanga. Mifugo na viwanda vidogo pia vitanufaika na mradi huu.
Katika Vijiji 38 vitakavyonufaika Vijiji vya Same ni Hedaru, Mabilioni, Gavao, Makanya, Mgwasi, Bangalala, Chajo, Mwembe, Njoro, Ishinde, Ruvu Mferejini, Ruvu Jiungeni, Majengo, Bendera, Mkonga Ijinyu, Mgandu (vijiji 16 katika Wilaya ya Same)
4.3 Utekelezaji wa Mradi
ii. Awamu ya nne ambayo ni kulete maji katika Mji wa Same, Mkandarasi ameshapatikana, anaitwa Badri East Africa Limited na alishafika eneo la kazi kujitambulisha. Ataanza kazi mara baada ya kusaini Mkataba na kulipwa malipo ya awali. Pia ataweka kambi (Camp Site) maeneo ya Same Mjini na Kijiji cha Njoro. Gharama za awamu hii ni USD 52 milion sawa na shilingi 104 bilioni
5.0 KITENGO CHA ARDHI
Sekta ya ardhi ni mojawapo ya sekta iliyopo chini ya idara ya ardhi na maliasili inayosimamia masuala yote ya ardhi. Sekta ina sehemu 4 ambazo ni ardhi utawala, mipango miji, upimaji na ramani na uthamini. Idadi ya Vijiji vilivyopimiwa Ardhi, Idadi ya Vijiji vilivyofanyiwa Matumizi bora ya Ardhi, Idadi ya Migogoro Sugu ya Ardhi Mjini na Vijiji, Sababu za kutokea kwa Migogoro ya Ardhi na kusababisha migogoro hiyo kuwepo kwa muda mrefu, Mipango/Mikakati ya kumaliza Migogoro ya Ardhi, Mipango/Mikakati ya kuboresha Mji/Master plan, Hali ya Ukusanyaji wa Kodi za Viwanja na Nyumba pamoja na Idadi ya Miji yenye Sifa ya kuwa Miji Midogo ni kama ilivyoainishwa katika jedwali hapa chini;
Jedwali 5.1: Hali ya Utekelezaji wa Shughuli za Kitengo cha Ardhi
S/N |
VIJIJI VILIVYOPIMWA |
VIJIJI VILIVYOGAWANYIKA |
VIJIJI VYENYE MATUMIZI BORA YA ARDHI |
MIGOGORO SUGU |
MIGOGORO YA KAWAIDA |
SABABU ZA MIGOGORO |
MIKAKATI YA KUMALIZA MIGOGORO |
MIPANGO YA KUBORESHA MJI |
UKUSANYAJI WA KODI ZA ARDHI/MAJENGO |
MIJI YENYE SIFA YA KUWA MIJI MIDOGO |
1 |
Halmashauri ya Wilaya ya Same ina jumla ya vijiji 100 kati ya Vijiji hivyo vilivyopimwa vilikuwa ni vijiji 84, kati ya vilivyokuwa vimepimwa vijiji saba (7) vimegawanyika kati ya Vijiji hivyo sasa vilivyogawanyika vimezaliwa Vijiji 16 |
-Chajo kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Chajo na Nasuro. -Tae kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Tae, Heikonti na Rikweni. -Njoro kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Njoro na Emuguri. -Gavao Saweni kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Gavao Ngarito na Saweni. -Mabilioni kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Mabilioni, Ruvu mbuyuni na Chekereli.-Hedaru kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Hedaru, Kijomu na Gundusine. Bangalala kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Bangalala na Mkanyeni. |
Duma, Lugulu, Kanza na Mtii, Makanya, Hedaru na Gavao Saweni.
Kutokana na ufinyu wa bajeti Halmashauri imefanikiwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji saba (7) kupitia ufadhili wa wadau wa maendeleo kama TFCG na Ongawa. |
-Kijiji cha Makanya na Ruvu
- Kijiji cha Mgwasi na Makanya,
Kitongoji cha Kavambughu Ishinde.
-Maore na Mheza.
-Migogoro ya wakulima na wafugaji kata ya Ruvu. |
Migogoro ya kawaida haiwezi kuhesabika kwani huibuka na kupatiwa ufumbuzi.
Baadhi ya wananchi wanadai kuchukuliwa maeneo yao bila kulipwa fidia. |
Kukosewa mipaka ya vijiji katika ramani zilizopimwa na Wizara ya Ardhi Wananchi kujenga bila vibali vya ujenzi kutoka mamlaka husika. |
Kukagua vijiji vyenye migogoro ya mipaka na kuiandikia Wizara barua ili waje warekebishe mipaka hiyo. Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji.
Kubaini na kuhakiki uhalali wa madai ya wananchi ambao wanadai maeneo yao kuchukuliwa bila kulipwa fidia. Halmashauri kutafuta eneo kwa ajili ya kulipima ili kuwafidia wananchi hao. |
Maandalizi yanafanyika ili kutenga fedha katika bajeti ijayo ili kuandaa master plan (Mpango kamambe) wa mji wa Same. |
Ukusanyaji wa kodi za ardhi unaendelea vizuri. Kodi ya majengo ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo hukusanywa na mamlaka ya Mji mdogo wa Same kama mapato ya ndani. |
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ipo miji ya kibiashara ambayo inakuwa kwa kasi na ina sifa ya kuwa miji midogo ambayo ni Hedaru,
Makanya,
Kisiwani,
Maore na
Ndungu. |
Chanzo: Kitengo cha Ardhi
6.0 IDARA YA KILIMO
6.1 Eneo la Kilimo na Mazao yanayolimwa
Eneo linalofaa kwa shughuli za kilimo katika Wilaya ya Same linakadiriwa kuwa na jumla ya hekta 45,000. Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni takriban hekta 20,000 ambazo kati ya hizo ni hekta 12,200 zinazotumika kwa umwagiliaji wa kisasa na wa asili.
Fursa zilizopo Wilayani kwa ajili ya shughuli za kilimo ni pamoja na kuwa na bonde zuri lenye maji ya mito upande wa Same Mashariki ukanda wa tambarare. Eneo hili lina Skimu za umwagiliaji ambapo mazao mbalimbali ya chakula na biashara huzalishwa kama vile Mpunga, mahindi, maharage na mbogamboga. Upande wa Magharibi hutegemea zaidi Mto Pangani ambapo kuna kilimo cha umwagiliaji wa mazao ya mahindi, mpunga na mbogamboga. Upande huu ndio wenye eneo kubwa la malisho kwa upande wa ufugaji.
Mazao ya biashara yanayolimwa katika Wilaya yetu ni Tangawizi, Pamba, Fiwi na Kahawa, na Iliki. Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, mpunga na mtama. Mazao aina ya mikunde ni pamoja na maharage na fiwi, mazao mengine ni viazi vikuu, viazi mviringo na mihogo. Aidha Wilaya inazalisha pia aina kadhaa za mbogamboga na matunda ikiwemo ndizi, matango, tikitimaji, na nyanya.
6.2 Malengo ya Kilimo na Matarajio ya mavuno
Wilaya hii ni mojawapo ya Wilaya zinazokabiliwa na upungufu wa chakula mara kwa mara. Hali hii inasababishwa na mvua chache zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo huathiri ustawi wa mazao ya kilimo hasa maeneo ya tambarare.
Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017 halmashauri ya wilaya ya same imeweka malengo ya kulima hekta 39,700 ambapo kiasi cha tani 208,297 cha mazao mbalimbali kinatarajiwa kuzalishwa, ambapo tani 155,668 ni mazao ya chakula, tani 3,289 ni mazao ya biashara, tani 26,403 ni mbogamboga, tani 7,440 ni matunda na tani 15,506 ni Viungo.
Jedwali 6.1: Malengo ya kilimo na utekelezaji wa mazao muhimu
|
2015/2016 |
2016/2017 |
||||
LENGO |
UTEKELEZAJI |
LENGO |
||||
Ha |
Tani |
Ha |
Tani |
Ha |
Tani |
|
MAZAO YA CHAKULA |
||||||
Mahindi |
20,500 |
48,000 |
19,781 |
63,299 |
15,200 |
50,000 |
Mpunga |
3,200 |
19,200 |
3,300 |
16,500 |
3,200 |
24,000 |
Mtama |
500 |
500 |
100 |
80 |
500 |
800 |
Maharage |
1,500 |
1,320 |
1,250 |
1,100 |
1,500 |
1,400 |
Muhogo |
3,140 |
31,400 |
3,140 |
29,400 |
3,140 |
32,000 |
Ndizi |
3,200 |
32,000 |
3,200 |
31,100 |
3,200 |
32,000 |
Viazi Vitamu |
600 |
3,000 |
550 |
2,750 |
600 |
3,000 |
Viazi Mviringo |
350 |
3,500 |
300 |
3,000 |
350 |
3,500 |
JUMLA |
32,990 |
138,920 |
31,621 |
147,229 |
27,690 |
146,700 |
MAZAO YA BIASHARA |
||||||
Pamba |
80 |
120 |
50 |
60 |
80 |
120 |
Tangawizi |
1,200 |
13,500 |
1,250 |
14,500 |
1,350 |
15,500 |
Kahawa |
1,650 |
660 |
1,500 |
320 |
1,650 |
660 |
Fiwi |
4,000 |
8,000 |
3,500 |
5,250 |
4,200 |
8000 |
JUMLA |
6,930 |
22,280 |
6,300 |
20,130 |
7,280 |
24,280 |
Chanzo: Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
6.3 Hali ya Chakula na mikakati ya kumaliza njaa
Kwa mwaka 2015/16 hali ya chakula Wilayani Same ilikuwa ya kuridhisha kutokana na mvua kunyesha kiasi cha kutosha. Kimsingi mahitaji ya chakula (nafaka) kwa mwaka ni tani 81,101 ambapo kila mtu mzima anastahili kiasi kisichopungua gunia 3 za mahindi kwa mwaka, makadirio haya ni kutokana na idadi ya watu iliyopo ndani ya Wilaya (Watu 269,807), na hii ni kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Uzalishaji wa chakula katika maeneo ya skimu za umwagiliaji za Ndungu, Maore, Kisiwani na sehemu za Kata ya Bendera nao umeongezeka kutokana na jitihada kubwa zilizofanyika za kuongeza uzalishaji katika maeneo ya umwagiliaji.
6.4 Mipango ya Wilaya wa kuongeza uzalishaji na kabiliana na upungufu wa chakula
· Kuhakikisha elimu ya uvunaji maji ya mvua, matumizi bora ya maji na hifadhi ya ardhi na udongo imetolewa kwa wakulima.
· Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuzuia/kupunguza upotevu wa
mazao ya nafaka na mikunde wakati wa kuvuna na kuhifadhi
(Post harvest loss handling).
· Kuhakikisha elimu ya ukadiriaji wa mahitaji ya mazao ya chakula kwa wakulima ngazi ya kaya imetolewa.
· Kutoa elimu kwa wakulima juu ya hifadhi na matumizi bora ya mazao ya chakula kwa maeneo ambayo yamepata mavuno mazuri msimu wa vuli hasa maeneo ya kilimo cha umwagiliaji.
· Kutoa ushauri kwa wakulima kutekeleza kilimo cha mazaoyanayostahimili ukame na yanayotumia kiasi kidogo cha unyevu hadi kukomaa kama mazao jamii ya mizizi na mikunde na Mtama.
· Kuhakikisha uimarishaji wa matumizi bora ya maji katika miundombinu ya umwagiliaji iliyopo na kuhakikisha kunakuwepo na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula kwa misimu miwili na wakulima wanazingatia ushauri wa wataalam waliopo vijijini.
· Kwa kuwatumia Maafisa Ugani waliopo kuhakikisha wakulima wanatumia teknolojia bora na sahihi za uzalishaji mazao ya chakula na biashara kwa ajili ya uhakika na usalama wa chakula ngazi ya kaya.
· Kuhimiza wafugaji walio na mifugo kuuza wakati bado ikiwa na hali nzuri ya kiafya na kununua chakula na kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia.
· Kuhimiza wakulima waliopo maeneo ya umwagiliaji kulima mazao yenye thamani na ubora kwa uhakika wa kuongeza kipato hatimaye kumudu kujinunulia chakula cha kutosha.
· Kuhamasisha wafanyabiashara wenye uwezo kununua chakula Katika maeneo yenye chakula cha ziada na kuleta kuuza katika maeneo yenye upungufu kwa bei nafuu/elekezi.
6.5 Mikakati ya mnyororo wa thamani wa mazao
Halmashauri ya Wilaya iliteua kuendeleza mnyororo wa thamani kwa mazao mawili ya biashara ambayo ni Tangawizi na Mpunga.
Kwa zao la tangawizi Halamashauri ikishirikia na wadau wengine imekuwa na mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya umwagiliaji katika maeneo yanayozalisha tangawizi ili kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa zao hilo. Vilevile kwa kupitia mradi wa MIVARF Halmashauri imekuwa na mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya mawasiliano katika maeneo yanayolimwa zao hilo, pia kujengea uwezo wakulima wa tangawizi kwa kuwapa mafunzo ya kilimo bora cha tangawizi na kuwaunganisha na masoko.
Kwa zao la mpunga Halmashauri imekua na mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya umwagiliaji katika maeneo yanayolimwa mpunga na kutoa mafunzo kwa wakulima wa mpunga kwa kuanzisha mashamba ya mfano na mashamba darasa. Aidha Halmashauri imekua na mikakati ya kufufua na kuhakikisha kinu cha kukoboa mpunga katika skimu ya Ndungu kinafanya kazi ili kuongeza thamani ya zao la mpunga.
6.6 Uendelezaji viwanda
6.6.1 Kiwanda cha Tangawizi
Wilaya ya Same ni miongoni mwa Wilaya zinazozalisha Tangawizi kwa wingi hapa nchini, ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya tani 14,500 zinazalishwa kila mwaka. Wakulima wengi hasa wa maeneo ya milimani hutegemea na kutumia zao hili kama zao la biashara. Kutokana na hali hiyo Ushirika wa wakulima wa Tangawizi Mamba Myamba uliamua kujenga kiwanda ili kuongeza thamani ya zao la Tangawizi. Kiwanda kilizinduliwa na Mhe. Rais Mstaafu mnamo mwaka 2012. Baada ya kuzinduliwa kiwanda kiliweza kusindika zaidi ya tani 100 za Tangawizi na kuziuza.
Katika uendeshaji baadhi ya mitambo ilieonekana kutofanya kazi vizuri na hivyo kuhitaji kuboreshwa. Hali hii ilipelekea kiwanda kusimama kwa muda na hivyo Shirika la SIDO wametakiwa kutengeneza na kuirekebisha mitambo hiyo. SIDO ndio waliosanifu na kutengeneza mitambo yote ya kiwanda hicho na wanaendelea kushirikiana na ushirika pale mitambo inapoleta hitilafu.
Soko la Tangawizi mbichi na iliyosindikwa lipo la kutosha nje na ndani ya nchi. Serikali kupitia Mradi wa uboreshaji miundo mbinu ya masoko na uongezaji thamani (MIVARF) kwa kushirikiana na Shirika la Faida Mali inaendelea kusaidia ushirika huo kutafuta na kuwaunganisha na masoko ya uhakika. Tayari masoko yafuatayo yameshapatikana Kampuni ya Afri Tea, kampuni ya Tausi, TAQWA, Kampuni ya India market na Kampuni ya lion wattle. Wanunuzi waliopatikana wapo tayari kununua tangawizi iliyosindikwa mara tu kiwanda kitakapoanza tena kufanya kazi.Kwa sasa bei ya Tangawizi ni Tshs. 1300 – 1500 kwa kilo ya tangawizi mbichi.
Zipo Changamoto za msingi zinazokabili ushirika kwa sasa, ambazo zinasababisha kiwanda kisifanye kazi vizuri. Changamoto hizo ni pamoja Uelewa mdogowa viongozi wa ushirika waliopo kwa sasa juu ya usimamizi na uendeshaji wa kiwanda, na Ukosefu wa mtaji wa kutosha kununua malighafi (Tangawizimbichi) kuajiri na kulipa watumishi na kulipia gharama za uendeshaji.
Hatua zinaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha kiwanda kinafanya kazi vizuri. Hatua hizo ni pamoja na Kuimarisha na kujengea uwezo viongozi wa ushirika na wanachama ili kuweza kujipanga na kuepuka bei zisizokuwa na maslahi zinazopangwa na wafanyabiashara. Aidha mafunzo yametolewa juu ya usimamizi na utunzaji wa fedha ili baada ya kuwa na uelewa wa kutosha waweze kuomba na kupata mkopo kutoka kwenye taasisi za fedha na hatimaye kuendesha kiwanda.
7.0 KITENGO CHA MALIASILI NA MAZINGIRA
7.1 Maliasili zilizopo Wilayani
7.1.1 Misitu Iliyopo
Wilaya ya Same ina jumla ya hakari 256,503 za misitu ambayo ni sawa na asilimia 20.3 (20.3%) ya eneo lote la Wilaya ya Same ambalo ni Kilomita za mraba 5,186 (5,186Km2). Misitu hii ni ya aina mbalimbali kama kama misitu ya Kupandwa, Mataji wazi (Miombo Woodland), Hifadhi za Serikali (Cathment Forests), Hifadhi za Vijiji na Hifadhi za kimila (Itasio).
7.1.2 Wanyamapori
Kitengo cha wanyamapori kina dhamana ya kuhifadhi rasilimali wanyamapori iliyoko kwenye maeneo ya wazi yenye wanyamapori kama vile Ruvu, kuwarudisha wanyamapori watoka nje ya na hifadhi ya taifa ya Mkomazi. Maeneo yaliyohifadhiwa yanachangia uhifadhi wa bioanuai mbalimbali ili zisitoweke kama vile tembo, nyani, kiboko, nyati, simba, mbwa mwitu pamoja na aina mbalimbali za ndege.
7.2 Utunzaji wa Maliasili zilizopo Wilayani
Wilaya ya Same ina jumla ya Misitu ya Hifadhi 17 ambayo kati ya misitu hiyo, Misitu minne (4) ipo chini ya Serikali kuu, Misitu tisa (9) chini ya Halmashauri na Misitu (4) ipo chini ya Vijiji.
Usimamzi wake unategemea na mmiliki ambapo Misitu ya Serikali kuu husimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Misitu ya halmashauri husimiwa na Halmashauri ya Wilaya kupitia Kitengo cha Maliasili na Misitu ya Vijiji inasimamiwa na Vijiji kupitia Kamati za Maliasili za Vijiji. Misitu hii husimamiwa kupitia mipango ya usimamizi ya misitu husika ambapo shughuli za Doria, Upandaji wa Misitu, kulinda mipaka ya hifadhi na kuzuia matukio ya moto hufanyika.
Kitengo hiki kinatunza rasilimali wanyamapori kwa kuwalinda dhidi ya majangili kwa kufanya doria mara kwa mara kwenye maeneo yenye wanyamapori ili kuwalinda dhidi na ujangili. Rasilimali hii pia inatunzwa kwa kuhakikisha kuna udhibiti na usimamizi wa umilikaji wa nyara kama vile kutoa kibali kwenye ukamataji wa ndege kama vile kanga.
Endapo wanyamapori watatoka nje ya hifadhi ya taifa ya Mkomazi au maeneo ya wazi na kwenda kwenye makazi na mashamba ya wananchi, ni jukumu la watumishi wa kitengo cha wanyamapori kuwarudisha kwenye hifadhi.
Pia hufanyika udhibiti wa wanyamapori waharibifu hususani viboko ambao huvamia maeneo ya wananchi na wakati mwingine kusababisha vifo au madhara kwa watu na mazao mashambani kwa kuwarudisha katika makazi yao. Aidha kumekuwa pia na udhibiti wa wanyamapori kama tembo na simba wanaotoka katika hifadhi ya taifa Mkomazi. Zoezi la kuwarudisha hifadhini hufanyika haraka iwezekanavyo ili wasilete madhara kwa wananchi na mali zao. Viongozi wa kata au vijiji husika huimizwa kutoa taarifa pindi wanyamapori hao watakapoonekana katika maeneo yao. Pia elimu dhidi ya kujikinga na wanyamapori hao hatari kwa mali na uhai wa wananchi hutolewa kwa wananchi ili kuwasaidia katika kujikinga na wanyamapori hao na kutoa taarifa katika Idara ya Ardhi na Maliasili.
7.3 Jinsi Maliasili zilizopo Wilayani zinavyochangia Uchumi
Misitu huchangia uchumi kupitia mapato yanayokusanywa na Halmashauri ya Wilaya na Serikali kuu kutokana na tozo mbalimbali za mazao ya misitu na mazao yasiyo ya misitu lakini yanayopatikana ndani ya misitu mfani ukindu. Tozo zinazokusanywa na Halmashauri ni zile zitokanazo na mbao, nguzo za umeme, simu na za kujengea, magome ya miti na mizizi kwa ajili ya dawa mbalimbali. Tozo zinazokusanywa na Serikali kuu ni zile za Usajili wa Biashara ya mazao ya misitu, kibali cha kusafirishia mazao ya misitu (Transit Pass) na mrahaba wa mazao ya misitu yaliyovunwa katika misitu ya asili.
Rasilimali hii inachangia kwenye uchumi kwa kutoa kibali cha ukamaji wa wanyamapori kama vile ndege aina ya kanga kwenye maeneo ya wazi yanayopatikana katika ya wilaya Same. . Kibali hicho kinatolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Wanyamapori na kuidhinishwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori na kumtaka Afisa Wanyamapori wa wilaya kumruhusu mdau huyo kukamata wanyama walioidhinishwa. Fungu la fedha lililotokana na ukamataji wa wanyamapori hao hugawiwa kwa Halmashauri husika.
Hata hivyo maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi kama vile Pori Tengefu (Ruvu-Same Game Controlled Area) yanakabiliwa na uharibifu mkubwa kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile uvamizi wa mifugo na shughuli za kilimo na ujangili kwenye maeneo yaliyohifadhiwa hivyo kusababisha kutokuwepo na wanyama wa kutosha kwa ajili ya shughuli za uwindaji ambazo zingeweza kuiletea halmashauri pato.
7.4 Upandaji wa Miti
Upandaji wa miti hufanyika kwa kuzingatia lengo la mwaka liliowekwa kwa kila Wilaya ambapo kwa Wilaya ya Same lengo la mwaka 2015/2016 lilikuwa ni kupanda miti 1,500,000.
Aidha pamoja na zoezi la upandaji wa miti, uhamaishaji wa uanzishaji wa vitalu vya miti hufanyika kwa jamii ili kupata vyanzo vya miche kwa ajili ya kupanda. Mpaka sasa jumla ya vitalu vya miti 35 vimeanzishwa na jamii katika Kata za Hedaru, Vunta, Makanya, Maore, Kisiwani, Vumari, Mtii, Bombo na Myamba. Kitalu cha Halmashauri kilichopo Mwembe kina jumla ya miti 9,780. Jumla ya miti 1,351,763 imeshapandwa mpaka sasa ndani ya Wilaya kati ya miti 1,500,000 iliyotarajiwa kupandwa kwa Mwaka 2015/2016 sawa na asilimia 90.01 (90.01%).
8.0 IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI/RASILIMALI WATU
8.1 Idadi ya Watumishi waliopo kulingana na Ikama
8.2 Taarifa ya Watumishi Hewa
8.3 Kiasi cha Fedha zilizopoyea kutokana na Watumishi Hewa
8.4 Mikakati/Hatua zilizochukuliwa ili kurejesha Fedha zilizopotea kutokana na Watumishi Hewa
8.5 Matatizo ya Watumishi na Namna Yanavyoshughulikiwa
Tangu January 2016 hadi sasa kuna jumla ya Matatizo ya Watumishi...........yaliyoshughulikiwa na matatizo.......... yanaendelea kushughulikiwa
8.6 Hali ya Vikao vya Kisheria Ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji na Hatua za kuvisimamia
8.7 Hatua zinazochukuliwa kwa kutofanya Vikao
8.8 Motisha zilizopo kwa Watumishi/ Viongozi
8.9 Utowaji wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watumishi /Viongozi
8.10 Zana za Ufuatiliaji Watumishi kwa kila Idara
Ø KITENGO CHA SHERIA
8.1 Idadi ya Kesi
Halmashauri ya Wilaya ya Same kama zilivyo Taasisi nyingine za kisheria ina uwezo wa kushitaki na kushitakiwa na katika kipindi cha 2015 hadi 2016 imekuwa na mashauri mbali mbali katika Mahakama ya Wilaya, Mahakama Kuu na Baraza la Ardhi na Nyumba Same.
· Katika kipindi cha 2015 hadi 2016 Halmashauri imefungua kesi mbili moja Baraza la Ardhi na Nyumba Same ambayo ni shauri la Madai kati ya Mamlaka ya Mji Mdogo Same dhidi ya Helios Tower Infanco Tanzania Ltd na Mahakama Kuu Moshi ya Halmashauri ya Wilaya dhidi ya Eliwaha Mbaga na Wenzake. Kesi hizi ziko katika hatua za awali.
Katika kipindi cha 2015 hadi 2016 Halmashauri imeshitakiwa katika Mahakama ya Wilaya, Mahakama Kuu na Baraza la Ardhi na Nyumba Same na jumla ya mashauri matano(5) yalifunguliwa dhidi yake. Mashauri dhidi ya Halmashauri ni ya Eiza Mkaze dhidi ya Halmashauri na Mwingine, Ramadhani Kanyama Msuya dhidi ya Halmashauri, Christina Elieskia na Miriam Kajiru dhidi ya Mkutugenzi Mtendaji Wilaya, Cheavo Johnson Kihara dhidi ya TANESCO na Halmashauri ya Wilaya na Octavius Leole dhidi ya Halmashauri ya Wilaya. Kesi hizi bado ziko kwenye hatua mbalambali za usikilizwaji na ya Christina na mwenzake imeamuliwa kwa njia ya usulihishi CMA na imerudishwa TSC kwa hatua zaidi
8.2 Mikakati ya kushinda Kesi na kuhakikisha Mikataba inakuwa na Tija kwa Halmashauri na Serikali
Halmashauri ya Wilaya ya Same kupitia Kitengo cha Sheria imejipanga kushinda katika kesi zote kwa kuhudhuria Mahakamani kufuatana na kalenda za Mahakama na kutoa ushahidi thabiti kwa mujibu wa sheria pia kushawishi utatuzi wa migogoro nje ya mahakama pale inapobidi kufanya hivyo ili kuepuka upotevu wa muda na rasilimali fedha.
Kitengo cha Sheria kinashughulika na uandaaji wa mikataba mbalimbali baina ya Halmashauri na wadau wake na vilavile kuandaa mikataba ya watumishi walioruhusiwa kwenda masomoni.
Katika hili Kitengo kinazingatia kanuni,taratibu na sheria za mikataba ili kuhakikisha kwamba mikataba yote inayiongiwa na Halmashauri ina tija kwa Serikali,wananchi na Halmashauri kwa ujumla.
8.3 Sheria Ndogondogo
Katika kipindi cha 2015 hadi 2016 Halmashauri kupitia Kitengo cha Sheria imeweza kuanda Sheria Ndogo 7 zitakazo saidia utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri katika kuhudumia wananchi wa Wilaya ya Same. Sheria hizo ni Sheria Ndogo za Ushuru wa Mabasi Stendi, Sheria Ndogo ya Kudhibiti Unywaji Holela wa Vileo, Sheria Ndogo za Ushuru wa Pumba za Nafaka, Sheria Ndogo ya Kilimo cha Mazao yanayohimili Ukame, Sheria Ndogo ya Mahudhurio ya Lazima kwa Shule za Msingi na Sekondari, Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni na Sheria Ndogo ya Kuzuia Ujazaji wa Lumbesa.
Katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na jamii ya watu walio sawa na huru, Halmashauri ya Wilaya ya Same inashirikiana na Taasisi zisizo za kiserikali katika kutoa msaada wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii katika wilaya ya Same.
IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
.1 Mambo ya kufanya ili kuhakikisha Jamii inapata Maendeleo
Kinachofanyika na kinachotarajiwa kufanyika ili kuhakikisha jamii inapata maendeleo ni;
.2 Idadi ya Vikundi vyenye Nguvu
Idadi ya vikundi vilivyopata usajili na vyenye nguvu ya kuweza kupata mikopon katika taasisi za kifedha ni kama ilivyoanishwa hapa chini;
Jedwali 5.1 Idadi ya Vikundi vyenye Nguvu
AINA YA KIKUNDI |
VIKUNDI VYA VIJANA |
VIKUDI VYA WANAWAKE |
VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI |
IDADI |
387 |
678 |
475 |
Chanzo: Idara ya Maendeleo ya Jamii
Jedwali 5.2: Idadi ya Vijana wasio na Kazi Maalum
WANAWAKE |
WANAUME |
JUMA YA VIJANA WASIOKUWA NAKAZI |
246 |
223 |
469 |
Chanzo: Idara ya Maendeleo ya Jamii
.3 Mikakati ya Kuwaendeleza Vijana
v Kuwahamasisha vijana ili waweze kujiunga na masomo ya ufundi stadi kv uashi useremala na ujenzi ili waweze kujiajiri
v Kwahamasisha vijana kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe mkopo yenye mashariti nafuu
v Kuwahamasisha vijana ili wajiunge kwenye makundi kwa ajili ya kupatiwa elimu juu ya ujasiriamali
v Kuwatengea vijana maeneo maalum kwa ajili ya kufanyia biashara ndogo ndogo
v Kuwahamasisha vijana kutumia elimu mbalimbali katika kuanzisha ufugaji wa kuku na n g”ombe wa maziwa na nyama
v Kuhamasiha vijana ili waweze kuanzisha viwanda vidovidogo kv, useremala uashi na ufndi vyuma.
5. Idadi ya SACCOS/Vikoba
Idadi ya SACCOS na Vikoba ni kama ifuatavyo;
Jedwali 5.3: Idadi ya SACCOS/Vikoba
S/N |
JINA LA SACCOS |
KATA/ENEO |
MMILIKI |
1 |
SAME KAYA SACCOS |
WILAYA |
WANANCHI/WANACHAMA |
2 |
SAME TEACHERS SACCOS |
WILAYA |
WAALIMU WANACHAMA |
3 |
KISIWANI SACCOS |
KISIWANI |
WANACHAMA |
4 |
MKONAPA SACCOS |
VUMARI |
WAFANYAKAZI/WANACHAMA |
5 |
NASHENGENA SACCOS |
MAORE |
WANACHAMA. |
6 |
KURUGENZI SACCOS |
WILAYA |
WAFANYAKAZI |
7 |
MARANATHA SACCOS |
SAME |
WAUMINI WASABATO |
8 |
GAHENDU |
SAWENI |
WANACHAMA WA GAVAO, HEDARU, GUNDU. |
Chanzo: Idara ya Maendeleo ya Jamii
o Fedha za Vikundi toka Halmashauri katika bajeti ya 2015/2016 zilizopangwa, Kiasi cha Fedha kilichotolewa na Idadi ya Vikundi vilivyopewa
Fedha zilizopangwa kutolewa na Halimashauri kwa kipindi cha 2015/16 ni jumla ya TShs. 112,000,000/= na zilizotolewa ni Tshs. 26,000,000/= na idadi ya vikundi vilivyopatiwa mikopo ni 14.
o Fedha zilizopangwa katika Bajeti ya 2016/2017
Kwa upande wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017, Fedha zilipangwa kutolewa kwa kipindi cha 2016/17 ni Tsh. 146,000,000/=
6. KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
o Idadi ya Hoja za Ukaguzi
Kwa kipindi kinachoishia mwezi Agosti, 2016, Halmashauri ilikuwa na hoja za ukaguzi 54 zinazohitaji majibu yatakayopelekea hoja hizo kufungwa.
o Mikakati ya kupunguza Hoja za Ukaguzi
Uongozi wa halmashauri umeweka mikakati ili kupunguza hoja za ukaguzi, mikakati hiyo ni:-
I. Kutumia mashine za elektroniki zinazowasiliana na makao makuu ya halmashauri kukusanyia mapato toka katika Kata, itasaidia kuhakikisha mapato yote yaliyokusanywa kufahamika na kuwasilishwa na kuondoa tatizo la upotevu/kutokuwasilishwa wa vitabu vya kukusanyia mapato
II. Kuendelea kuwasiliana na TAMISEMI , ili kuweza kupata wakuu wa Idara/au kuwathibitisha makaimu wakuu wa idara waliopo, hii itasaidia kupunguza madeni kwa wakuu wa idara wanaokaimu kwa muda mrefu
III. Kuendelea kufuatilia uwepo wa watumishi hewa kwa kufanya uhakiki wa watumishi kila mwezi
IV. Kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuibua vyanzo vipya vya mapato ya ndani , na kuendelea kuwasiliana na Hazina /Serikali kuu ili iweze kuleta fedha kwa wakati kulingana na bajeti , hii itasaidia halmashauri kutekeleza kazi kulingana na bajeti na kuwa na uwezo wa kupeleka asilimia 10 ya mapato ya ndani yaliyokusanywa katika mfuko wa wanawake na vijana
V. Kuendelea kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo ambazo hazijawasilishwa toka Hazina na kuomba fedha hizo kuwasilishwa kwa wakati
VI. Kutenganisha thamani ya majengo na ardhi kwa kufanya uthaminishaji
VII. Kuwaelekeza wakuu wa Idara/vitengo/watumishi kutekeleza majukumu kwa kufuata taratibu na sheria
VIII. Kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani katika usimamizi wa fedha/manunuzi/ubora
IX. Kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika mapema mara fedha zinapowasili
X. Kuimarisha Kitengo cha ukaguzi wa ndani kwa kuwajengea uwezo katika mifumo, mfano, mfumo wa ukusanyaji wa mapato kielektronic, LAWSON, EPICOR, PLAN REP.
o Changamoto zinazosababisha kutokuisha kwa Hoja za Ukaguzi
I. Upungufu wa mkaguzi mmoja kulingana na Ikama
II. Kukosekana/kutokuwasilishwa kwa fedha , kumepelekea kaguzi kutofanyika kulingana na mpango wa ukaguzi wa mwaka
XI. Wakaguzi kutokujengewa uwezo kuhusiana na mifumo ya ukusanyaji wa mapato kielektronic, LAWSON, EPICOR, PLAN REP
7. IDARA YA UJENZI
o Idadi ya Miradi inayoendelea kutekelezwa
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 idara ya ujenzi ilitengewa kiasi cha Tshs 956,160, 000/= kutoka mfuko wa barabara (Road fund) hadi kufikia 30/06/2016 halmashauri imepokea kiasi cha Tsh 215,460, 000/= tu. Miradi inayoendelea kutekelezwa kwa kazi za barabara ni kama ifuatavyo:-
Jedwali 11.1: Idadi ya Miradi inayoendelea kutekelezwa
Na. |
Jina la mradi |
Jina la Mkandarasi |
Gharama ya Mkataba |
Maoni |
1 |
Matengenezo ya kawaida na muda maalumu barabara za Makanya – Chankoko na Njia panda – Chankoko - Mvungwe |
OLDONYOMAS ENGINEERING |
105,577,550 |
Kazi zinaendelea |
2. |
Matengenezo ya kawaida muda maalumu na miundo mbinu ya maji barabara za Mpirani -Kadando,Maore- Vuje,Ndungu-Makokane na Mpirani-Bombo |
CORNEL (T) LTD |
88,030,950 |
Kazi zinaendelea |
3. |
Matengenezo ya kawaida, sehemu korofi na matengenezo ya muda maalumu barabara za Same -Ruvu-Mferejini na Ishinde-Vumari. |
CORNEL (T) LTD |
77,881,180 |
Kazi zinaendelea |
4. |
Matengenezo ya kawaida,sehemu korofi na miundombinu ya maji ya mvua barabara za Kisiwani -Msindo,Mwembe- Mhezi,Mbuyuni-Marindi na Ijinyu - Kamadufa |
MUGENZO CO. LTD |
64,431,540 |
Kazi zinaendelea |
5. |
Matengenezo ya kawaida na sehemu korofi barabara za Saweni-Gavao -Bwambo,Kidenge- Mwala na Hedaru- Makasa-Kirangare |
HAMORIC INVESTMENT (T) LTD |
34,499,660 |
Kazi zinaendelea |
6 |
Matengenezo ya kawaida na miundombinu ya maji barabara za Majevu-Dido- Njoro, Minyala -Mbono-Mgagao na dengude- Dido. |
KIV CO.LTD |
70,825,960 |
Kazi zinaendelea |
7 |
Matengenezo ya kawaida muda maalumu na miundo mbinu ya maji barabara za Same Mjini. |
SIMJO TECH CO.LTD |
128,118,500 |
Kazi zinaendelea |
8 |
Matengenezo ya kawaida na sehemu korofi barabara za Bangalala -Chome na Chome - Ikokoa |
MSHUNGA INVESTMENT LTD |
22,774,000 |
Kazi zinaendelea |
Chanzo: Idara ya Ujenzi
11.2 Ubora wa Miradi inayotekelezwa.
Miradi inayotekelezwa ipo katika ubora unaotakiwa kwa kuzingatia taratibu za mikataba.
11.3 Uhakiki kwa Wakandarasi wanaopatiwa Kazi/Tenda
Uhakiki wa wakandarasi wanaopatiwa kazi/tenda hufanyika kipindi cha kufanyiwa uchambuzi wa zabuni (Tender evaluation) wa wazabuni wanapoomba tenda/zabuni.
11.4 Ubora na Muda wa Ukamilishaji wa Miradi
Ubora wa kazi unazingatiwa na Mkandarasi kam hajakamilisha kazi kwa wakati anapata adhabu ya kuchelewesha kazi (liquidated damages)
11.5 Idadi ya Miradi ambayo haikukamilika kwa Wakati na sababu zilizopelekea
Miradi yote haijakamilika kwa wakati kutokana na kuchelewa kupokea fedha kutoka serikali kuu. (Mfuko wa barabara)
11.6 Hali na urefu wa Mtandao wa Barabara
Hadi kufikia mwezi Juni mwaka 2016 Halmashauri ya wilaya ya Same ina mtandao wa Barabara wenye Jumla ya 668.63 Km zinazofanyiwa matengenezo kwa usimamizi wa Halmashauri kupitia kitengo cha barabara. Kati ya barabara hizo 0.8Km ni za lami ambazo zipo Same mjini,128 Km ni za changarawe na 539.83 Km ni za udongo.Asilimia 85 ya barabara ziko milimani na asilimia 15 ni za tambarare.
8. IDARA YA FEDHA
12.1 Utangulizi
Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa mwaka wa fedha 2015/2016 iliidhinishiwa kupokea fedha Tshs. 43,351,398,248 hadi kufikia Juni 2016 ilikuwa imepokea Tshs. 41,467,376,632 sawa na asilimia 95.
Jedwali hapo chini linaonyesha vyanzo vya Halmashauri, Makadirio, hali halisi, asilimia, utekelezaji na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti hiyo kama ifuatavyo:-
Jedwali 12.I: Bajeti ya Halmashauri 2015/2016
Na. |
Vyanzo vya Halmashauri |
Makadirio |
Hali halisi ya makusanyo ya Fedha |
Asilimia |
Utekelezaji |
Changamoto |
1. |
Vyanzo vya ndani |
2,274,732,000 |
1,933,320,538 |
85 |
Fedha za mapato ya ndani zimechangia miradi ya maendeleo;- Mchango wa madawati Tshs. 212,021,051 Kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa maabara na ununuzi wa vifaa vya maabara Tshs. 37,810,000 Kuwezesha unununzi wa kipaza sauti ukumbi wa Halmashauri Tshs. 4,613,400 Ukamilishaji wa kituo cha kilimo Tshs. 5,600,000 Kuchangia ujenzi wa ofisi mpya ya Mkurugenzi Tshs. 30,000,000 Kuchangia ukarabati wa shule za msingi Tshs. 10,000,000 Kufunga mfumo wa kieletronic Tshs. 75,417,808 Kuchangia mfuko wanawake na Vijana Tshs. 22,150,360 na Uendeshaji wa shughuli za ofisi vikao na ulipaji wa mishahara kwa watumish wanaolipwa na mapato ya ndani. |
-Mwamko mdogo wa wananchi kulipa kodi na ushuru. -Baadhi ya Vijiji kutokuwa na Maafisa watendaji Vijiji. -Shughuli za uchaguzi Mkuu -Mabasi kutoingia stand. |
2. |
Fidia ya vyanzo vilivyofutwa |
200,023,000 |
31,977,000 |
16 |
Shughuli za uendeshaji wa ofisi zilifanyika kulingana na fedha iliyotolewa. |
Fedha kuto kutolewa kulingana na Bajeti. |
3. |
Serikali kuu - Ruzuku – OC |
2,327,258,000 |
1,769,377,000 |
76 |
Idara ilitekeleza shughuli zilizopangwa kutokana na fedha zilizopokelewa |
Fedha kutopokelewa kwa wakati. Fedha kuto kutolewa kulingana na Bajeti. |
4. |
Mishahara |
32,612,236,000 |
31,899,123,217 |
98 |
Mishahara ililipwa kwa Watumishi kwa wakati |
Madeni ya Malimbikizo ya mapunjo ya mishahara. |
5. |
Miradi ya maendeleo.
- EGPAF - EASTERN ARC - MIVAF - TANAPA - Performance For Result (P4R) - Ujenzi / Uboreshaji Miundombinu- Kibacha - TASAF |
3,177,944,465
239,474,300
15,400,000 21,300,000
18,000,000 72,377,209
221,902,836
2,170,750,438
|
3,147,136,623
166,711,771
15,400,000 21,300,000
18,000,000 72,377,209
221,902,836
2,170,750,438 |
99
70
100 100
100 100
100
100 |
Utekelezaji wa miradi umefanyika kulingana na fedha iliyotolewa na lengo lililokusudiwa |
Kuchelewa kupokea fedha kwa wakati. |
|
Jumla |
43,351,398,248 |
41,467,376,632 |
95 |
|
|
Jedwali 12.2: Bajeti ya Halmashauri 2016/2017
Vyanvo |
Makadirio |
Mikakati ya kufikia malengo |
Vyanzo vya ndani |
2,335,264,000 |
- Kuhakikisha Takwimu na Bajeti za Mapato zinaandaliwa kutoka kwenye kila Kijiji pia itawezesha Kijiji kuwa na makadirio ya asilimia 20 itakayorejeshwa Kijijini. - Kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na malengo ya kukusanya mapato - Kuhakikisha kila Kata inakuwa na machine ya kukusanyia mapato. - Kuhakikisha kuna kuwa na ufatiliaji wa mara kwa mara wa mapato na ufatiliaji wa kushtukiza - Kubuni vyanzo vipya vya mapato - Kuendelea kutoa elimu kwa walipa kodi na ushuru ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na ushuru. - Kuendelea kufatilia mikakati iliyowekwa na kufanya tathmini.. |
Fidia ya vyanzo vilivyofutwa |
192,362,000 |
- |
Serikali kuu - Ruzuku – OC |
3,245,916,850 |
- |
Mishahara |
39,475,823,940 |
- |
Miradi ya maendeleo
|
11,251,205,280 |
- |
JUMLA |
56,500,572,071 |
|
12.2 Halmashauri inakusanya mapato Kwa njia ya kieletroniki Na kupitia mfumo WA LGRCIS ambao umeunganishwa na NMB
Halmashauri ilianza kutumia mashine ya kukusanyia mapato ngazi ya Kata, mwezi Julai 2016. Tumeshanunua mashine 35 kwa sasa Kata zinazotumia mashine ni Kata 17 nazo ni Mamlaka ya Mji mdogo kata 3, Hedaru, Makanya, Njoro, Bendera, Kihurio, Ndungu, Maore, Kisiwani, Ruvu ,Vumari, Kalemawe, Bwambo, Myamba na Mpinji Sambamba na ilo tumeshanunua Mashine zingine 30 za kukusanyia mpato.
12.3 Vyanzo Vipya Vya Mapato
· Halmashauri imeanza mpango wa kuanzisha soko la mazao katika Kata ya Ruvu ambalo litawezesha Halmashauri kukusanya ushuru wa mazao, tayari timu ya Wilaya imeshakutana na serikali ya Kijiji kwa ajili ya kuwashirikisha kupata eneo sahihi.
· Halmashauri imeanza mpango wa kuanzisha mnada wa mifugo Kata ya Njoro siku ya Alhamisi na Same siku ya Jumapili.
12.4 Kudhibiti Wizi /Upotevu
Halmashauri imeweka utaratibu wa kuwasilisha mapato mara mbili kwa Mwezi na ukaguzi wa nyaraka za fedha unafanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kushirikisha Kitengo cha Ukaguzi wa ndani.
12.5 Ufanisi wa Malipo
Halmashauri inafanya malipo yote kupitia mfumo wa malipo wa EPICOR, mfumo huu unategemea uwepo wa fedha kwenye kasma na kifungu husika, hivyo kasma na kifungu vinapokuwa na fedha malipo huchukua siku 3 mhusika kulipwa. Iwapo madai yanafika ofisini pasipo kuwa na fedha mhusika hufahamishwa kwa barua kusubiri mpaka hapo itakapopatikana.
9. IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI
o Mipango kiidara
Mipango kiidara ipo, na idara hii ndiyo yenye jukumu la kuunganisha Mipango na shughuli za Idara mbalimbali kupitia mfumo ujulikanao kama Medium Term Expenditure Framework (MTEF). Miradi yote ya kila Idara ngazi ya Kata na Vijiji pamoja na miradi ngazi ya Wilaya huunganishwa na kuratibiwa na Idara hii, ili kuleta ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii.
o Mpango Mkakati/ Strategic Plan
Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji pia ina jukumu la Kuratibu na kusimamia uandaaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Halmashauri (Strategic Plan). Zoezi hili hufanyika kila baada ya Miaka mitano katika Halmashauri, ambapo Idara inaanda Mpango Mkakati mpya au kuhuisha Mpango Mkakati uliopo. Hadi sasa Idara bado ipo kwenye mchakato wa kuhuisha Mpango Mkakati wa Halmashauri ambapo mda sio mrefu zoezi hili litakamilika.
o Hali ya Pato la Mwananchi kwa sasa (GDP)
Pato la Mwananchi (GDP) ni jambo muhimu sana la kuzingatia ili kupima halihalisi ya uchumi kwa kila Mwananchi katika Jamii. Hali ya Pato la Mwananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ni Shilingi 720,000/=
o Uwepo wa Takwimu zinazosaidia Idara kupanga na kufanya Maamuzi
Katika Halmashauri ya Wilaya, Takwimu zote za Kiuchumi na Kijamii zipo na zinatumika ipasavyo katika utekelezaji shughululi mbalimbali za maendeleo. Takwimu kama vile Idadi ya Watu ndizo tunazozitumia sana katika utekelezaji wa shughuli za Miradi ya maendeleo. Takwimu zingine ni za sekta mbalimbali kama vile Takwimu za Elimu, Afya, Kilimo, Mifugo na zingine mbalimbali.
o Usambazaji wa Takwimu sahihi kwa Matumizi
Hali ya usambazaji wa Takwimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ni ya kuridhisha, kwani Takwimu hizi zinasambazwa pale zinapohitajika na kwa wakati.
o Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Kazi za Miradi
Idara hii pia ina jukumu la kufanya ufuatiliaji kwa kina juu ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Miradi ya Maendeleo pamoja Kuratibu, kusimamia, kutathmini na kufanya uhakiki wa programu za maendeleo ya Halmashauri. Ufuatliaji wa utekelezaji wa shughuli za Miradi inayotekelezwa Vijijini sio ya kuridhisha sana ukilinganisha na miaka iliyopita. Hali ya ufuatiliaji wa Miradi inaathiriwa na uhaba wa Fedha hasa baada ya Kifungu cha Monitoring and Evaluation katika Bajeti ya Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo (LGCDG) kufutwa. Idara imekuwa ikipata changamoto sana juu ya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri. Idara imejitahidi na inaendelea kujitahidi sana kufuatilia miradi ya maendeleo katika Halmashauri kwa kuomba Fedha kutoka kwenye Mfuko Mkuu (GF). Pia ili kuendelea kusimamia ufanisi wa miradi inayotekelezwa, Idara inawatumia Watendaji wa Kata na Vijiji kwa kufanya mawasiliano ya karibu sana kipindi miradi inatekelezwa jambo ambalo linasaidia pia katika ufanisi wa Miradi ya Maendeleo.
o Mfumo wa kuhakikisha Utekelezaji wa Shughuli za Miradi na Idara
Pamoja na majukumu mengine Idara hii inatumia Mfumo wa kuhakikisha Utekelezaji wa Shughuli za Miradi ndani ya Idara na nje ya Idara. Maelekezo na miongozo hutolewa kutoka kwenye Ofisi ya Mkurugenzi na kuletwa ndani ya Idara. Idara hii inasimamia Mipango yote ya shughuli mbalimbali ndani na nje ya Idara. Idara zote huandaa Mipango yao na kazi kubwa ya Idara hii ni Kuratibu na kusimamia mchakato wa Mipango shirikishi na uandaaji wa bajeti ya Halmashauri. Mipango hii ya Halmashauri kiidara huunganishwa katika mfumo mmoja ujulikanao kama Medium Term Expenditure Framework (MTEF). Pia Idara hii inafanya kazi za Kuratibu mchakato wa menejiment ya Takwimu mbalimbali za Halmashauri na kupendekeza sera na mipango inayohitajika. Kazi nyingine ya Idara hii ni Kufanya makisio ya idadi ya watu ya Wilaya (Population Projection) kwa kila mwaka ambapo zoezi hili ni muhimu sana kwani husaidia katika swala zima la uandaaji wa Maoteo [Indicative Planning Figure (IPF)] wakati wa kipindi cha mchakato wa uandaaji wa Mpango na Bajeti. Yote hii ni kuhakikisha kunakuwa na usawa katika ugawaji wa huduma za kiuchumi na kijamii pamoja na Maendeleo kwa ujumla.
o Dira, Dhima, Desturi na Namna ya Kuzimiliki
Halmashauri ya Wilaya ina Dira, Dhima na Desturi kama ifuatavyo;
Dira: Kuwa na Jamii yenye Maisha bora, iliyohamasika na kuendana na mabadiliko endelevu ya Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ifikapo mwaka 2016.
Dhima: Kutoa Huduma bora kwa Jamii kupitia matumizi sahihi ya Rasilimali, kuwajengea uwezo, Utawala bora na kuwa na Maisha bora.
Desturi: Kutoa huduma kwa Jamii kwa kutumia mbinu shirikishi (Participatory Approach) ili kuleta ufanisi wa huduma ya utawala bora na Huduma kwa Jamii. Idara ina uhuru wa kumiliki desturi yake ya kutoa huduma katiaka jamii kwa kushirikisha Idara zote na Vitengo katiaka Halmashauri pamoja na ngazi za Kata na Vijiji. Idara inaendelea kufanya shughuli zake kwa kufuata desturi yake ya ushirikishwaji wa jamii.
10. KITENGO CHA MANUNUZI
o Ufanisi wa Idara
Kitengo cha manunuzi ni miongoni mwa kitengo (6) vilicho chini ya Mkurugenzi Mtendaji, aidha Majukumu ya kitengo cha manunuzi ni kama ifuatavyo;-
Ø Kusimamia shughuli zote za manunuzi
Ø Kutekeleza maagizo ya Bodi ya zabuni
Ø Sekretarieti ya bodi ya zabuni
Ø Kupanga manunuzi na mpango wa kuuza mali za serikali
Ø Kupendekeza manunuzi njia ya manunuzi na kuuza mali za serikali kwa njia ya zabuni
Ø Kuandaa mahitaji mahitaji taarifa ya mahitaji
Ø Kuandaa kabrasha za Zabuni
Ø Kuandaa matangazo ya Zabuni
Ø Kuandaa Mikataba ya Zabuni
Ø Kutoa Mikataba iliyo idhinishwa
o Idadi ya Kazi zilizotangazwa, zilizoleta Migogoro na zenye Kesi
Kwa kipindi cha Mwaka 2015/2016 zabuni zilizo tangazwa ni kama ifuatavyo;
1. Ujenzi wa barabara zabuni zilizo tangazwa ni 9
2. Ujenzi wa majengo zabuni zilizotangazwa ni 7
Idadi ya wa tumishi katika kitengo ni 4
Upungufu uliopo ni 1
Kwa upande wa Kazi zilizotangazwa hakuna kazi zozote zenye migogoro na Kesi katika Halmashauri yetu.
14.3 Changamoto
Ø Sheria ya Ununuzi Umma Kurefusha mchakato wa Manunuzi kwa serikaliza Mitaa
Ø Upungufu wa Mtumishi (1) katika kitengo cha Manunuzi
Ø Uelewa Mdogo wa sheria kwa baadhi ya Idara tumizi (User departiments)
14.4 Mikakati
Ø Kushauri wakuu wa Idara na vitengo Kuanzisha michakato ya manunuzi kwa wakati
Ø Tayari Kitengo kilisha omba kibali cha kupatiwa Mtumishi mmoja.
Ø Tayari kitengo cha Manunuzi kimefanya mafunzo kwa wakuuu wa idara na vitengo na kinaendelea
11. KITENGO CHA TEHAMA
15.1Hali ya Matumizi ya Tehama katika Idara na Vitengo mbalimbali Ndani ya Halmashauri
Kitengo cha TEHAMA ni miongoni mwa vitengo (6) vilivyopo chini ya Mkurugenzi Mtendaji, aidha matumizi ya TEHAMA kwa kila Idara ni kwa asilimia 100,kwa maana ya kwamba kila Idara na Kitengo ili ufanisi ni Mzuri kwa sababu shughuli zao za kila siku inategemea TEHAMA.
Sambamba na ilo kuna baadhi ya Idara hawawezi kabisa kuendesha shughuli zao za kila siku kama Miundo mbinu ya TEHAMA haipo,mfano Idara ya Utumishi na Utawala,kwaajili ya mfumo wa taarifa za kiutumishi yaani LAWSON,Idara ya Fedha kwaajili ya Mfumo wa Malipo na Matumizi ya Fedha za Serikali yaani EPICOR 9.05, LGRCIS kwaajili ya ukusanyaji wa Mapato.TASAF kwaajili ya uhakiki wa taarifa sahihi ya kaya maskini yaani PSSN,TOMSHA kwaajili ya taarifa sahihi ya WAVIU na Idara ya Mipango na Takwimu kwamaan ya Mfumo wa uandaaji Bajeti ya Halmashauri yaani PLANREP.
15.2Mipango ya Kukuza Tehama
Kama ilivyo kwa Vitengo vingine ifuatayo ni mipango kabambe ya kukuza kitengo cha TEHAMA ndani ya Wilaya:-
v Kuwa na Tovuti iliyo huishwa (Hosting) ambayo itakuwa inatoa taarifa za Wilaya kwa wakati na ueledi.Touvti iyo ni www.samedc.go.tz kwa sasa tovuti iyo ipo hewani na inatoa taarifa za Wilaya kwa wakati.
v Kusimamia taasisi zote za Serikali zilizopo ndani ya Wilaya kuwa na matumizi sahihi na bora ya TEHAMA.mfano huduma ya mtandao (internet).
v Kutumia baadhi ya miundo mbinu ya TEHAMA kwaajili ya kutumika kama vyanzo vya mapato ndani ya Halmashauri mfano Internet Café,
v Kufuatilia,kusimamia na kujua gharama za uendeshaji na uanzishwaji wa Gazeti au makala ya Wilaya kiujuma.
v Kufuatilia,kusimamia na kujua gharama za uendeshaji na uanzishwaji wa Redio ya Wilaya
15.3Mipango ya uimarishaji wa Mawasiliano kati ya Halmashauri na Wananchi ndani ya Halmashauri.
Ifuatayo ni Mipango ya uhimarisha wa mawasiliano kati jamii na halmashauri:-
15.4 Mipango ya Kuitangaza Wilaya kwa Wananchi wa Same, Nje ya Same na Nje ya Nchi
i) Kuanzisha gazeti/jarida ambalo litaeleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na halmashauri ya wilaya ya Same.Gazeti hilo tayari lipo kwenye mchakato nimewasilisha maelezo husika kwa Mkurugenzi Mtendaji.
ii) Kuanzisha redio ya halmashauri ya Wilaya ya Same.Kuanzisha redio kunahitaji vitu vifuatavyo;
· Ofisi/sehemu maalum kwa ajili ya studio
· Kuandika barua ya maombi kwaTCRA ili tupate kibali maalum cha kuanzisha redio na kurusha matangazo.
· Vifaa vya studio ikiwemo mitambo ya kisasa (digital machines) ya kurushia matangazo.
· Mzabuni kwa ajili ya kutengeneza studio kwa shughuli za redio
iii) Kuendelea kujenga mahusiano mazuri na vyombo vya habari ili kuleta urahisi wa kupenyeza taarifa chanya za Halmashauri ya Wilaya. Mfano mpaka sasa tuna mahusiano mazuri na vyombo mbalimbali ambavyo taarifa zetu zinatoka mara kwa mara vyombo kama gazeti la majira na TBC.
iv) Kuanza kutumia Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya kuweka taarifa mbalimbali pamoja na matangazo mbalimbali ya tender na maonyesho yenye tija kwa Wilaya nzima.
v) Kuboresha page ya facebook ya Halmashauri ya Wilaya pamoja na Blog
vi) Kuunda group la whatup kwa baadhi ya watumishi watakaoweza kuunganishwa kulingana na uwezo wa simu zao ili wapate taarifa kwa wakati zaidi.
15.5 Kuboresha Mifumo ya ufuatiliaji kwa kutumia Tehama
Kama ilivyo katika Halmashauri nyingine,Halmashauri ya Wilaya ya Same inayo mifumo ambayo inayotumia katika kutekeleza majuku ya kila siku,mifumo ni EPICOR-FEDHA, LAWSON- UTUMISHI, PSSN-TASAF,TOMSHA-TACAIDS, BEMIS-ELIMU MSINGI/SEKONDARI, LGRCIS- UKUSANYAJI WA MAPATO na LMS- ARDHI.
Mifumo yote iyo kimsingi imeboreshwa na ufuatiliaji wake upo vizuri kwani kila wakati imekuwa ikitumika bila ya Tatizo lolote,kwa kushirikiana na TAMISEMI.Pamoja na ayo yote changamoto kubwa iliyopo ndani ya Kitengo cha TEHAMA ni ufinyu wa Bajeti hivyo baadhi ya shughuli zimekuwa ngumu kutekelezeka kabisa.
16. IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
16.1Idadi Ya Mifugo
Wilaya ya same ina kanda tatu za ufugaji wa mifugo ambazo ni ukanda wa juu (Milimani), ukanda wa kati na ukanda wa tambarare (Magharibi na Mashariki). Ukanda wa milimani mifugo hufugwa na kulishwa ndani (zero grazing and tethering) kanda zinazobaki yaani ukanda wa kati na tambarare mifugo hufugwa huria (free range) kwa mifugo asili na kufugwa/kulishwa ndani (zero grazing and tethering) kwa mifugo chotara.
Eneo kubwa la malisho kwa ukanda wa tambarare ya Mashariki limepakana na Mbuga ya Taifa ya Mkomazi na ukanda wa tambarare ya Magharibi malisho haya yamepakana na mto Pangani. Wilaya ya Same ina mifugo mingi kuliko wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro. Eneo la malisho (Range land) lililoainishwa lina ukubwa wa hekta 356,200 ambazo ni asilimia 67.25 ya eneo lote la wilaya. Idadi ya mifugo wilayani ni kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini;
Jedwali 16.1: Aina na Idadi ya Mifugo inayofugwa Wilayani
AINA YA MIFUGO |
IDADI YA MIFUGO |
JULMA YA MIFUGO |
||
ASILI |
CHOTARA |
|||
Ng’ombe |
176,484 |
|
184,380 |
|
Mbuzi |
112,427 |
|
112,905 |
|
Kuku |
210,839 |
|
231,760 |
|
Kondoo |
70,903 |
70,903 |
||
Punda |
6,426 |
6,426 |
||
Nguruwe |
2,811 |
2,811 |
||
Ngamia |
18 |
18 |
||
Bata |
9,990 |
9,990 |
||
Mbwa |
8,796 |
8,796 |
Chanzo: Idara ya Mifugo na Uvuvi
16.2Aina ya Ufugaji na Mikakati ya Kufuga Kisasa
Katika halmashauri ya wilaya ya Same, kuna aina kuu tatu za ufugaji. Aina hizo ni;
i). Ufugaji huria ambao unatumika kufuga Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Punda, Mbwa, Bata, Kuku na Ngamia
ii). Ufugaji nusu huria ambao unatumika kufuga Kuku na Bata
iii). Ufugaji wa ndani na/ au kufunga ambao unatumika kufuga Ng’ombe na Mbuzi chotara wa maziwa, Kondoo, Kuku, Bata na Mbwa.
Aidha kuna mikakati mbalimbali ambayo imewekwa ili kuhakikisha kuwa ufugaji bora na wakisasa unatekelezwa na wafugaji kama ifuatavyo;
i). Kushirikiana na idara ya ardhi ili kuhakikisha mipango ya matumizi bora ya ardhi inatekelezwa ili kuepusha migogoro kati ya wafugaji na wadau wengine wanaotumia ardhi.
ii). Kuwaelimisha wafugaji juu ya kanuni za ufugaji bora na faida zake ikiwemo aina bora na sahihi ya ufugaji pamoja na uvunaji wa mifugo ili kuendana na eneo la nyanda za malisho lililopo.
iii). Kuboresha koo safu za mifugo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo kwa kutumia uhimilishaji na madume yaliyoboreshwa, mitetea pamoja na majogoo bora na kupunguza idadi ya mifugo na kuwa na mifugo michache yenye tija. Hili linafanyika katika ngazi ya mtu mmojammoja, kaya na vikundi.
16.3Mipango ya kuboresha Bidhaa za Mifugo
i). Kushirikiana na sekta binafsi zinazofanya kazi za kuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi ikiweo ujenzi wa machinjio za kisasa, masoko ya bidhaa za mifugo na viwanda vidogo vya kusindika mazao yatokanayo na mifugo.
ii). Kuboresha koo safu za mifugo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo kwa kutumia uhimilishaji na madume yaliyoboreshwa, mitetea pamoja na majogoo bora na kutoa elimu ya ufugaji bora ili kuongeza kipato ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla.
iii). Kudhibiti magonjwa ya mlipuko kwa kufanya chanjo, tiba za mifugo, uogeshaji wa mifugo pamoja na usimamizi wa minada ili kuongeza ubora na thamani ya mazao yatokanayo na mifugo.
iv). Kutoa huduma bora ya ukaguzi wa nyama kwa lengo la kulinda afya ya jamii na kuzuia magonjwa ya kuambukiza (Zoonoses).
v). Kusajili vituo vya huduma za mifugo ili kusogeza huduma za mifugo karibu na wafugaji na kusimamia utoaji wa huduma bora za mifugo zinazotolewa na wadau wa sekta binafsi.
vi). Kutoa elimu juu ya ufugaji bora wa samaki kwenye mabwawa ya jamii na binafsi na kuzuia uvuvi haramu ili kuongeza kiwango bora cha uzalishaji wa samaki.
17. KITENGO CHA NYUKI
17.1Idadi ya Mizinga
Mizinga ya asili = 30,000
Mizinga ya kisasa = 2200
17.2 Uzalishaji Na Mazao Ya Nyuki Kwa Mwaka Na Kwa Aina Ya (Nyuki Wanaouma Na Wasiouma)
a) Asali – Wastani wa Kilo 27,576 kwa mwaka.
b) Nta - Wastani wa Kilo 2,519 kwa mwaka
17.3 Mikakati Ya Kukuza Uzalishaji Wa Mazao Ya Nyuki
17.4 Mikakati Ya Kufanya Zao La Asali Kuwa Zao La Kiuchumi Linalotegemewa Na Wilaya
I. Kuanzisha utaratibu wa kukagua mazao ya nyuki ili kudhibiti ubora wake.
II. Kuanzisha na kusimamia vituo vya kukusanyia na kuchakata asali.
III. Kuwa na utaratibu wa kupima asali ili kudhibiti ubora wake.
IV. Kuanzisha utaratibu wa kuweka asali katika madaraja ili kupata bei nzuri. (Viwango vya ubora wa asali vitumike)
V. Kutoa mafunzo na kuelimisha wafugaji nyuki (wazalishaji) na wafanyabiashara wadogo kuhusu njia bora zaidi za kutunza mazao ya nyuki.
VI. Kuhakikisha vifaa vya uvunaji, uchakataji, ufungashaji, uhifadhi na usafirishaji wa asali vinapatika kwa urahisi.
VII. Kuandaa mwongozo wa sheria ndogo kuhusu makusanyo ya mapato (ushuru) utokanao na mazao ya nyuki kwa wafanyabiashara wanaosafirisha nje ya Wilaya.
18. KITENGO CHA UWEKEZAJI
Halmashauri ya Wilaya ya Same ni miongoni ya wilaya 6 katika Mkoa wa Kilimanjaro ambayo inafursa za uwekezaji katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta ya kilimo, madini, usafiri, utalii, ujenzi, uvuvi, ufugaji, mifugo, viwanda, biashara na kijamii (Elimu, Afya na Maji) na Kiutamaduni (Michezo na Utamaduni).n.k. Uwekezaji kwa mujibu wa kitaifa pia unalenga katika kuwezesha maendeleo ya nchi lakini pia kwa wakazi kufaidika na fursa mbalimbali.
18.1 Idadi ya wawekezaji waliopo na aina ya uwekezaji
Na |
Jina la mwekezaji |
aina ya uwekezaji |
Mahali ulipo |
Maelezo |
1. |
Willy Enterprises |
Madini ya boxite |
Mwembe/Chome |
Mwekezaji anachimba madini hayo na kupeleka katika nchi ya Kenya |
2. |
Umoja wa wakulima wa Tangawizi |
Kilimo cha tangawizi |
Myamba |
Umoja wa ushirika unawanachama zaidi 600 |
3. |
|
Kiwanda cha Tangawizi |
Myamba |
Kiwanda kimesimama |
4. |
Miller International Agrovet |
Kilimo cha vitunguu |
Kijiji cha Jiungeni |
Miller inamiliki eneo la zaidi ya ekari 400. |
5. |
SMK |
Kilimo cha vitunguu |
Kijiji cha Jiungeni |
Anamiliki zaidi ya ekari 200 za vitunguu |
6. |
Tona lodge |
Utalii/Asili |
Kata ya Mshewa |
Uwekezaji unafanya shughuli za utalii wa asili |
7. |
MKUNAPA |
Utalii/wanyama pori |
Mbuga ya Mkomazi |
Eneo la uwekezaji linalolimilikiwa ni ekari 3245. |
8. |
KIDC |
Kiwanda cha vikombe |
Kata ya Same |
Kiwanda hakifanyi kazi kwa ufanisi kutokana na uongozi. |
9. |
Makampuni ya simu |
Mitandao ya simu |
Wilaya ya Same |
Makampuni ya simu ya Airtel, Haloteli Tigo, Vodacom na Zantel |
10. |
Mashirika ya Fedha |
Huduma ya ya fedha |
Wilaya ya Same |
NMB, CRDB, Same Kaya SACCOs, CWT, Amacha, BRAC n.k. |
19.2 Vivutio vya uwekezaji vilivyopo
Na. |
Aina ya kivutio cha uwekezaji |
Vivutio |
1. |
Mbuga ya Taifa ya Mkomazi yenye ukubwa wa ekari 3245 |
Wanyama wa aina mbalimbali, ndege na eneo lenye miti ya asili |
2. |
Uchimbaji wa madini |
Eneo la uchimbaji jasi, green garnet, green tourmaline, rhodilite na boxite. |
3. |
Bwawa la Kalimawe na Karamba |
Aina ya samaki kama vile: Tilapia, perege, kambale na mkunga. Bwawa ili lina kilomita za mraba 3. |
4. |
Msitu wa Shengena hekta 27,880 |
Aina ya miti, vipepeo, nyuki, ndege, mbega, nyani, tumbili na maji yanayotiririka kwa mwaka mzima. |
5. |
Mawasiliano na miundo mbinu |
Kuna barabara zinazopitika kwa mwaka mzima, mitandao ya simu na usafiri wa kampuni za Kilenga, Kimbwe na Phiba. |
6. |
Ujenzi wa viwanda |
Kuna maeneo ya ujenzi wa viwanda kama:- saruji n.k |
7. |
Mto Pangani |
Mto Pangani unaopita katika Kata ya Ruvu wenye urefu wa km 91, maji yanafaa kwa kilimo cha umwagiliaji na ufugaji wa samaki. |
8. |
Huduma za Malazi (Hotel) |
Katika Wilaya tuna wawekezaji katika huduma za malazi km Elephant Motel, Orlando, Nzoroko n.k. |
Chanzo: Kitengo cha Uwekezaji
18.3 Maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji
Halmashauri ya wilaya ya Same imetenga jumla ya ekari kama ifuatavyo:-
-Eneo la Kitamri Halmashauri imetenga ekari 150 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda
-Eneo la Kata ya Makanya Kijiji kimetenga jumla ya ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha saruji.
Mkakati wa halmashauri ya uendelezaji wa fursa za uwekezaji;-
Ø Halmashauri imeandaa mpango wa kujenga mazingira kwa makundi haya ya wakulima wadogo na wafugaji kuchangamkia fursa hizi badala ya kuelekeza jitihada kubwa katika uwekezaji kutoka nje.
Ø Halmashauri inautaratibu wa kuwashirikisha wawekezaji kutoka nje wawekeze katika msingi wa ubia na wazalishaji wadogo, kwa maana kuwa wazalishaji wadogo - wakulima na wafugaji - katika vikundi vyao, msingi wao mkubwa ukiwa ni rasilimali ardhi, wanaweza kuingia katika ubia na wawekezaji toka nje kwa namna ambayo wanakuwa na sauti katika maamuzi na hivyo kuwezesha kile tukiitacho win win situation, yaani 'hali ya mafanikio kwa pande zote zinazohusika'.
Ø Halmashauri inawezesha vikundi vya wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu ili kuwa na fursa za wazalishaji wadogo vijijini.
Ø Halmashauri kwa kushirikiana na wawekezaji kuimarisha miundombinu ya barabara na mawasiliano ya simu katika maeneo ya Wilaya ya Same.
18.4 Mikakati ya kuwa na viwanda Wilayani
· Kampuni ya DOTT Services (T) imeanza mazungumzo na Halmashauri kwa ajili ujenzi wa kiwanda cha kuparck maji na uvunjaji wa kokoto katika eneo la Saweni.
· Uwekezaji wa kiwanda cha saruji katika Kata ya Makanya, ambapo mkakati wa kumpatia mwekezaji wa kampuni ya A to Z toka Arusha. Taratibu za kupata eneo katika Kata ya Makanya (Vikao vya awali vya kijiji cha Makanya vimekwisha fanyika)
· Kilimo cha miwa; Uwekezaji wa kilimo cha miwa kampuni ya Kilimanjaro Biochem Limited inayomiliki kiwanda cha utengenezaji wa spiriti katika wilaya ya Mwanga kimeanza maandalizi ya kuwa na mikataba na wakulima ili waweze kulima miwa katika kata ya Ruvu. KBL inahitaji kulimiwa miwa kiasi cha ekari 2000 wameanza mazungumzo na wakulima wa maeneo ya kata ya Ruvu. Endapo wakulima wataridhia mikataba hiyo, kampuni hiyo imepanga kujenga kiwanda katika eneo la Ruvu Muungano cha kukamua miwa na kusafirisha ikiwa maji ya miwa (syrup). Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 200. (Ombi la KBL liliwasilishwa kwenye kamati ya Fedha, Utawala na Mipango).
19. CHANGAMOTO ZA KIWILAYA
19.1Njaa
19.2Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
19.3Changamoto zingine
20. MIKAKATI YA KIWILAYA
20.1Kumaliza Tatizo la Njaa
· Kuhakikisha elimu ya uvunaji maji ya mvua, matumizi bora ya maji na hifadhi ya ardhi na udongo imetolewa kwa wakulima.
· Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuzuia/kupunguza upotevu wa
mazao ya nafaka na mikunde wakati wa kuvuna na kuhifadhi
(Post harvest loss handling).
· Kuhakikisha elimu ya ukadiriaji wa mahitaji ya mazao ya chakula kwa wakulima ngazi ya kaya imetolewa.
· Kutoa elimu kwa wakulima juu ya hifadhi na matumizi bora ya mazao ya chakula kwa maeneo ambayo yamepata mavuno mazuri msimu wa vuli hasa maeneo ya kilimo cha umwagiliaji.
· Kutoa ushauri kwa wakulima kutekeleza kilimo cha mazaoyanayostahimili ukame na yanayotumia kiasi kidogo cha unyevu hadi kukomaa kama mazao jamii ya mizizi na mikunde na Mtama.
· Kuhakikisha uimarishaji wa matumizi bora ya maji katika miundombinu ya umwagiliaji iliyopo na kuhakikisha kunakuwepo na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula kwa misimu miwili na wakulima wanazingatia ushauri wa wataalam waliopo vijijini.
· Kwa kuwatumia Maafisa Ugani waliopo kuhakikisha wakulima wanatumia teknolojia bora na sahihi za uzalishaji mazao ya chakula na biashara kwa ajili ya uhakika na usalama wa chakula ngazi ya kaya.
· Kuhimiza wafugaji walio na mifugo kuuza wakati bado ikiwa na hali nzuri ya kiafya na kununua chakula na kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia.
· Kuhimiza wakulima waliopo maeneo ya umwagiliaji kulima mazao yenye thamani na ubora kwa uhakika wa kuongeza kipato hatimaye kumudu kujinunulia chakula cha kutosha.
· Kuhamasisha wafanyabiashara wenye uwezo kununua chakula Katika maeneo yenye chakula cha ziada na kuleta kuuza katika maeneo yenye upungufu kwa bei nafuu/elekezi.
20.2Kumaliza Tatizo la Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
20.3Kuongeza Pato la Mwananchi
20.4Kuongeza Mapato ya Halmashauri
20.5Kuongeza Fedha tunayochangia kwenye Mfuko wa Taifa (TRA)
20.6Kuongeza na Kuboresha Viwanda
· Kampuni ya DOTT Services (T) imeanza mazungumzo na Halmashauri kwa ajili ujenzi wa kiwanda cha kuparck maji na uvunjaji wa kokoto katika eneo la Saweni.
· Uwekezaji wa kiwanda cha saruji katika Kata ya Makanya, ambapo mkakati wa kumpatia mwekezaji wa kampuni ya A to Z toka Arusha. Taratibu za kupata eneo katika Kata ya Makanya (Vikao vya awali vya kijiji cha Makanya vimekwisha fanyika)
· Kilimo cha miwa; Uwekezaji wa kilimo cha miwa kampuni ya Kilimanjaro Biochem Limited inayomiliki kiwanda cha utengenezaji wa spiriti katika wilaya ya Mwanga kimeanza maandalizi ya kuwa na mikataba na wakulima ili waweze kulima miwa katika kata ya Ruvu. KBL inahitaji kulimiwa miwa kiasi cha ekari 2000 wameanza mazungumzo na wakulima wa maeneo ya kata ya Ruvu. Endapo wakulima wataridhia mikataba hiyo, kampuni hiyo imepanga kujenga kiwanda katika eneo la Ruvu Muungano cha kukamua miwa na kusafirisha ikiwa maji ya miwa (syrup). Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 200. (Ombi la KBL liliwasilishwa kwenye kamati ya Fedha, Utawala na Mipango).
20.7Kuongeza Ajira kwa Vijana
HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KISEKTA KWA MKUU WA WILAYA YA SAME BI. ROSEMARY SITAKI
UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Same ilianzishwa rasmi kwa Sheria ya Bunge Sura ya 287 (Mamlaka za Wilaya) ya Sheria za Tanzania na ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 01 Januari 1984. Aidha Halmashauri ina Idara 13 na vitengo 6 ambavyo vinatekeleza majukumu mbalimbali kama ambavyo imeanishwa hapo chini:-
IDARA YA AFYA
1.1 Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Asilimia 30.6 ya kaya za Wilaya ya Same zimejiunga na CHF. Kwa Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Same ni ya 3 Kati ya Wilaya saba za Mkoa.
1.1.1 Mipango/Mikakati Iliyopo kufikisha 80%
Jedwali 1.1: Vituo Vya Kutolea Huduma Za Afya Wilayani
S/No |
AINA YA KITUO |
IDADI |
|||
|
|
SERIKALI |
MASHIRIKA YA DINI |
BINAFSI |
JUMLA |
1 |
Hospitali |
1 |
1 |
- |
2 |
2 |
Vituo vya Afya |
6 |
1 |
1 |
8 |
3 |
Zahanati |
39 |
15 |
9 |
62 |
|
Jumla |
46 |
17 |
10 |
72 |
Chanzo: Idara ya Afya
1.3 Hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
1.4 Mkakati makini wa zoezi la usafi na Mipango ya kuwafanya watu wajenge tabia ya usafi
Kila kitongoji kuwa na siku moja ya usafi itakayoshirikisha kila mwananchi tofauti na siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi ya usafi kitaifa
Kuunnda/kuwa na vikundi kazi kwa kila kata vitakavyotokana na jamii , vitakavyohusika kusimamia usafi kwa kila kata na watakao kaidi watatozwa faini. Aidha asilimia kadhaa ya faini itakuwa ya vikundi/kikundi kutegemeana na makubaliano
Kila kata kuwa na Afisa afya atakayeshirikiana na wataalamu wengine waliopo kwenye kata. Kata ambayo haina Afisa afya ateuliwe afisa maendeleo ya jamii kukaimu nafasi ya Afisa afya
Kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani wote watakaokiuka sheria na kanuni za afya ya mazingira
Kuwa na dampo la taka ngumu na taka maji katika Halmashauri
Kuwa na vitendea kazi, gari rasmi la kusomba taka na ada za uzoaji taka zitumike kwa makusudi ya uzoaji taka
Kuwezesha walezi wa kata siku 5 kila robo mwaka kwa ajili ya kutembelea kata na kuhamasisha jamii juu ya usafi wa mazingira
Kila biashara/ kaya kuwa na chombo/vyombo vya kuhifadhia taka
Kushinadanisha kitongoji au mtaa, kata na kata ili kuleta ushindani na kuboresha usafi
Kujenga vizimba vya taka katika maeneo yatakayo ainishwa Elimu ya usafi na mazingira ikaziwe shuleni (shule za msingi, sekondari na vyuo) mahali pa kazi yao.
1.5 Idadi ya Watumishi waliopo, Ikama na Pungufu ndani ya Idara
Idara ya afya inahitaji jumla ya watumishi 1114 waliopo ni 462, idara ina upungufu wa watumishi 689. Sawa na 61.8%. Hospitali ya Wilaya inahitaji Watumishi kwa kada kama ifuatavyo:-
Jedwali 1.1: Idadi ya Watumishi waliopo, Ikama na Pungufu ndani ya Idara
FANI YA MTUMISHI |
HITAJIKA |
WALIYOPO |
PUNGUFU |
|
Medical Doctor |
23 |
4 |
19 |
|
Assistant Medical officer |
39 |
3 |
36 |
|
Assistant Dental officer |
1 |
- |
1 |
|
Dental therapist |
2 |
1 |
1 |
|
Pharmacist |
2 |
1 |
1 |
|
Pharmaceutical Technologist |
|
5 |
|
|
AssistantPharmaceutical Technologist |
8 |
- |
8 |
|
Social welfare |
3 |
- |
3 |
|
Environmental officer Health officer |
2 |
1 |
1 |
|
Wauguzi |
99 |
71 |
28 |
|
Laboratory scientist |
1 |
1 |
- |
|
Health laboratory technologist |
4 |
4 |
- |
|
AssistantHealth laboratory technologist |
4 |
1 |
3 |
|
Occupational therapist |
2 |
1 |
1 |
|
Physiotherapist |
2 |
2 |
- |
|
Medicall attendants |
59 |
44 |
15 |
|
Health secretary |
1 |
1 |
- |
|
Medical recoder |
5 |
1 |
4 |
|
Radiology scientist |
1 |
- |
1 |
|
Radiographer technologist |
3 |
- |
3 |
|
Nutritionist |
1 |
1 |
- |
|
Ophthalmologist |
1 |
1 |
- |
|
Optometrist |
3 |
- |
3 |
|
Economist |
1 |
- |
1 |
|
Biomedical technologist |
4 |
- |
4 |
|
Motury attendants |
5 |
- |
5 |
|
Computer system analysit |
1 |
- |
1 |
|
Computer operator |
1 |
- |
1 |
|
Accountant |
1 |
- |
1 |
|
Assistant Accountants |
2 |
- |
2 |
|
Supplier officer |
1 |
- |
1 |
|
Assistant supplier officer |
1 |
1 |
- |
|
Electrical Technician |
4 |
- |
4 |
|
Personal secretary |
1 |
1 |
- |
|
Plumber |
1 |
- |
1 |
|
Security guard |
4 |
2 |
2 |
|
Cooker |
4 |
- |
4 |
|
Dhobi |
4 |
- |
4 |
|
Driver |
5 |
2 |
3 |
|
|
|
|
|
|
Chanzo: Idara ya Afya
Kwa upande wa Hospitali ya Wilaya, kutokana na staffing level 2014-2018 Hospitali ya wilaya ina upungufu wa watumishi 97.
1.6 Magonjwa Kumi yanayoongoza kwa Idara ya Wagonjwa wa Nje ni:
Magonjwa ya njia ya hewa, Nimonia, Malaria, Magonjwa ya kuhara, Minyoo ya tumbo, Magonjwa ya ngozi, Magonjwa mengine, Upasuaji wa dharura, Upungufu wa damu na Magonjwa ya macho.
1.7 Magonjwa Kumi yanayoongoza kwa Idara ya Wagonjwa wa Ndani ni: Nimonia, Magonjwa ya njia ya hewa, Magonjwa mengine, Malaria kali, Upungufu wa damu, Magonjwa ya kuhara, Watoto waliozaliwa na uzito mdogo, Upasuaji wa dharura, Ukimwi na Majeraha mbalimbali.
1.8 Vifo Vya Watoto Umri Chini Ya Siku 28
Mwaka 2015 vilitokea vifo 5 katika vizazi hai 1000
1.9 Vifo Vya Watoto Chini Ya Miaka 5
Mwaka 2015 vilitokea vifo 8 katika vizazi hai 1000
1.10 Hali Ya Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI
Kiwango cha maambukizi ni 1.4%, Watu wanaoishi na VVU ni 6,181, wanaotumia dawa ni WAVIU 4, 688, vituo vinavyotoa huduma kwa WAVIU ni 8, na huduma kwa njia ya kliniki ya mkoba ziko 9.
1.11 Changamoto
Idara ya afya inapambana na Changamoto zifuatazo: -
Upungufu wa watumishi wenye taaluma mbalimbali kwa asilimia 61.4%
Kuchelewa kupokea fedha za mfuko wa pamoja na kutokupokea kabisa fedha za kutokana na kutokupata fedha za matumizi mengineyo (OC) ruzuku kutoka serikali kuu tangu mwezi Januari 2016
Wodi zilizopo ni ndogo hazikidhi mahitaji.
Upungufu na uchakavu wa nyumba za watumishi katika ngazi zote za vituo vya huduma.
Maabara ya Hospitali ya wilaya ni ndogo, Halmashauri imeanza funya mawasiliano na marafiki wake wa Tillburg Partnership Uholanzi ili kupata fedha za ujenzi wa Maabara mpya.
Kutokupokea fedha ya kulipa watumishi walioitwa kazini (on call allowance) tangu mwezi Janauri 2016.
1.12 Mikakati ya kupambana na Changamoto
Ili kupambana na changamoto hizo, idara imeweka mikakati ifuatayo:
Kuomba vibali vya ajira na kuweka vivutio kwa waajiriwa wapya na watumishi kwa ujumla (Staff attraction and Retention strategies)
Kushirikiana na Bohari ya dawa (MSD) kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kwa kuhakikisha kwamba kila kituo kinaandaa na kutuma taarifa na maombi ya dawa na vifaa – tiba kwa wakati kwenda MSD, na Idara kufuatilia maombi hayo ili yafanyiwe kazi na makasha kusambazwa vituoni kwa wakati muafaka.
Halmashauri tayari imeomba mkopo wa dawa kutoka Mfuko wa Taifya wa Bima ya Afya na inakarabati chumba kwa ajili ya duka la dawa ndani ya hospitali ya Wilaya ili kukabiliana na changamoto ya wagonjwa kununua dawa na vifaa tiba nje ya hospitali.
Kushirikisha wadau wengine wa sekta ya Afya katika upatikanaji wa Vifaa tiba na vitendea kazi Muhimu vya kutolea huduma bora za afya. Hadi sasa Idara imewashirikisha Tillburg Partnership (Uholanzi), PSPF, CRDB na NMB. Bado Idara inatafuta wadau wengine.
Kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kupata fedha za kujengea jengo la kusubiria wajawazito na wodi za wagonjwa katika Hospitali ya wilaya.
Kuendelea kuomba fedha serikali kuu kwa ajili ya ruzuku, posho za kuitwa kazini na posho ya kujikimu kwa waajiriwa wapya.
2.0 IDARA YA ELIMU MSINGI
2.1 Utangulizi
Halmashauri ina jumla ya shule za Msingi 192 kati ya hizo shule 185 ni za Serikali na 7 ni za binafsi. Shule hizi ziko katika Kata za Kiutawala 34 na Kata 1 ya Kielimu.. Shule hizi zina jumla ya wanafunzi 59833 kati yao wasichana ni 30613 na wavulana ni 2920.
2.2 Ufaulu wa Wanafunzi
Kiwango cha kufaulu kwa Mtihani wa Taifa darasa la Saba Kimkoa na Kitaifa ni kama ifuatavyo:-
Jedwali 2.1: Ufaulu wa Mtihani wa Taifa darasa la Saba Kimkoa na Kitaifa
MWAKA |
KIWANGO CHA UFAULU (%) |
NAFASI KIMKOA |
NAFASI TAIFA |
2014 |
63.48 |
7 |
52 |
2015 |
75.94 |
6 |
51 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
2.3 Malengo Ya Kuongeza Ufaulu
Ili kufikia malengo ya asilimia themanini na tano ya ufaulu (85%), Halmashauri kupitia idara ya Elimu Msingi imeweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la ufaulu duni katika mitihani ya ndani na ya kitaifa kama ifuatavyo:
Kufuatiliaji utendaji kazi wa walimu katika Uongozi na Utawala na Utekelzaji wa Mtaala. Zoezi lilianza kwa kufuatilia shule 35 zilizofanya vibaya zaidi
Kuomba walimu toka TAMISEMI ili tuweze kupunguza upungufu mkubwa wa walimu.
Kuhamashisha wazazi na walezi kuchangia chakula cha mchana ili wanafunzi wapate chakula cha mchana shuleni.
Shule zote zimepewa maagizo ya kutekeleza Ratiba ya ufundishaji wa muda wa ziada ili kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kipindi kilichopita.
Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa elimu itaendelea kutoa mafunzo ya mbinu za ufundishaji kwa walimu mfano semina ya somo la Lugha na Hisabati.
Idara inaendelea na mpango wa kusoma na kutafisiri mpango wa kuinua taaluma ya Mkoa wa Katavi ujulikanao kama “ Katavi model” ili uweze kuhawilishwa na kutumika katika wilaya ya Same kwa lengo la kuinua na kuboresha taaluma.
Kuhimiza na kusimamia mazoezi ya mwisho wa wiki, mwezi, mitihani ya utamirifu na ile ya Mwisho wa mihula ili kuchochea ushindani katika ngazi ya darasa, shule, Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa.
Kupitia na kutekeleza Ushauri na Mapendekezo Mthibiti Ubora wa Elimu shuleni.
Kutoa motisha chanya kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya utamirifu Wilaya, Mkoa na Mitihani ya Kitaifa.
Jedwali 2.2: Miundo Mbinu Ya Shule: Samani Na Majengo
SAMANI |
MAHITAJI |
VILIVYOPO |
UPUNGUFU |
MADAWATI |
26389 |
32775 |
6387 |
MEZA |
2914 |
1719 |
1195 |
VITI |
3211 |
1692 |
1519 |
KABATI |
1714 |
523 |
1191 |
MAJENGO |
|
|
|
NYUMBA ZA WALIMU |
1463 |
368 |
1095 |
MADARASA |
1551 |
1298 |
253 |
VYOO |
2602 |
1599 |
1003 |
STOO |
370 |
93 |
277 |
OFISI |
372 |
295 |
77 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
2.4 Hali Ya Walimu Katika Shule Za Msingi:
Hali ya walimu ni kama ifuatavyo:-
Jedwali 2.3: Walimu wa Shule Za Msingi Kwa Madaraja
SIFA |
MAHITAJI |
WALIOPO |
PUNGUFU |
||
ME |
KE |
JML |
|||
DARAJA IIIA |
1999 |
558 |
846 |
1404 |
581 |
STASHAHADA |
7 |
7 |
14 |
||
SHAHADA |
0 |
0 |
0 |
||
JUMLA |
565 |
853 |
1418 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
Jedwali 2.4: Idadi Ya Walimu Katika Shule Za Msingi (Angalia Kiambatisho)
MAHITAJI |
WALIOPO |
ASILIMIA |
UPUNGUFU |
ASILIMIA |
1999 |
1418 |
70.9 |
581 |
29.1 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
2.5 Utoaji wa Chakula Shuleni
Idadi ya shule zinazotoa chakula katika wilaya Same ni 17 kati ya 185 shule hizo Nasuro, Daghaseta, Mughungani, Mkanyeni, Mwembe, Mshewa, Kafingiro, Goma, Kwizu Mrindi, Manka, Kweresha ,Kiomande, Parane, Ivuga, Mpinji na Tae.
2.6 Hali Ya Mimba
Hakuna taarifa ya mwanafunzi aliyepata mimba toka mwezi Januari hadi sasa
2.7 Changamoto Mbalimbambali Zilizopo
Shule za Msingi Wilaya ya Same zinakumbana na changamoto mbali mbali, ambazo zinasababisha ufaulu wa wanafunzi kuwa wa kiwango cha chini. Baadhi ya changamoto hizo ni :
Uhaba wa nyumba za walimu katika maeneo ya shule.
Kukosekana kwa chakula cha mchana kwa wanafunzi shuleni.
Upungufu mkubwa wa Walimu.
Upungufu wa rasilimali fedha na vifaa kwa ajili ya ufuatiliji utendaji kazi wa walimu
3.0 IDARA YA ELIMU SEKONDARI
3.1 Utangulizi
Halmashauri ya Wilaya ya Same ina jumla shule 51 za sekondari, kati ya shule hizo 36 ni za serikali na 15 ni za binafsi. Mwaka 2015 shule 47 za sekondari ndizo zilikuwa na watahiniwa wa shule wa Mtihani Taifa kidato cha nne. Shule moja ya Hedaru Sekondari haikufanikiwa kupata matokeo mpaka tathmini hii inafanyika kutokana na kutokuwasilisha nyaraka muhimu Baraza kwa wakati.
Idadi ya Wanafunzi, kabla na baada ya Uhakiki ni kama ilivyoainishwa katika Majedwali hapa chini;
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
IDADI YA WANAFUNZI ILIVYO MWEZI AGOSTI, 2016 BAADA YA UHAKIKI |
|
||||||||||||||||||||
KID I |
KID II |
KID III |
KID IV |
KID V |
KID VI |
JUMLA KUU |
|
||||||||||||||
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
|
2133 |
2553 |
4686 |
1748 |
2142 |
3890 |
1162 |
1293 |
2455 |
1568 |
1865 |
3433 |
438 |
0 |
438 |
459 |
0 |
459 |
7508 |
7853 |
15361 |
|
|
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
Watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 5044, kati yao wasichana ni 2816 na wavulana ni 2228.watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa ni 4958 na waliopata daraja la ufaulu kuanzia daraja I-IV ni 2809 sawa na asilimia 56.6 ya waliofanya mtihani huo, ambapo watahiniwa 2149 walifeli, sawa na asilimia 43.4. Aidha, ufaulu huu umeshuka kwa asilimia 1.6 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2014 ambapo ulikuwa ni asilimia 58.2.
Aidha, matokeo ya kidato cha pili, 2015, Watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa upimaji walikuwa 4977, kati yao watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 4720 sawa na aslimia 94.8 ya waliosajiliwa. Kati ya Watahiniwa 4720 waliofanya Mtihani wa upimaji wa Taifa kidato cha pili, Watahiniwa waliopata madaraja ya ufaulu walikuwa 3856 sawa na asilimia 82 ya waliofanya mtihani. Watahiniwa waliofeli walikuwa 864 sawa na asilimia 18 ya waliofanya mtihani.
3.2.1 Mchanganuo wa Ufaulu Kidato cha Nne
Kufuatia utaratibu ambao Baraza la Mitihani la Tanzania limetumia kutunuku matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne 2015 kwa kutumia madaraja ya ufaulu kama ilivyokuwa mwaka 2013 na kurudi nyuma, matokeo ya kila shule yameainishwa katika madaraja matano ambayo ni “daraja la kwanza, pili, tatu, nne na waliofeli. Ufaulu huo kimadaraja ni kama ifuatavyo;
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
3. 2.2 Nafasi Ya Wilaya Kimkoa Na Kitaifa
Katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE) mwaka 2014 wilaya ilishika nafasi ya 96. Kwa mwaka 2015 wilaya imeshika nafasi 7 kati ya wilaya 7 kimkoa na nafasi ya 102 kitaifa. Aidha, katika mtihani wa upimaji wa kidato cha pili (FTNA) kwa mwaka 2014, wilaya ilishika nafasi ya 47, na mwaka 2015 wilaya imeshika nafasi ya 57.
vi. Wakuu wa shule wameagizwa kushirikiana na waratibu Elimu Kata kudhibiti utoro wa wanafunzi ambao hawahudhurii masomo badala yake wanakuja siku za mitihani tu.
Kwa upande wa hali ya Madarasa, Vyoo na Nyumba za Walimu ni kama ilivyoainishwa katika jedwali lifuatalo;
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
Kwa upande wa Idati ya Walimu, tuna uhaba mkubwa kwa upande wa Walimu wa Masomo ya Sayansi ukilinganisha na Walimu wa Masomo ya sanaa ambao wapo wakutosha na baadhi ya masomo wamezidi. Mfano katika somo la Kiswahili kuna zidio la Walimu 32 na somo la Kingereza kuna zidio la Walimu 13 kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini;
Jedwali 3.5: Idadi ya Walimu Wanaohitajika, Waliopo na Pungufu kwa kila somo
Chanzo: Idara ya Elimu Secondari
3.6 Ukamilishaji wa Maabara
Idara imejitahidi kusimamia ujenzi wa maabara katika shule zote 36, kama ambavyo iliagizwa na Mh. Rais wa awamu iliyopita. Ambapo jumla ya vyumba vya maabara vilivyotakiwa ni 108. Kwa sasa vyumba ambavyo havijakamilika ni vinne (04), vyumba vilivyokamilika ni 104. Ambayo havijakamilika ni katika shule za sekondari Lugulu na Masheko ambazo zote ni shule mpya. Aidha katika baadhi ya shule samani za maabara hazijakamili pia bado kuna upungufu wa vifaa vya ufundishiaji na ujifunzaji kwa masomo ya sayansi.
3.7 Mikakati ya Ukamilishaji
Mikakati iliyopo katika kukamilisha ujenzi wa maabara hizo ni;
Hali ya utoaji chakula katika shule za kutwa za serikali kwa sasa siyo nzuri, baada ya tangazo la Elimu bila malipo ambapo shule zote za sekondari zilikuwa zinatoa chakula cha mchana. Aidha, kwasasa idadi ya wanafunzi wanaopata chakula cha mchana ni kama ifuatavyo; wanafunzi 8445 wanapata chakula na ambao hawapati chakula ni 6916.
Aidha, ofisi imepokea waraka wa Elimu Na. 3 wa mwaka 2016, ambao unawataka wajumbe wa bodi na wazazi kuhakikisha wanafunzi wote wa shule za sekondari za kutwa wanapata chakula cha mchana. Waraka huu umeshapelekwa shuleni kwa ajili ya utekelezaji. Kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 3.7 kamati / bodi za shule za serikali (iii) kushirikiana na wazazi/jamii kuweka utaratibu wa chakula cha mchana au chakula na huduma za hosteli katika shule za kutwa kulingana na mazingira yao, na kutuma mapendekezo kwa MkurugenziMtendaji wa Halmashauri.
3.9 Mikakati Ya Kudhibiti Utoro Na Mimba Shuleni
Hali ya utoro limekuwa tatizo sugu kwa baadhi ya wanafunzi, hii ni kutokana na baadhi ya wanafunzi kushiriki katika biashara za kuendesha boda boda na shughuli nyingine zinazofanywa na wazazi / walezi.
Kupitia vikao vya bodi, wazazi /walezi, jamii kutoa malezi mfungamano, basipo kuangalia na kubagua watoto ili kuboresha nidhamu na kuwajengea uwezo wa kujitambua kama sehemu ya jamii wanayoishi.
Jedwali 3.6: Taarifa za Wanafunzi Watoro, Waliopata Mimba, Waliohama Na Kuhamia pamoja na Wanaopata na Wasiopata Chakula
S/N |
SHULE |
MIMBA |
WATORO |
WALIOHAMA |
WALIOHAMIA |
WANAOPATA CHAKULA |
WASIOPATA CHAKULA |
|
||||||
|
||||||||||||||
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
ME |
KE |
JML |
|
|||||
1 |
BANGALALA |
4 |
6 |
7 |
13 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
106 |
81 |
|
2 |
BEMKO |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
408 |
0 |
|
3 |
BOMBO |
2 |
3 |
4 |
7 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
46 |
310 |
|
4 |
CHALAO |
3 |
3 |
2 |
5 |
2 |
3 |
|
3 |
0 |
3 |
539 |
0 |
|
5 |
CHANJAGAA |
1 |
3 |
5 |
8 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
100 |
112 |
|
6 |
GONJA |
3 |
27 |
9 |
36 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
835 |
|
7 |
KASEMPOMBE |
2 |
10 |
8 |
18 |
4 |
2 |
0 |
0 |
0 |
0 |
180 |
171 |
|
8 |
KAZITA |
3 |
3 |
2 |
5 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
183 |
0 |
|
9 |
KIBACHA |
2 |
13 |
15 |
28 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
765 |
0 |
|
10 |
KIGANGO |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
160 |
0 |
|
11 |
KIHURIO |
2 |
2 |
4 |
6 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
193 |
349 |
|
12 |
KIMALA |
1 |
7 |
9 |
16 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
491 |
0 |
|
13 |
KIRANGARE |
1 |
4 |
2 |
6 |
4 |
1 |
0 |
0 |
6 |
0 |
50 |
363 |
|
14 |
KISIWANI |
4 |
2 |
0 |
2 |
2 |
0 |
0 |
3 |
3 |
6 |
730 |
0 |
|
15 |
KWAKOKO |
4 |
7 |
10 |
17 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
405 |
0 |
|
16 |
KWIZU |
0 |
0 |
0 |
0 |
1 |
0 |
1 |
1 |
0 |
1 |
375 |
0 |
|
17 |
LUGULU |
3 |
2 |
2 |
4 |
13 |
26 |
39 |
11 |
18 |
29 |
78 |
124 |
|
18 |
MABILIONI |
1 |
2 |
1 |
3 |
2 |
7 |
9 |
2 |
16 |
18 |
140 |
306 |
|
19 |
MADIVENI |
1 |
11 |
18 |
29 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
300 |
0 |
|
20 |
MAKANYA |
1 |
13 |
6 |
19 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
497 |
0 |
|
21 |
MALINDI |
0 |
2 |
0 |
2 |
1 |
1 |
2 |
2 |
0 |
2 |
153 |
117 |
|
22 |
MASHEKO |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
130 |
75 |
|
23 |
MKOMBOZI |
3 |
22 |
0 |
22 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
48 |
1091 |
|
24 |
MOIPO |
1 |
23 |
12 |
35 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
219 |
143 |
|
25 |
MTII |
3 |
3 |
2 |
5 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
100 |
213 |
|
26 |
MVUREKONGEI |
4 |
2 |
3 |
5 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
184 |
|
27 |
MYAMBA |
0 |
1 |
0 |
1 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
245 |
321 |
|
28 |
NDUNGU |
3 |
4 |
0 |
4 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
687 |
|
29 |
NTENGA |
2 |
2 |
4 |
6 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
618 |
|
30 |
PARENI |
2 |
1 |
2 |
3 |
3 |
4 |
7 |
0 |
0 |
|
274 |
0 |
|
31 |
SAME |
0 |
2 |
0 |
2 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
756 |
0 |
|
32 |
SAWENI |
0 |
6 |
12 |
18 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
252 |
0 |
|
33 |
TAE |
0 |
6 |
8 |
14 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
145 |
72 |
|
34 |
VUDEE |
1 |
6 |
4 |
10 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
198 |
58 |
|
35 |
VUMARI |
0 |
7 |
8 |
15 |
6 |
4 |
10 |
4 |
5 |
9 |
96 |
459 |
|
36 |
VUNTA |
0 |
9 |
5 |
14 |
0 |
2 |
2 |
0 |
0 |
0 |
83 |
227 |
|
|
JUMLA |
57 |
214 |
164 |
378 |
38 |
50 |
88 |
26 |
48 |
68 |
8445 |
6916 |
|
IDARA YA MAJI
Upatikanaji wa Huduma ya maji
Upatikanaji wa maji vijijini ni 70% na Vijiji vyenye maji ni 75
4.2 Mpango uliopo kwa mji wa Same
Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe unalenga kuhudumia watu 456,931 ifikapo mwaka 2038 katika Wilaya za Same (watu 264,793), Mwanga (watu 177,085) na watu 15,053 katika Wilaya ya Korogwe, kwenye vijiji 38 na miji ya Same na Mwanga. Mifugo na viwanda vidogo pia vitanufaika na mradi huu.
Katika Vijiji 38 vitakavyonufaika Vijiji vya Same ni Hedaru, Mabilioni, Gavao, Makanya, Mgwasi, Bangalala, Chajo, Mwembe, Njoro, Ishinde, Ruvu Mferejini, Ruvu Jiungeni, Majengo, Bendera, Mkonga Ijinyu, Mgandu (vijiji 16 katika Wilaya ya Same)
4.3 Utekelezaji wa Mradi
KITENGO CHA ARDHI
Sekta ya ardhi ni mojawapo ya sekta iliyopo chini ya idara ya ardhi na maliasili inayosimamia masuala yote ya ardhi. Sekta ina sehemu 4 ambazo ni ardhi utawala, mipango miji, upimaji na ramani na uthamini. Idadi ya Vijiji vilivyopimiwa Ardhi, Idadi ya Vijiji vilivyofanyiwa Matumizi bora ya Ardhi, Idadi ya Migogoro Sugu ya Ardhi Mjini na Vijiji, Sababu za kutokea kwa Migogoro ya Ardhi na kusababisha migogoro hiyo kuwepo kwa muda mrefu, Mipango/Mikakati ya kumaliza Migogoro ya Ardhi, Mipango/Mikakati ya kuboresha Mji/Master plan, Hali ya Ukusanyaji wa Kodi za Viwanja na Nyumba pamoja na Idadi ya Miji yenye Sifa ya kuwa Miji Midogo ni kama ilivyoainishwa katika jedwali hapa chini;
Jedwali 5.1: Hali ya Utekelezaji wa Shughuli za Kitengo cha Ardhi
S/N |
VIJIJI VILIVYOPIMWA |
VIJIJI VILIVYOGAWANYIKA |
VIJIJI VYENYE MATUMIZI BORA YA ARDHI |
MIGOGORO SUGU |
MIGOGORO YA KAWAIDA |
SABABU ZA MIGOGORO |
MIKAKATI YA KUMALIZA MIGOGORO |
MIPANGO YA KUBORESHA MJI |
UKUSANYAJI WA KODI ZA ARDHI/MAJENGO |
MIJI YENYE SIFA YA KUWA MIJI MIDOGO |
1 |
Halmashauri ya Wilaya ya Same ina jumla ya vijiji 100 kati ya Vijiji hivyo vilivyopimwa vilikuwa ni vijiji 84, kati ya vilivyokuwa vimepimwa vijiji saba (7) vimegawanyika kati ya Vijiji hivyo sasa vilivyogawanyika vimezaliwa Vijiji 16 |
-Chajo kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Chajo na Nasuro. -Tae kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Tae, Heikonti na Rikweni. -Njoro kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Njoro na Emuguri. -Gavao Saweni kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Gavao Ngarito na Saweni. -Mabilioni kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Mabilioni, Ruvu mbuyuni na Chekereli.-Hedaru kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Hedaru, Kijomu na Gundusine. Bangalala kimegawanyika na kuwa Kijiji cha Bangalala na Mkanyeni. |
Duma, Lugulu, Kanza na Mtii, Makanya, Hedaru na Gavao Saweni. Kutokana na ufinyu wa bajeti Halmashauri imefanikiwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji saba (7) kupitia ufadhili wa wadau wa maendeleo kama TFCG na Ongawa. |
-Kijiji cha Makanya na Ruvu - Kijiji cha Mgwasi na Makanya, Kitongoji cha Kavambughu Ishinde. -Maore na Mheza. -Migogoro ya wakulima na wafugaji kata ya Ruvu. |
Migogoro ya kawaida haiwezi kuhesabika kwani huibuka na kupatiwa ufumbuzi. Baadhi ya wananchi wanadai kuchukuliwa maeneo yao bila kulipwa fidia. |
Kukosewa mipaka ya vijiji katika ramani zilizopimwa na Wizara ya Ardhi Wananchi kujenga bila vibali vya ujenzi kutoka mamlaka husika. |
Kukagua vijiji vyenye migogoro ya mipaka na kuiandikia Wizara barua ili waje warekebishe mipaka hiyo. Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji. Kubaini na kuhakiki uhalali wa madai ya wananchi ambao wanadai maeneo yao kuchukuliwa bila kulipwa fidia. Halmashauri kutafuta eneo kwa ajili ya kulipima ili kuwafidia wananchi hao. |
Maandalizi yanafanyika ili kutenga fedha katika bajeti ijayo ili kuandaa master plan (Mpango kamambe) wa mji wa Same. |
Ukusanyaji wa kodi za ardhi unaendelea vizuri. Kodi ya majengo ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo hukusanywa na mamlaka ya Mji mdogo wa Same kama mapato ya ndani. |
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ipo miji ya kibiashara ambayo inakuwa kwa kasi na ina sifa ya kuwa miji midogo ambayo ni Hedaru, Makanya, Kisiwani, Maore na Ndungu. |
Chanzo: Kitengo cha Ardhi
IDARA YA KILIMO
Fursa zilizopo Wilayani kwa ajili ya shughuli za kilimo ni pamoja na kuwa na bonde zuri lenye maji ya mito upande wa Same Mashariki ukanda wa tambarare. Eneo hili lina Skimu za umwagiliaji ambapo mazao mbalimbali ya chakula na biashara huzalishwa kama vile Mpunga, mahindi, maharage na mbogamboga. Upande wa Magharibi hutegemea zaidi Mto Pangani ambapo kuna kilimo cha umwagiliaji wa mazao ya mahindi, mpunga na mbogamboga. Upande huu ndio wenye eneo kubwa la malisho kwa upande wa ufugaji.
Mazao ya biashara yanayolimwa katika Wilaya yetu ni Tangawizi, Pamba, Fiwi na Kahawa, na Iliki. Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, mpunga na mtama. Mazao aina ya mikunde ni pamoja na maharage na fiwi, mazao mengine ni viazi vikuu, viazi mviringo na mihogo. Aidha Wilaya inazalisha pia aina kadhaa za mbogamboga na matunda ikiwemo ndizi, matango, tikitimaji, na nyanya.
Malengo ya Kilimo na Matarajio ya mavuno
Wilaya hii ni mojawapo ya Wilaya zinazokabiliwa na upungufu wa chakula mara kwa mara. Hali hii inasababishwa na mvua chache zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo huathiri ustawi wa mazao ya kilimo hasa maeneo ya tambarare.
Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017 halmashauri ya wilaya ya same imeweka malengo ya kulima hekta 39,700 ambapo kiasi cha tani 208,297 cha mazao mbalimbali kinatarajiwa kuzalishwa, ambapo tani 155,668 ni mazao ya chakula, tani 3,289 ni mazao ya biashara, tani 26,403 ni mbogamboga, tani 7,440 ni matunda na tani 15,506 ni Viungo.
Jedwali 6.1: Malengo ya kilimo na utekelezaji wa mazao muhimu
|
2015/2016 |
2016/2017 |
||||
LENGO |
UTEKELEZAJI |
LENGO |
||||
Ha |
Tani |
Ha |
Tani |
Ha |
Tani |
|
MAZAO YA CHAKULA |
||||||
Mahindi |
20,500 |
48,000 |
19,781 |
63,299 |
15,200 |
50,000 |
Mpunga |
3,200 |
19,200 |
3,300 |
16,500 |
3,200 |
24,000 |
Mtama |
500 |
500 |
100 |
80 |
500 |
800 |
Maharage |
1,500 |
1,320 |
1,250 |
1,100 |
1,500 |
1,400 |
Muhogo |
3,140 |
31,400 |
3,140 |
29,400 |
3,140 |
32,000 |
Ndizi |
3,200 |
32,000 |
3,200 |
31,100 |
3,200 |
32,000 |
Viazi Vitamu |
600 |
3,000 |
550 |
2,750 |
600 |
3,000 |
Viazi Mviringo |
350 |
3,500 |
300 |
3,000 |
350 |
3,500 |
JUMLA |
32,990 |
138,920 |
31,621 |
147,229 |
27,690 |
146,700 |
MAZAO YA BIASHARA |
||||||
Pamba |
80 |
120 |
50 |
60 |
80 |
120 |
Tangawizi |
1,200 |
13,500 |
1,250 |
14,500 |
1,350 |
15,500 |
Kahawa |
1,650 |
660 |
1,500 |
320 |
1,650 |
660 |
Fiwi |
4,000 |
8,000 |
3,500 |
5,250 |
4,200 |
8000 |
JUMLA |
6,930 |
22,280 |
6,300 |
20,130 |
7,280 |
24,280 |
Chanzo: Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
6.3 Hali ya Chakula na mikakati ya kumaliza njaa
Kwa mwaka 2015/16 hali ya chakula Wilayani Same ilikuwa ya kuridhisha kutokana na mvua kunyesha kiasi cha kutosha. Kimsingi mahitaji ya chakula (nafaka) kwa mwaka ni tani 81,101 ambapo kila mtu mzima anastahili kiasi kisichopungua gunia 3 za mahindi kwa mwaka, makadirio haya ni kutokana na idadi ya watu iliyopo ndani ya Wilaya (Watu 269,807), na hii ni kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Uzalishaji wa chakula katika maeneo ya skimu za umwagiliaji za Ndungu, Maore, Kisiwani na sehemu za Kata ya Bendera nao umeongezeka kutokana na jitihada kubwa zilizofanyika za kuongeza uzalishaji katika maeneo ya umwagiliaji.
Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuzuia/kupunguza upotevu wa
mazao ya nafaka na mikunde wakati wa kuvuna na kuhifadhi
(Post harvest loss handling).
Kuhakikisha elimu ya ukadiriaji wa mahitaji ya mazao ya chakula kwa wakulima ngazi ya kaya imetolewa.
Kutoa elimu kwa wakulima juu ya hifadhi na matumizi bora ya mazao ya chakula kwa maeneo ambayo yamepata mavuno mazuri msimu wa vuli hasa maeneo ya kilimo cha umwagiliaji.
Kutoa ushauri kwa wakulima kutekeleza kilimo cha mazaoyanayostahimili ukame na yanayotumia kiasi kidogo cha unyevu hadi kukomaa kama mazao jamii ya mizizi na mikunde na Mtama.
Kuhakikisha uimarishaji wa matumizi bora ya maji katika miundombinu ya umwagiliaji iliyopo na kuhakikisha kunakuwepo na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula kwa misimu miwili na wakulima wanazingatia ushauri wa wataalam waliopo vijijini.
Kwa kuwatumia Maafisa Ugani waliopo kuhakikisha wakulima wanatumia teknolojia bora na sahihi za uzalishaji mazao ya chakula na biashara kwa ajili ya uhakika na usalama wa chakula ngazi ya kaya.
Kuhimiza wafugaji walio na mifugo kuuza wakati bado ikiwa na hali nzuri ya kiafya na kununua chakula na kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia.
Kuhimiza wakulima waliopo maeneo ya umwagiliaji kulima mazao yenye thamani na ubora kwa uhakika wa kuongeza kipato hatimaye kumudu kujinunulia chakula cha kutosha.
Kuhamasisha wafanyabiashara wenye uwezo kununua chakula Katika maeneo yenye chakula cha ziada na kuleta kuuza katika maeneo yenye upungufu kwa bei nafuu/elekezi.
Halmashauri ya Wilaya iliteua kuendeleza mnyororo wa thamani kwa mazao mawili ya biashara ambayo ni Tangawizi na Mpunga.
Kwa zao la tangawizi Halamashauri ikishirikia na wadau wengine imekuwa na mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya umwagiliaji katika maeneo yanayozalisha tangawizi ili kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa zao hilo. Vilevile kwa kupitia mradi wa MIVARF Halmashauri imekuwa na mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya mawasiliano katika maeneo yanayolimwa zao hilo, pia kujengea uwezo wakulima wa tangawizi kwa kuwapa mafunzo ya kilimo bora cha tangawizi na kuwaunganisha na masoko.
Kwa zao la mpunga Halmashauri imekua na mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya umwagiliaji katika maeneo yanayolimwa mpunga na kutoa mafunzo kwa wakulima wa mpunga kwa kuanzisha mashamba ya mfano na mashamba darasa. Aidha Halmashauri imekua na mikakati ya kufufua na kuhakikisha kinu cha kukoboa mpunga katika skimu ya Ndungu kinafanya kazi ili kuongeza thamani ya zao la mpunga.
6.6.1 Kiwanda cha Tangawizi
Wilaya ya Same ni miongoni mwa Wilaya zinazozalisha Tangawizi kwa wingi hapa nchini, ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya tani 14,500 zinazalishwa kila mwaka. Wakulima wengi hasa wa maeneo ya milimani hutegemea na kutumia zao hili kama zao la biashara. Kutokana na hali hiyo Ushirika wa wakulima wa Tangawizi Mamba Myamba uliamua kujenga kiwanda ili kuongeza thamani ya zao la Tangawizi. Kiwanda kilizinduliwa na Mhe. Rais Mstaafu mnamo mwaka 2012. Baada ya kuzinduliwa kiwanda kiliweza kusindika zaidi ya tani 100 za Tangawizi na kuziuza.
Katika uendeshaji baadhi ya mitambo ilieonekana kutofanya kazi vizuri na hivyo kuhitaji kuboreshwa. Hali hii ilipelekea kiwanda kusimama kwa muda na hivyo Shirika la SIDO wametakiwa kutengeneza na kuirekebisha mitambo hiyo. SIDO ndio waliosanifu na kutengeneza mitambo yote ya kiwanda hicho na wanaendelea kushirikiana na ushirika pale mitambo inapoleta hitilafu.
Soko la Tangawizi mbichi na iliyosindikwa lipo la kutosha nje na ndani ya nchi. Serikali kupitia Mradi wa uboreshaji miundo mbinu ya masoko na uongezaji thamani (MIVARF) kwa kushirikiana na Shirika la Faida Mali inaendelea kusaidia ushirika huo kutafuta na kuwaunganisha na masoko ya uhakika. Tayari masoko yafuatayo yameshapatikana Kampuni ya Afri Tea, kampuni ya Tausi, TAQWA, Kampuni ya India market na Kampuni ya lion wattle. Wanunuzi waliopatikana wapo tayari kununua tangawizi iliyosindikwa mara tu kiwanda kitakapoanza tena kufanya kazi.Kwa sasa bei ya Tangawizi ni Tshs. 1300 – 1500 kwa kilo ya tangawizi mbichi.
Zipo Changamoto za msingi zinazokabili ushirika kwa sasa, ambazo zinasababisha kiwanda kisifanye kazi vizuri. Changamoto hizo ni pamoja Uelewa mdogowa viongozi wa ushirika waliopo kwa sasa juu ya usimamizi na uendeshaji wa kiwanda, na Ukosefu wa mtaji wa kutosha kununua malighafi (Tangawizimbichi) kuajiri na kulipa watumishi na kulipia gharama za uendeshaji.
Hatua zinaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha kiwanda kinafanya kazi vizuri. Hatua hizo ni pamoja na Kuimarisha na kujengea uwezo viongozi wa ushirika na wanachama ili kuweza kujipanga na kuepuka bei zisizokuwa na maslahi zinazopangwa na wafanyabiashara. Aidha mafunzo yametolewa juu ya usimamizi na utunzaji wa fedha ili baada ya kuwa na uelewa wa kutosha waweze kuomba na kupata mkopo kutoka kwenye taasisi za fedha na hatimaye kuendesha kiwanda.
KITENGO CHA MALIASILI NA MAZINGIRA
7.1.1 Misitu Iliyopo
Wilaya ya Same ina jumla ya hakari 256,503 za misitu ambayo ni sawa na asilimia 20.3 (20.3%) ya eneo lote la Wilaya ya Same ambalo ni Kilomita za mraba 5,186 (5,186Km2). Misitu hii ni ya aina mbalimbali kama kama misitu ya Kupandwa, Mataji wazi (Miombo Woodland), Hifadhi za Serikali (Cathment Forests), Hifadhi za Vijiji na Hifadhi za kimila (Itasio).
7.1.2 Wanyamapori
Kitengo cha wanyamapori kina dhamana ya kuhifadhi rasilimali wanyamapori iliyoko kwenye maeneo ya wazi yenye wanyamapori kama vile Ruvu, kuwarudisha wanyamapori watoka nje ya na hifadhi ya taifa ya Mkomazi. Maeneo yaliyohifadhiwa yanachangia uhifadhi wa bioanuai mbalimbali ili zisitoweke kama vile tembo, nyani, kiboko, nyati, simba, mbwa mwitu pamoja na aina mbalimbali za ndege.
Wilaya ya Same ina jumla ya Misitu ya Hifadhi 17 ambayo kati ya misitu hiyo, Misitu minne (4) ipo chini ya Serikali kuu, Misitu tisa (9) chini ya Halmashauri na Misitu (4) ipo chini ya Vijiji.
Usimamzi wake unategemea na mmiliki ambapo Misitu ya Serikali kuu husimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Misitu ya halmashauri husimiwa na Halmashauri ya Wilaya kupitia Kitengo cha Maliasili na Misitu ya Vijiji inasimamiwa na Vijiji kupitia Kamati za Maliasili za Vijiji. Misitu hii husimamiwa kupitia mipango ya usimamizi ya misitu husika ambapo shughuli za Doria, Upandaji wa Misitu, kulinda mipaka ya hifadhi na kuzuia matukio ya moto hufanyika.
Kitengo hiki kinatunza rasilimali wanyamapori kwa kuwalinda dhidi ya majangili kwa kufanya doria mara kwa mara kwenye maeneo yenye wanyamapori ili kuwalinda dhidi na ujangili. Rasilimali hii pia inatunzwa kwa kuhakikisha kuna udhibiti na usimamizi wa umilikaji wa nyara kama vile kutoa kibali kwenye ukamataji wa ndege kama vile kanga.
Endapo wanyamapori watatoka nje ya hifadhi ya taifa ya Mkomazi au maeneo ya wazi na kwenda kwenye makazi na mashamba ya wananchi, ni jukumu la watumishi wa kitengo cha wanyamapori kuwarudisha kwenye hifadhi.
Pia hufanyika udhibiti wa wanyamapori waharibifu hususani viboko ambao huvamia maeneo ya wananchi na wakati mwingine kusababisha vifo au madhara kwa watu na mazao mashambani kwa kuwarudisha katika makazi yao. Aidha kumekuwa pia na udhibiti wa wanyamapori kama tembo na simba wanaotoka katika hifadhi ya taifa Mkomazi. Zoezi la kuwarudisha hifadhini hufanyika haraka iwezekanavyo ili wasilete madhara kwa wananchi na mali zao. Viongozi wa kata au vijiji husika huimizwa kutoa taarifa pindi wanyamapori hao watakapoonekana katika maeneo yao. Pia elimu dhidi ya kujikinga na wanyamapori hao hatari kwa mali na uhai wa wananchi hutolewa kwa wananchi ili kuwasaidia katika kujikinga na wanyamapori hao na kutoa taarifa katika Idara ya Ardhi na Maliasili.
Misitu huchangia uchumi kupitia mapato yanayokusanywa na Halmashauri ya Wilaya na Serikali kuu kutokana na tozo mbalimbali za mazao ya misitu na mazao yasiyo ya misitu lakini yanayopatikana ndani ya misitu mfani ukindu. Tozo zinazokusanywa na Halmashauri ni zile zitokanazo na mbao, nguzo za umeme, simu na za kujengea, magome ya miti na mizizi kwa ajili ya dawa mbalimbali. Tozo zinazokusanywa na Serikali kuu ni zile za Usajili wa Biashara ya mazao ya misitu, kibali cha kusafirishia mazao ya misitu (Transit Pass) na mrahaba wa mazao ya misitu yaliyovunwa katika misitu ya asili.
Rasilimali hii inachangia kwenye uchumi kwa kutoa kibali cha ukamaji wa wanyamapori kama vile ndege aina ya kanga kwenye maeneo ya wazi yanayopatikana katika ya wilaya Same. . Kibali hicho kinatolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Wanyamapori na kuidhinishwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori na kumtaka Afisa Wanyamapori wa wilaya kumruhusu mdau huyo kukamata wanyama walioidhinishwa. Fungu la fedha lililotokana na ukamataji wa wanyamapori hao hugawiwa kwa Halmashauri husika.
Hata hivyo maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi kama vile Pori Tengefu (Ruvu-Same Game Controlled Area) yanakabiliwa na uharibifu mkubwa kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile uvamizi wa mifugo na shughuli za kilimo na ujangili kwenye maeneo yaliyohifadhiwa hivyo kusababisha kutokuwepo na wanyama wa kutosha kwa ajili ya shughuli za uwindaji ambazo zingeweza kuiletea halmashauri pato.
Upandaji wa miti hufanyika kwa kuzingatia lengo la mwaka liliowekwa kwa kila Wilaya ambapo kwa Wilaya ya Same lengo la mwaka 2015/2016 lilikuwa ni kupanda miti 1,500,000.
Aidha pamoja na zoezi la upandaji wa miti, uhamaishaji wa uanzishaji wa vitalu vya miti hufanyika kwa jamii ili kupata vyanzo vya miche kwa ajili ya kupanda. Mpaka sasa jumla ya vitalu vya miti 35 vimeanzishwa na jamii katika Kata za Hedaru, Vunta, Makanya, Maore, Kisiwani, Vumari, Mtii, Bombo na Myamba. Kitalu cha Halmashauri kilichopo Mwembe kina jumla ya miti 9,780. Jumla ya miti 1,351,763 imeshapandwa mpaka sasa ndani ya Wilaya kati ya miti 1,500,000 iliyotarajiwa kupandwa kwa Mwaka 2015/2016 sawa na asilimia 90.01 (90.01%).
IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI/RASILIMALI WATU
Tangu January 2016 hadi sasa kuna jumla ya Matatizo ya Watumishi...........yaliyoshughulikiwa na matatizo.......... yanaendelea kushughulikiwa
KITENGO CHA SHERIA
8.1 Idadi ya Kesi
Halmashauri ya Wilaya ya Same kama zilivyo Taasisi nyingine za kisheria ina uwezo wa kushitaki na kushitakiwa na katika kipindi cha 2015 hadi 2016 imekuwa na mashauri mbali mbali katika Mahakama ya Wilaya, Mahakama Kuu na Baraza la Ardhi na Nyumba Same.
Katika kipindi cha 2015 hadi 2016 Halmashauri imefungua kesi mbili moja Baraza la Ardhi na Nyumba Same ambayo ni shauri la Madai kati ya Mamlaka ya Mji Mdogo Same dhidi ya Helios Tower Infanco Tanzania Ltd na Mahakama Kuu Moshi ya Halmashauri ya Wilaya dhidi ya Eliwaha Mbaga na Wenzake. Kesi hizi ziko katika hatua za awali.
Katika kipindi cha 2015 hadi 2016 Halmashauri imeshitakiwa katika Mahakama ya Wilaya, Mahakama Kuu na Baraza la Ardhi na Nyumba Same na jumla ya mashauri matano(5) yalifunguliwa dhidi yake. Mashauri dhidi ya Halmashauri ni ya Eiza Mkaze dhidi ya Halmashauri na Mwingine, Ramadhani Kanyama Msuya dhidi ya Halmashauri, Christina Elieskia na Miriam Kajiru dhidi ya Mkutugenzi Mtendaji Wilaya, Cheavo Johnson Kihara dhidi ya TANESCO na Halmashauri ya Wilaya na Octavius Leole dhidi ya Halmashauri ya Wilaya. Kesi hizi bado ziko kwenye hatua mbalambali za usikilizwaji na ya Christina na mwenzake imeamuliwa kwa njia ya usulihishi CMA na imerudishwa TSC kwa hatua zaidi
Halmashauri ya Wilaya ya Same kupitia Kitengo cha Sheria imejipanga kushinda katika kesi zote kwa kuhudhuria Mahakamani kufuatana na kalenda za Mahakama na kutoa ushahidi thabiti kwa mujibu wa sheria pia kushawishi utatuzi wa migogoro nje ya mahakama pale inapobidi kufanya hivyo ili kuepuka upotevu wa muda na rasilimali fedha.
Kitengo cha Sheria kinashughulika na uandaaji wa mikataba mbalimbali baina ya Halmashauri na wadau wake na vilavile kuandaa mikataba ya watumishi walioruhusiwa kwenda masomoni.
Katika hili Kitengo kinazingatia kanuni,taratibu na sheria za mikataba ili kuhakikisha kwamba mikataba yote inayiongiwa na Halmashauri ina tija kwa Serikali,wananchi na Halmashauri kwa ujumla.
Katika kipindi cha 2015 hadi 2016 Halmashauri kupitia Kitengo cha Sheria imeweza kuanda Sheria Ndogo 7 zitakazo saidia utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri katika kuhudumia wananchi wa Wilaya ya Same. Sheria hizo ni Sheria Ndogo za Ushuru wa Mabasi Stendi, Sheria Ndogo ya Kudhibiti Unywaji Holela wa Vileo, Sheria Ndogo za Ushuru wa Pumba za Nafaka, Sheria Ndogo ya Kilimo cha Mazao yanayohimili Ukame, Sheria Ndogo ya Mahudhurio ya Lazima kwa Shule za Msingi na Sekondari, Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni na Sheria Ndogo ya Kuzuia Ujazaji wa Lumbesa.
Katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na jamii ya watu walio sawa na huru, Halmashauri ya Wilaya ya Same inashirikiana na Taasisi zisizo za kiserikali katika kutoa msaada wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii katika wilaya ya Same.
IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Kinachofanyika na kinachotarajiwa kufanyika ili kuhakikisha jamii inapata maendeleo ni;
Idadi ya vikundi vilivyopata usajili na vyenye nguvu ya kuweza kupata mikopon katika taasisi za kifedha ni kama ilivyoanishwa hapa chini;
Jedwali 5.1 Idadi ya Vikundi vyenye Nguvu
AINA YA KIKUNDI |
VIKUNDI VYA VIJANA |
VIKUDI VYA WANAWAKE |
VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI |
IDADI |
387 |
678 |
475 |
Chanzo: Idara ya Maendeleo ya Jamii
Jedwali 5.2: Idadi ya Vijana wasio na Kazi Maalum
WANAWAKE |
WANAUME |
JUMA YA VIJANA WASIOKUWA NAKAZI |
246 |
223 |
469 |
Chanzo: Idara ya Maendeleo ya Jamii
Kuwahamasisha vijana ili waweze kujiunga na masomo ya ufundi stadi kv uashi useremala na ujenzi ili waweze kujiajiri
Kwahamasisha vijana kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe mkopo yenye mashariti nafuu
Kuwahamasisha vijana ili wajiunge kwenye makundi kwa ajili ya kupatiwa elimu juu ya ujasiriamali
Kuwatengea vijana maeneo maalum kwa ajili ya kufanyia biashara ndogo ndogo
Kuwahamasisha vijana kutumia elimu mbalimbali katika kuanzisha ufugaji wa kuku na n g”ombe wa maziwa na nyama
Kuhamasiha vijana ili waweze kuanzisha viwanda vidovidogo kv, useremala uashi na ufndi vyuma.
Idadi ya SACCOS na Vikoba ni kama ifuatavyo;
Jedwali 5.3: Idadi ya SACCOS/Vikoba
S/N |
JINA LA SACCOS |
KATA/ENEO |
MMILIKI |
1 |
SAME KAYA SACCOS |
WILAYA |
WANANCHI/WANACHAMA |
2 |
SAME TEACHERS SACCOS |
WILAYA |
WAALIMU WANACHAMA |
3 |
KISIWANI SACCOS |
KISIWANI |
WANACHAMA |
4 |
MKONAPA SACCOS |
VUMARI |
WAFANYAKAZI/WANACHAMA |
5 |
NASHENGENA SACCOS |
MAORE |
WANACHAMA. |
6 |
KURUGENZI SACCOS |
WILAYA |
WAFANYAKAZI |
7 |
MARANATHA SACCOS |
SAME |
WAUMINI WASABATO |
8 |
GAHENDU |
SAWENI |
WANACHAMA WA GAVAO, HEDARU, GUNDU. |
Chanzo: Idara ya Maendeleo ya Jamii
Fedha zilizopangwa kutolewa na Halimashauri kwa kipindi cha 2015/16 ni jumla ya TShs. 112,000,000/= na zilizotolewa ni Tshs. 26,000,000/= na idadi ya vikundi vilivyopatiwa mikopo ni 14.
Kwa upande wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017, Fedha zilipangwa kutolewa kwa kipindi cha 2016/17 ni Tsh. 146,000,000/=
KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
Kwa kipindi kinachoishia mwezi Agosti, 2016, Halmashauri ilikuwa na hoja za ukaguzi 54 zinazohitaji majibu yatakayopelekea hoja hizo kufungwa.
Uongozi wa halmashauri umeweka mikakati ili kupunguza hoja za ukaguzi, mikakati hiyo ni:-
Kutumia mashine za elektroniki zinazowasiliana na makao makuu ya halmashauri kukusanyia mapato toka katika Kata, itasaidia kuhakikisha mapato yote yaliyokusanywa kufahamika na kuwasilishwa na kuondoa tatizo la upotevu/kutokuwasilishwa wa vitabu vya kukusanyia mapato
Kuendelea kuwasiliana na TAMISEMI , ili kuweza kupata wakuu wa Idara/au kuwathibitisha makaimu wakuu wa idara waliopo, hii itasaidia kupunguza madeni kwa wakuu wa idara wanaokaimu kwa muda mrefu
Kuendelea kufuatilia uwepo wa watumishi hewa kwa kufanya uhakiki wa watumishi kila mwezi
Kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuibua vyanzo vipya vya mapato ya ndani , na kuendelea kuwasiliana na Hazina /Serikali kuu ili iweze kuleta fedha kwa wakati kulingana na bajeti , hii itasaidia halmashauri kutekeleza kazi kulingana na bajeti na kuwa na uwezo wa kupeleka asilimia 10 ya mapato ya ndani yaliyokusanywa katika mfuko wa wanawake na vijana
Kuendelea kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo ambazo hazijawasilishwa toka Hazina na kuomba fedha hizo kuwasilishwa kwa wakati
Kutenganisha thamani ya majengo na ardhi kwa kufanya uthaminishaji
Kuwaelekeza wakuu wa Idara/vitengo/watumishi kutekeleza majukumu kwa kufuata taratibu na sheria
Kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani katika usimamizi wa fedha/manunuzi/ubora
Kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika mapema mara fedha zinapowasili
Kuimarisha Kitengo cha ukaguzi wa ndani kwa kuwajengea uwezo katika mifumo, mfano, mfumo wa ukusanyaji wa mapato kielektronic, LAWSON, EPICOR, PLAN REP.
Upungufu wa mkaguzi mmoja kulingana na Ikama
Kukosekana/kutokuwasilishwa kwa fedha , kumepelekea kaguzi kutofanyika kulingana na mpango wa ukaguzi wa mwaka
Wakaguzi kutokujengewa uwezo kuhusiana na mifumo ya ukusanyaji wa mapato kielektronic, LAWSON, EPICOR, PLAN REP
IDARA YA UJENZI
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 idara ya ujenzi ilitengewa kiasi cha Tshs 956,160, 000/= kutoka mfuko wa barabara (Road fund) hadi kufikia 30/06/2016 halmashauri imepokea kiasi cha Tsh 215,460, 000/= tu. Miradi inayoendelea kutekelezwa kwa kazi za barabara ni kama ifuatavyo:-
Jedwali 11.1: Idadi ya Miradi inayoendelea kutekelezwa
Na. |
Jina la mradi |
Jina la Mkandarasi |
Gharama ya Mkataba |
Maoni |
1 |
Matengenezo ya kawaida na muda maalumu barabara za Makanya – Chankoko na Njia panda – Chankoko - Mvungwe |
OLDONYOMAS ENGINEERING |
105,577,550 |
Kazi zinaendelea |
2. |
Matengenezo ya kawaida muda maalumu na miundo mbinu ya maji barabara za Mpirani -Kadando,Maore- Vuje,Ndungu-Makokane na Mpirani-Bombo |
CORNEL (T) LTD |
88,030,950 |
Kazi zinaendelea |
3. |
Matengenezo ya kawaida, sehemu korofi na matengenezo ya muda maalumu barabara za Same -Ruvu-Mferejini na Ishinde-Vumari. |
CORNEL (T) LTD |
77,881,180 |
Kazi zinaendelea |
4. |
Matengenezo ya kawaida,sehemu korofi na miundombinu ya maji ya mvua barabara za Kisiwani -Msindo,Mwembe- Mhezi,Mbuyuni-Marindi na Ijinyu - Kamadufa |
MUGENZO CO. LTD |
64,431,540 |
Kazi zinaendelea |
5. |
Matengenezo ya kawaida na sehemu korofi barabara za Saweni-Gavao -Bwambo,Kidenge- Mwala na Hedaru- Makasa-Kirangare |
HAMORIC INVESTMENT (T) LTD |
34,499,660 |
Kazi zinaendelea |
6 |
Matengenezo ya kawaida na miundombinu ya maji barabara za Majevu-Dido- Njoro, Minyala -Mbono-Mgagao na dengude- Dido. |
KIV CO.LTD |
70,825,960 |
Kazi zinaendelea |
7 |
Matengenezo ya kawaida muda maalumu na miundo mbinu ya maji barabara za Same Mjini. |
SIMJO TECH CO.LTD |
128,118,500 |
Kazi zinaendelea |
8 |
Matengenezo ya kawaida na sehemu korofi barabara za Bangalala -Chome na Chome - Ikokoa |
MSHUNGA INVESTMENT LTD |
22,774,000 |
Kazi zinaendelea |
Chanzo: Idara ya Ujenzi
11.2 Ubora wa Miradi inayotekelezwa.
Miradi inayotekelezwa ipo katika ubora unaotakiwa kwa kuzingatia taratibu za mikataba.
Uhakiki wa wakandarasi wanaopatiwa kazi/tenda hufanyika kipindi cha kufanyiwa uchambuzi wa zabuni (Tender evaluation) wa wazabuni wanapoomba tenda/zabuni.
IDARA YA FEDHA
12.1 Utangulizi
Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa mwaka wa fedha 2015/2016 iliidhinishiwa kupokea fedha Tshs. 43,351,398,248 hadi kufikia Juni 2016 ilikuwa imepokea Tshs. 41,467,376,632 sawa na asilimia 95.
Jedwali hapo chini linaonyesha vyanzo vya Halmashauri, Makadirio, hali halisi, asilimia, utekelezaji na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti hiyo kama ifuatavyo:-
Jedwali 12.I: Bajeti ya Halmashauri 2015/2016
Na. |
Vyanzo vya Halmashauri |
Makadirio |
Hali halisi ya makusanyo ya Fedha |
Asilimia |
Utekelezaji |
Changamoto |
1. |
Vyanzo vya ndani |
2,274,732,000 |
1,933,320,538 |
85 |
Fedha za mapato ya ndani zimechangia miradi ya maendeleo;- Mchango wa madawati Tshs. 212,021,051 Kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa maabara na ununuzi wa vifaa vya maabara Tshs. 37,810,000 Kuwezesha unununzi wa kipaza sauti ukumbi wa Halmashauri Tshs. 4,613,400 Ukamilishaji wa kituo cha kilimo Tshs. 5,600,000 Kuchangia ujenzi wa ofisi mpya ya Mkurugenzi Tshs. 30,000,000 Kuchangia ukarabati wa shule za msingi Tshs. 10,000,000 Kufunga mfumo wa kieletronic Tshs. 75,417,808 Kuchangia mfuko wanawake na Vijana Tshs. 22,150,360 na Uendeshaji wa shughuli za ofisi vikao na ulipaji wa mishahara kwa watumish wanaolipwa na mapato ya ndani. |
-Mwamko mdogo wa wananchi kulipa kodi na ushuru. -Baadhi ya Vijiji kutokuwa na Maafisa watendaji Vijiji. -Shughuli za uchaguzi Mkuu -Mabasi kutoingia stand. |
2. |
Fidia ya vyanzo vilivyofutwa |
200,023,000 |
31,977,000 |
16 |
Shughuli za uendeshaji wa ofisi zilifanyika kulingana na fedha iliyotolewa. |
Fedha kuto kutolewa kulingana na Bajeti. |
3. |
Serikali kuu - Ruzuku – OC |
2,327,258,000 |
1,769,377,000 |
76 |
Idara ilitekeleza shughuli zilizopangwa kutokana na fedha zilizopokelewa |
Fedha kutopokelewa kwa wakati. Fedha kuto kutolewa kulingana na Bajeti. |
4. |
Mishahara |
32,612,236,000 |
31,899,123,217 |
98 |
Mishahara ililipwa kwa Watumishi kwa wakati |
Madeni ya Malimbikizo ya mapunjo ya mishahara. |
5. |
Miradi ya maendeleo.
EGPAF EASTERN ARC MIVAF TANAPA Performance For Result (P4R) Ujenzi / Uboreshaji Miundombinu- Kibacha TASAF |
3,177,944,465
239,474,300
15,400,000 21,300,000
18,000,000 72,377,209
221,902,836
2,170,750,438 |
3,147,136,623
166,711,771
15,400,000 21,300,000
18,000,000 72,377,209
221,902,836
2,170,750,438 |
99 70 100 100 100 100 100 100 |
Utekelezaji wa miradi umefanyika kulingana na fedha iliyotolewa na lengo lililokusudiwa |
Kuchelewa kupokea fedha kwa wakati. |
|
Jumla |
43,351,398,248 |
41,467,376,632 |
95 |
|
|
Jedwali 12.2: Bajeti ya Halmashauri 2016/2017
Vyanvo |
Makadirio |
Mikakati ya kufikia malengo |
Vyanzo vya ndani |
2,335,264,000 |
Kuhakikisha Takwimu na Bajeti za Mapato zinaandaliwa kutoka kwenye kila Kijiji pia itawezesha Kijiji kuwa na makadirio ya asilimia 20 itakayorejeshwa Kijijini. Kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na malengo ya kukusanya mapato Kuhakikisha kila Kata inakuwa na machine ya kukusanyia mapato. Kuhakikisha kuna kuwa na ufatiliaji wa mara kwa mara wa mapato na ufatiliaji wa kushtukiza Kubuni vyanzo vipya vya mapato Kuendelea kutoa elimu kwa walipa kodi na ushuru ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na ushuru. Kuendelea kufatilia mikakati iliyowekwa na kufanya tathmini.. |
Fidia ya vyanzo vilivyofutwa |
192,362,000 |
|
Serikali kuu - Ruzuku – OC |
3,245,916,850 |
|
Mishahara |
39,475,823,940 |
|
Miradi ya maendeleo |
11,251,205,280 |
|
JUMLA |
56,500,572,071 |
|
12.2 Halmashauri inakusanya mapato Kwa njia ya kieletroniki Na kupitia mfumo WA LGRCIS ambao umeunganishwa na NMB
Halmashauri ilianza kutumia mashine ya kukusanyia mapato ngazi ya Kata, mwezi Julai 2016. Tumeshanunua mashine 35 kwa sasa Kata zinazotumia mashine ni Kata 17 nazo ni Mamlaka ya Mji mdogo kata 3, Hedaru, Makanya, Njoro, Bendera, Kihurio, Ndungu, Maore, Kisiwani, Ruvu ,Vumari, Kalemawe, Bwambo, Myamba na Mpinji Sambamba na ilo tumeshanunua Mashine zingine 30 za kukusanyia mpato.
12.3 Vyanzo Vipya Vya Mapato
Halmashauri imeanza mpango wa kuanzisha soko la mazao katika Kata ya Ruvu ambalo litawezesha Halmashauri kukusanya ushuru wa mazao, tayari timu ya Wilaya imeshakutana na serikali ya Kijiji kwa ajili ya kuwashirikisha kupata eneo sahihi.
Halmashauri imeanza mpango wa kuanzisha mnada wa mifugo Kata ya Njoro siku ya Alhamisi na Same siku ya Jumapili.
12.4 Kudhibiti Wizi /Upotevu
Halmashauri imeweka utaratibu wa kuwasilisha mapato mara mbili kwa Mwezi na ukaguzi wa nyaraka za fedha unafanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kushirikisha Kitengo cha Ukaguzi wa ndani.
12.5 Ufanisi wa Malipo
Halmashauri inafanya malipo yote kupitia mfumo wa malipo wa EPICOR, mfumo huu unategemea uwepo wa fedha kwenye kasma na kifungu husika, hivyo kasma na kifungu vinapokuwa na fedha malipo huchukua siku 3 mhusika kulipwa. Iwapo madai yanafika ofisini pasipo kuwa na fedha mhusika hufahamishwa kwa barua kusubiri mpaka hapo itakapopatikana.
IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI
Mipango kiidara ipo, na idara hii ndiyo yenye jukumu la kuunganisha Mipango na shughuli za Idara mbalimbali kupitia mfumo ujulikanao kama Medium Term Expenditure Framework (MTEF). Miradi yote ya kila Idara ngazi ya Kata na Vijiji pamoja na miradi ngazi ya Wilaya huunganishwa na kuratibiwa na Idara hii, ili kuleta ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii.
Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji pia ina jukumu la Kuratibu na kusimamia uandaaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Halmashauri (Strategic Plan). Zoezi hili hufanyika kila baada ya Miaka mitano katika Halmashauri, ambapo Idara inaanda Mpango Mkakati mpya au kuhuisha Mpango Mkakati uliopo. Hadi sasa Idara bado ipo kwenye mchakato wa kuhuisha Mpango Mkakati wa Halmashauri ambapo mda sio mrefu zoezi hili litakamilika.
Pato la Mwananchi (GDP) ni jambo muhimu sana la kuzingatia ili kupima halihalisi ya uchumi kwa kila Mwananchi katika Jamii. Hali ya Pato la Mwananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ni Shilingi 720,000/=
Katika Halmashauri ya Wilaya, Takwimu zote za Kiuchumi na Kijamii zipo na zinatumika ipasavyo katika utekelezaji shughululi mbalimbali za maendeleo. Takwimu kama vile Idadi ya Watu ndizo tunazozitumia sana katika utekelezaji wa shughuli za Miradi ya maendeleo. Takwimu zingine ni za sekta mbalimbali kama vile Takwimu za Elimu, Afya, Kilimo, Mifugo na zingine mbalimbali.
Hali ya usambazaji wa Takwimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ni ya kuridhisha, kwani Takwimu hizi zinasambazwa pale zinapohitajika na kwa wakati.
Idara hii pia ina jukumu la kufanya ufuatiliaji kwa kina juu ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Miradi ya Maendeleo pamoja Kuratibu, kusimamia, kutathmini na kufanya uhakiki wa programu za maendeleo ya Halmashauri. Ufuatliaji wa utekelezaji wa shughuli za Miradi inayotekelezwa Vijijini sio ya kuridhisha sana ukilinganisha na miaka iliyopita. Hali ya ufuatiliaji wa Miradi inaathiriwa na uhaba wa Fedha hasa baada ya Kifungu cha Monitoring and Evaluation katika Bajeti ya Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo (LGCDG) kufutwa. Idara imekuwa ikipata changamoto sana juu ya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri. Idara imejitahidi na inaendelea kujitahidi sana kufuatilia miradi ya maendeleo katika Halmashauri kwa kuomba Fedha kutoka kwenye Mfuko Mkuu (GF). Pia ili kuendelea kusimamia ufanisi wa miradi inayotekelezwa, Idara inawatumia Watendaji wa Kata na Vijiji kwa kufanya mawasiliano ya karibu sana kipindi miradi inatekelezwa jambo ambalo linasaidia pia katika ufanisi wa Miradi ya Maendeleo.
Pamoja na majukumu mengine Idara hii inatumia Mfumo wa kuhakikisha Utekelezaji wa Shughuli za Miradi ndani ya Idara na nje ya Idara. Maelekezo na miongozo hutolewa kutoka kwenye Ofisi ya Mkurugenzi na kuletwa ndani ya Idara. Idara hii inasimamia Mipango yote ya shughuli mbalimbali ndani na nje ya Idara. Idara zote huandaa Mipango yao na kazi kubwa ya Idara hii ni Kuratibu na kusimamia mchakato wa Mipango shirikishi na uandaaji wa bajeti ya Halmashauri. Mipango hii ya Halmashauri kiidara huunganishwa katika mfumo mmoja ujulikanao kama Medium Term Expenditure Framework (MTEF). Pia Idara hii inafanya kazi za Kuratibu mchakato wa menejiment ya Takwimu mbalimbali za Halmashauri na kupendekeza sera na mipango inayohitajika. Kazi nyingine ya Idara hii ni Kufanya makisio ya idadi ya watu ya Wilaya (Population Projection) kwa kila mwaka ambapo zoezi hili ni muhimu sana kwani husaidia katika swala zima la uandaaji wa Maoteo [Indicative Planning Figure (IPF)] wakati wa kipindi cha mchakato wa uandaaji wa Mpango na Bajeti. Yote hii ni kuhakikisha kunakuwa na usawa katika ugawaji wa huduma za kiuchumi na kijamii pamoja na Maendeleo kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ina Dira, Dhima na Desturi kama ifuatavyo;
Dira: Kuwa na Jamii yenye Maisha bora, iliyohamasika na kuendana na mabadiliko endelevu ya Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ifikapo mwaka 2016.
Dhima: Kutoa Huduma bora kwa Jamii kupitia matumizi sahihi ya Rasilimali, kuwajengea uwezo, Utawala bora na kuwa na Maisha bora.
Desturi: Kutoa huduma kwa Jamii kwa kutumia mbinu shirikishi (Participatory Approach) ili kuleta ufanisi wa huduma ya utawala bora na Huduma kwa Jamii. Idara ina uhuru wa kumiliki desturi yake ya kutoa huduma katiaka jamii kwa kushirikisha Idara zote na Vitengo katiaka Halmashauri pamoja na ngazi za Kata na Vijiji. Idara inaendelea kufanya shughuli zake kwa kufuata desturi yake ya ushirikishwaji wa jamii.
KITENGO CHA MANUNUZI
Kitengo cha manunuzi ni miongoni mwa kitengo (6) vilicho chini ya Mkurugenzi Mtendaji, aidha Majukumu ya kitengo cha manunuzi ni kama ifuatavyo;-
Kusimamia shughuli zote za manunuzi
Kutekeleza maagizo ya Bodi ya zabuni
Sekretarieti ya bodi ya zabuni
Kupanga manunuzi na mpango wa kuuza mali za serikali
Kupendekeza manunuzi njia ya manunuzi na kuuza mali za serikali kwa njia ya zabuni
Kuandaa mahitaji mahitaji taarifa ya mahitaji
Kuandaa kabrasha za Zabuni
Kuandaa matangazo ya Zabuni
Kuandaa Mikataba ya Zabuni
Kutoa Mikataba iliyo idhinishwa
Kwa kipindi cha Mwaka 2015/2016 zabuni zilizo tangazwa ni kama ifuatavyo;
Ujenzi wa barabara zabuni zilizo tangazwa ni 9
Ujenzi wa majengo zabuni zilizotangazwa ni 7
Idadi ya wa tumishi katika kitengo ni 4
Upungufu uliopo ni 1
Kwa upande wa Kazi zilizotangazwa hakuna kazi zozote zenye migogoro na Kesi katika Halmashauri yetu.
14.3 Changamoto
Sheria ya Ununuzi Umma Kurefusha mchakato wa Manunuzi kwa serikaliza Mitaa
Upungufu wa Mtumishi (1) katika kitengo cha Manunuzi
Uelewa Mdogo wa sheria kwa baadhi ya Idara tumizi (User departiments)
14.4 Mikakati
Kushauri wakuu wa Idara na vitengo Kuanzisha michakato ya manunuzi kwa wakati
Tayari Kitengo kilisha omba kibali cha kupatiwa Mtumishi mmoja.
Tayari kitengo cha Manunuzi kimefanya mafunzo kwa wakuuu wa idara na vitengo na kinaendelea
KITENGO CHA TEHAMA
Kusimamia taasisi zote za Serikali zilizopo ndani ya Wilaya kuwa na matumizi sahihi na bora ya TEHAMA.mfano huduma ya mtandao (internet).
Kutumia baadhi ya miundo mbinu ya TEHAMA kwaajili ya kutumika kama vyanzo vya mapato ndani ya Halmashauri mfano Internet Café,
Kufuatilia,kusimamia na kujua gharama za uendeshaji na uanzishwaji wa Gazeti au makala ya Wilaya kiujuma.
Kufuatilia,kusimamia na kujua gharama za uendeshaji na uanzishwaji wa Redio ya Wilaya
Ifuatayo ni Mipango ya uhimarisha wa mawasiliano kati jamii na halmashauri:-
Kama ilivyo katika Halmashauri nyingine,Halmashauri ya Wilaya ya Same inayo mifumo ambayo inayotumia katika kutekeleza majuku ya kila siku,mifumo ni EPICOR-FEDHA, LAWSON- UTUMISHI, PSSN-TASAF,TOMSHA-TACAIDS, BEMIS-ELIMU MSINGI/SEKONDARI, LGRCIS- UKUSANYAJI WA MAPATO na LMS- ARDHI.
Mifumo yote iyo kimsingi imeboreshwa na ufuatiliaji wake upo vizuri kwani kila wakati imekuwa ikitumika bila ya Tatizo lolote,kwa kushirikiana na TAMISEMI.Pamoja na ayo yote changamoto kubwa iliyopo ndani ya Kitengo cha TEHAMA ni ufinyu wa Bajeti hivyo baadhi ya shughuli zimekuwa ngumu kutekelezeka kabisa.
Wilaya ya same ina kanda tatu za ufugaji wa mifugo ambazo ni ukanda wa juu (Milimani), ukanda wa kati na ukanda wa tambarare (Magharibi na Mashariki). Ukanda wa milimani mifugo hufugwa na kulishwa ndani (zero grazing and tethering) kanda zinazobaki yaani ukanda wa kati na tambarare mifugo hufugwa huria (free range) kwa mifugo asili na kufugwa/kulishwa ndani (zero grazing and tethering) kwa mifugo chotara.
Eneo kubwa la malisho kwa ukanda wa tambarare ya Mashariki limepakana na Mbuga ya Taifa ya Mkomazi na ukanda wa tambarare ya Magharibi malisho haya yamepakana na mto Pangani. Wilaya ya Same ina mifugo mingi kuliko wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro. Eneo la malisho (Range land) lililoainishwa lina ukubwa wa hekta 356,200 ambazo ni asilimia 67.25 ya eneo lote la wilaya. Idadi ya mifugo wilayani ni kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini;
Jedwali 16.1: Aina na Idadi ya Mifugo inayofugwa Wilayani
AINA YA MIFUGO |
IDADI YA MIFUGO |
JULMA YA MIFUGO |
||
ASILI |
CHOTARA |
|||
Ng’ombe |
176,484 |
|
184,380 |
|
Mbuzi |
112,427 |
|
112,905 |
|
Kuku |
210,839 |
|
231,760 |
|
Kondoo |
70,903 |
70,903 |
||
Punda |
6,426 |
6,426 |
||
Nguruwe |
2,811 |
2,811 |
||
Ngamia |
18 |
18 |
||
Bata |
9,990 |
9,990 |
||
Mbwa |
8,796 |
8,796 |
Chanzo: Idara ya Mifugo na Uvuvi
Katika halmashauri ya wilaya ya Same, kuna aina kuu tatu za ufugaji. Aina hizo ni;
i). Ufugaji huria ambao unatumika kufuga Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Punda, Mbwa, Bata, Kuku na Ngamia
ii). Ufugaji nusu huria ambao unatumika kufuga Kuku na Bata
iii). Ufugaji wa ndani na/ au kufunga ambao unatumika kufuga Ng’ombe na Mbuzi chotara wa maziwa, Kondoo, Kuku, Bata na Mbwa.
Aidha kuna mikakati mbalimbali ambayo imewekwa ili kuhakikisha kuwa ufugaji bora na wakisasa unatekelezwa na wafugaji kama ifuatavyo;
i). Kushirikiana na idara ya ardhi ili kuhakikisha mipango ya matumizi bora ya ardhi inatekelezwa ili kuepusha migogoro kati ya wafugaji na wadau wengine wanaotumia ardhi.
ii). Kuwaelimisha wafugaji juu ya kanuni za ufugaji bora na faida zake ikiwemo aina bora na sahihi ya ufugaji pamoja na uvunaji wa mifugo ili kuendana na eneo la nyanda za malisho lililopo.
iii). Kuboresha koo safu za mifugo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo kwa kutumia uhimilishaji na madume yaliyoboreshwa, mitetea pamoja na majogoo bora na kupunguza idadi ya mifugo na kuwa na mifugo michache yenye tija. Hili linafanyika katika ngazi ya mtu mmojammoja, kaya na vikundi.
i). Kushirikiana na sekta binafsi zinazofanya kazi za kuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi ikiweo ujenzi wa machinjio za kisasa, masoko ya bidhaa za mifugo na viwanda vidogo vya kusindika mazao yatokanayo na mifugo.
ii). Kuboresha koo safu za mifugo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo kwa kutumia uhimilishaji na madume yaliyoboreshwa, mitetea pamoja na majogoo bora na kutoa elimu ya ufugaji bora ili kuongeza kipato ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla.
iii). Kudhibiti magonjwa ya mlipuko kwa kufanya chanjo, tiba za mifugo, uogeshaji wa mifugo pamoja na usimamizi wa minada ili kuongeza ubora na thamani ya mazao yatokanayo na mifugo.
iv). Kutoa huduma bora ya ukaguzi wa nyama kwa lengo la kulinda afya ya jamii na kuzuia magonjwa ya kuambukiza (Zoonoses).
v). Kusajili vituo vya huduma za mifugo ili kusogeza huduma za mifugo karibu na wafugaji na kusimamia utoaji wa huduma bora za mifugo zinazotolewa na wadau wa sekta binafsi.
vi). Kutoa elimu juu ya ufugaji bora wa samaki kwenye mabwawa ya jamii na binafsi na kuzuia uvuvi haramu ili kuongeza kiwango bora cha uzalishaji wa samaki.
KITENGO CHA NYUKI
Nta - Wastani wa Kilo 2,519 kwa mwaka
17.3 Mikakati Ya Kukuza Uzalishaji Wa Mazao Ya Nyuki
17.4 Mikakati Ya Kufanya Zao La Asali Kuwa Zao La Kiuchumi Linalotegemewa Na Wilaya
Kuanzisha utaratibu wa kukagua mazao ya nyuki ili kudhibiti ubora wake.
Kuanzisha na kusimamia vituo vya kukusanyia na kuchakata asali.
Kuwa na utaratibu wa kupima asali ili kudhibiti ubora wake.
Kuanzisha utaratibu wa kuweka asali katika madaraja ili kupata bei nzuri. (Viwango vya ubora wa asali vitumike)
Kutoa mafunzo na kuelimisha wafugaji nyuki (wazalishaji) na wafanyabiashara wadogo kuhusu njia bora zaidi za kutunza mazao ya nyuki.
Kuhakikisha vifaa vya uvunaji, uchakataji, ufungashaji, uhifadhi na usafirishaji wa asali vinapatika kwa urahisi.
Kuandaa mwongozo wa sheria ndogo kuhusu makusanyo ya mapato (ushuru) utokanao na mazao ya nyuki kwa wafanyabiashara wanaosafirisha nje ya Wilaya.
KITENGO CHA UWEKEZAJI
Halmashauri ya Wilaya ya Same ni miongoni ya wilaya 6 katika Mkoa wa Kilimanjaro ambayo inafursa za uwekezaji katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta ya kilimo, madini, usafiri, utalii, ujenzi, uvuvi, ufugaji, mifugo, viwanda, biashara na kijamii (Elimu, Afya na Maji) na Kiutamaduni (Michezo na Utamaduni).n.k. Uwekezaji kwa mujibu wa kitaifa pia unalenga katika kuwezesha maendeleo ya nchi lakini pia kwa wakazi kufaidika na fursa mbalimbali.
18.1 Idadi ya wawekezaji waliopo na aina ya uwekezaji
Na |
Jina la mwekezaji |
aina ya uwekezaji |
Mahali ulipo |
Maelezo |
1. |
Willy Enterprises |
Madini ya boxite |
Mwembe/Chome |
Mwekezaji anachimba madini hayo na kupeleka katika nchi ya Kenya |
2. |
Umoja wa wakulima wa Tangawizi |
Kilimo cha tangawizi |
Myamba |
Umoja wa ushirika unawanachama zaidi 600 |
3. |
|
Kiwanda cha Tangawizi |
Myamba |
Kiwanda kimesimama |
4. |
Miller International Agrovet |
Kilimo cha vitunguu |
Kijiji cha Jiungeni |
Miller inamiliki eneo la zaidi ya ekari 400. |
5. |
SMK |
Kilimo cha vitunguu |
Kijiji cha Jiungeni |
Anamiliki zaidi ya ekari 200 za vitunguu |
6. |
Tona lodge |
Utalii/Asili |
Kata ya Mshewa |
Uwekezaji unafanya shughuli za utalii wa asili |
7. |
MKUNAPA |
Utalii/wanyama pori |
Mbuga ya Mkomazi |
Eneo la uwekezaji linalolimilikiwa ni ekari 3245. |
8. |
KIDC |
Kiwanda cha vikombe |
Kata ya Same |
Kiwanda hakifanyi kazi kwa ufanisi kutokana na uongozi. |
9. |
Makampuni ya simu |
Mitandao ya simu |
Wilaya ya Same |
Makampuni ya simu ya Airtel, Haloteli Tigo, Vodacom na Zantel |
10. |
Mashirika ya Fedha |
Huduma ya ya fedha |
Wilaya ya Same |
NMB, CRDB, Same Kaya SACCOs, CWT, Amacha, BRAC n.k. |
19.2 Vivutio vya uwekezaji vilivyopo
Na. |
Aina ya kivutio cha uwekezaji |
Vivutio |
1. |
Mbuga ya Taifa ya Mkomazi yenye ukubwa wa ekari 3245 |
Wanyama wa aina mbalimbali, ndege na eneo lenye miti ya asili |
2. |
Uchimbaji wa madini |
Eneo la uchimbaji jasi, green garnet, green tourmaline, rhodilite na boxite. |
3. |
Bwawa la Kalimawe na Karamba |
Aina ya samaki kama vile: Tilapia, perege, kambale na mkunga. Bwawa ili lina kilomita za mraba 3. |
4. |
Msitu wa Shengena hekta 27,880 |
Aina ya miti, vipepeo, nyuki, ndege, mbega, nyani, tumbili na maji yanayotiririka kwa mwaka mzima. |
5. |
Mawasiliano na miundo mbinu |
Kuna barabara zinazopitika kwa mwaka mzima, mitandao ya simu na usafiri wa kampuni za Kilenga, Kimbwe na Phiba. |
6. |
Ujenzi wa viwanda |
Kuna maeneo ya ujenzi wa viwanda kama:- saruji n.k |
7. |
Mto Pangani |
Mto Pangani unaopita katika Kata ya Ruvu wenye urefu wa km 91, maji yanafaa kwa kilimo cha umwagiliaji na ufugaji wa samaki. |
8. |
Huduma za Malazi (Hotel) |
Katika Wilaya tuna wawekezaji katika huduma za malazi km Elephant Motel, Orlando, Nzoroko n.k. |
Chanzo: Kitengo cha Uwekezaji
18.3 Maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji
Halmashauri ya wilaya ya Same imetenga jumla ya ekari kama ifuatavyo:-
-Eneo la Kitamri Halmashauri imetenga ekari 150 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda
-Eneo la Kata ya Makanya Kijiji kimetenga jumla ya ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha saruji.
Mkakati wa halmashauri ya uendelezaji wa fursa za uwekezaji;-
Halmashauri imeandaa mpango wa kujenga mazingira kwa makundi haya ya wakulima wadogo na wafugaji kuchangamkia fursa hizi badala ya kuelekeza jitihada kubwa katika uwekezaji kutoka nje.
Halmashauri inautaratibu wa kuwashirikisha wawekezaji kutoka nje wawekeze katika msingi wa ubia na wazalishaji wadogo, kwa maana kuwa wazalishaji wadogo - wakulima na wafugaji - katika vikundi vyao, msingi wao mkubwa ukiwa ni rasilimali ardhi, wanaweza kuingia katika ubia na wawekezaji toka nje kwa namna ambayo wanakuwa na sauti katika maamuzi na hivyo kuwezesha kile tukiitacho win win situation, yaani 'hali ya mafanikio kwa pande zote zinazohusika'.
Halmashauri inawezesha vikundi vya wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu ili kuwa na fursa za wazalishaji wadogo vijijini.
Halmashauri kwa kushirikiana na wawekezaji kuimarisha miundombinu ya barabara na mawasiliano ya simu katika maeneo ya Wilaya ya Same.
18.4 Mikakati ya kuwa na viwanda Wilayani
Kampuni ya DOTT Services (T) imeanza mazungumzo na Halmashauri kwa ajili ujenzi wa kiwanda cha kuparck maji na uvunjaji wa kokoto katika eneo la Saweni.
Uwekezaji wa kiwanda cha saruji katika Kata ya Makanya, ambapo mkakati wa kumpatia mwekezaji wa kampuni ya A to Z toka Arusha. Taratibu za kupata eneo katika Kata ya Makanya (Vikao vya awali vya kijiji cha Makanya vimekwisha fanyika)
Kilimo cha miwa; Uwekezaji wa kilimo cha miwa kampuni ya Kilimanjaro Biochem Limited inayomiliki kiwanda cha utengenezaji wa spiriti katika wilaya ya Mwanga kimeanza maandalizi ya kuwa na mikataba na wakulima ili waweze kulima miwa katika kata ya Ruvu. KBL inahitaji kulimiwa miwa kiasi cha ekari 2000 wameanza mazungumzo na wakulima wa maeneo ya kata ya Ruvu. Endapo wakulima wataridhia mikataba hiyo, kampuni hiyo imepanga kujenga kiwanda katika eneo la Ruvu Muungano cha kukamua miwa na kusafirisha ikiwa maji ya miwa (syrup). Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 200. (Ombi la KBL liliwasilishwa kwenye kamati ya Fedha, Utawala na Mipango).
CHANGAMOTO ZA KIWILAYA
MIKAKATI YA KIWILAYA
Kuhakikisha elimu ya uvunaji maji ya mvua, matumizi bora ya maji na hifadhi ya ardhi na udongo imetolewa kwa wakulima.
Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuzuia/kupunguza upotevu wa
mazao ya nafaka na mikunde wakati wa kuvuna na kuhifadhi
(Post harvest loss handling).
Kuhakikisha elimu ya ukadiriaji wa mahitaji ya mazao ya chakula kwa wakulima ngazi ya kaya imetolewa.
Kutoa elimu kwa wakulima juu ya hifadhi na matumizi bora ya mazao ya chakula kwa maeneo ambayo yamepata mavuno mazuri msimu wa vuli hasa maeneo ya kilimo cha umwagiliaji.
Kutoa ushauri kwa wakulima kutekeleza kilimo cha mazaoyanayostahimili ukame na yanayotumia kiasi kidogo cha unyevu hadi kukomaa kama mazao jamii ya mizizi na mikunde na Mtama.
Kuhakikisha uimarishaji wa matumizi bora ya maji katika miundombinu ya umwagiliaji iliyopo na kuhakikisha kunakuwepo na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula kwa misimu miwili na wakulima wanazingatia ushauri wa wataalam waliopo vijijini.
Kwa kuwatumia Maafisa Ugani waliopo kuhakikisha wakulima wanatumia teknolojia bora na sahihi za uzalishaji mazao ya chakula na biashara kwa ajili ya uhakika na usalama wa chakula ngazi ya kaya.
Kuhimiza wafugaji walio na mifugo kuuza wakati bado ikiwa na hali nzuri ya kiafya na kununua chakula na kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia.
Kuhimiza wakulima waliopo maeneo ya umwagiliaji kulima mazao yenye thamani na ubora kwa uhakika wa kuongeza kipato hatimaye kumudu kujinunulia chakula cha kutosha.
Kuhamasisha wafanyabiashara wenye uwezo kununua chakula Katika maeneo yenye chakula cha ziada na kuleta kuuza katika maeneo yenye upungufu kwa bei nafuu/elekezi.
Kampuni ya DOTT Services (T) imeanza mazungumzo na Halmashauri kwa ajili ujenzi wa kiwanda cha kuparck maji na uvunjaji wa kokoto katika eneo la Saweni.
Uwekezaji wa kiwanda cha saruji katika Kata ya Makanya, ambapo mkakati wa kumpatia mwekezaji wa kampuni ya A to Z toka Arusha. Taratibu za kupata eneo katika Kata ya Makanya (Vikao vya awali vya kijiji cha Makanya vimekwisha fanyika)
Kilimo cha miwa; Uwekezaji wa kilimo cha miwa kampuni ya Kilimanjaro Biochem Limited inayomiliki kiwanda cha utengenezaji wa spiriti katika wilaya ya Mwanga kimeanza maandalizi ya kuwa na mikataba na wakulima ili waweze kulima miwa katika kata ya Ruvu. KBL inahitaji kulimiwa miwa kiasi cha ekari 2000 wameanza mazungumzo na wakulima wa maeneo ya kata ya Ruvu. Endapo wakulima wataridhia mikataba hiyo, kampuni hiyo imepanga kujenga kiwanda katika eneo la Ruvu Muungano cha kukamua miwa na kusafirisha ikiwa maji ya miwa (syrup). Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 200. (Ombi la KBL liliwasilishwa kwenye kamati ya Fedha, Utawala na Mipango).
Kuongeza Ajira kwa Vijana
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.