Wananchi, Halmashauri ya Same wameungana na watu wote duniani, kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani,Wakizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Sokoni kata ya Hedaru halmashauri ya Same, wanaSame na vikundi mbalimbali vya kijamii wameweka wazi kuwa, kutokana na uwezeshaji kupitia mafunzo mbalimbali ya kiafya, kijamii na kiuchumi, wanayoyapata kupitia wataaalamu wa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii, wamepata motisha na kuwafanya watu wanaoishi na VVU, kujikubali na kujiamini kwa kuacha kujinyanyapaa wenyewe, kuimarika kiafya kwa kutumia ARV kwa ufasaha, kujiinua kiuchumi kupitia shughuli za ujasiriamali zinazofanywa kupitia vikundi.
Naye Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Edward Mpogolo, amewapongeza wananchi wa Same na vikundi mbalimbali vya kijamii na kuwatia moyo kuendelea kuishi kwa matumaini, huku wakijiamini mbele ya jamii na kufanya kazi zao za uzalishaji mali kwa bidii, kazi ambazo licha ya kuingiza kipato cha familia lakini pia ni msingi wa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
"Nimevutiwa sana na maonesho ya shughuli mbalimbalai za kupambana na UKIMWI kiseta, nendelee kuwatia moyo ndugu zangu, serikali yenu makini iko pamoja na ninyi, kwa kuwa mnazidi kuuthibitishia Umma, kwamba UKIMWI ni ugonjwa kama magonjwa mengine, ugonjwa ambao ukijikubali na ukizingatia masharti yanayolelekezwa na wahudumu wa afya, na ukatumia dawa kwa usahihi, unaweza kuishi maisha marefu na kutimiza ndoto zako, tofauti na dhana iliyojengeka hapo awali, kwamba ukipata maambukizi ya VVU wewe ni wa kufa tuu" amesisitiza Mhe.Mpogolo.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Same Bi.Anastazia Tutuba amesema halmashauri itaendela kushirikiana na ASAS za kiraia, kuviimarisha na kuvijengea uwezo vikundi hivyo vya kijamii, pamoja na kuhamasisha jamii, kupambana na maambukizi mapya ya VVU mpaka kufikia asilimia 95 ifikapo 2030, kuondoa unyanyapaa ndani ya jamii, pamoja na kuhakikisha watu wenye maambukizi wanapata dawa za kufubaza makali ya VVU kwa wakati na kwa usahihi, kupitia vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Same Benedict Missani amesema Lengo la maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, ni kitoa fursa ya kutathmini hali na kuhusu uthibiti UKIMWI ambayo husaidi katika kubaini changamoto, mafanikio na kuwa na mkakati katika kupambana na maambukizi ya VVU pamoja na UKIMWI katika jamii zetu.
"Maadhimisho haya yanafanyika ili kuikumbusha jamiii kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya mapya ya VVU na kuwakumbusha watu wenye maambukizi kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU kwa ufasaha bili kuacha, kubwa zaidi, jamii kuacha unyanyapaa kwa watu wenye amambukizi na kuwapa huduma stahiki kwa upendo."Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani halmashauri ya Same 2021, yamefanyika kwa ushirikiano wa halmashauri hiyo na Vikundi mbalimbali huku kauli mbiu ikisisistiza 'Zingatia Usawa, Tokomeza UKIMWI, Tokomeza magonjwa ya Mlipuko'.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.