Halmashauri ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro,imeandikisha wanafunzi 6,707 wa darasa la awali kwa mwaka 2024 ambapo kati yao Wavulana ni 3,492 na Wasichana ni 3,215 ambapo kati ya hao wenye mahitaji maalum ni 28 wakiwemo wasichana 14 na wavulana 14.
Afisa Elimu ya Awali na Msingi Wilayani Same, Bw. Marclaud Mero amesema idadi hiyo ni sawa na asilimi 83 ya matarajio ya uandikishaji ambayo yalikuwa 8,102.
Akizungumzia uandikishaji kwa darasa la kwanza Bw.Mero alisema Wilaya imefanikiwa kuandiisha wanafunzi 6,510 , sawa na asilimia 85 ya lengo la uandikishaji ambalo lilikuwa ni kuandikisha wanafunzi 7,638.
Alisema kati ya hao walioandikisha darasa lwa kwanza 20 ni wenye mahitaji maalum wakiwemo 9 wavulana na 11 wasichana.
“Taarifa hizi ni hadi kufikia tarehe 30 Machi 2024 ambapo ndio muda ambao tulifunga zoezi la uandikishaji kwa darasa la awali na darasa la kwanza “ alisema Bw. Mero.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.