Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linatarajia kuendesha Mradi shirikishi kwa wananchi wa Kijiji cha Saweni Wilayani Same ili kuwezesha wananchi hao kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali na mafisa kutokaShirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)walifika kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Saweni ili kufahamu mahitaji yao ambayo yatawezesha utekelezaji wa Mradi huo ambao unatarajiwa kutekelezwa kwa miaka mitano katika Kijiji hicho.
Akizungumza katika kikao hicho Mkazi wa Saweni Bw. Elikunda Mseli aliomba WFP kufanya utafiti wa mbegu zinazohimili ukame ili waweze kuwagaia.
“Tunaomba tafiti zifanyike ili kujua mazao yanastahamili ukame ili tuweze kugaiwa lakini pia tujengewe maghala ya kuhifadhi chakula” Alisema Mseli
Nae Bi Aziza Ally ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Saweni aliomba WFP kuwajengea mabwawa ya maji kwaajili ya umwagiliaji.
“Kila mwaka tunalima lakini hatuvuni maana tunategemea maji ya mvua na yakija yanapita tu,hivyo tunaomba tujengewe mabwawa ya kuvuna maji ya mvua” alisema Bi. Aziza.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Saweni Mratibu wa Miradi wa WFP nchini Tanzania Bw.Elisha Moyo alisema wamefika kijijini hapo kama hatua ya mwanzo ya kusikiliza mahitaji ya wananchi ili kuyachambua na kuanzagalia viapaumbele vya kuanzia.
Alisema Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)limeanza kufanya upembuzi yakinifu kwenye Kijiji cha hicho kwa lengo la kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye upatikanaji wa chakula.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Bi Anastazia Tutuba alilishukuru shirika la WFP kukichagua Kijiji cha Saweni katika kutekeleza Mradi huo na ameahidi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa malengo yanatimia. .
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.