Watoto wenye mahitaji maalum wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto cha Mother Kevina Hope Center na wanaosoma kitengo maalum shule ya Msingi Same wameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa kuwapatia vyandarua.
Halmashauri ya wilaya ya Same imegawa vyandarua 100 kwa watoto hao ili kuwalinda na maambukizi ya malaria ili waweze kushiriki vyama masomo yao wakiwa na afya njema.
Akitoa shukrani hizo, Rachel Mbwambo anayelelewa Kituo cha Mama Kevina alisema Halmashauri imefanya jambo jema kuwakumbuka katika mapambano dhidi ya malaria.
Zoezi hilo lilifanyika April 25 siku ambayo hutumika kuadhimisha siku ya Malaria Duniani ambapo serikali imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali zenye lengo la kudhibiti maambukizi ya malaria.
Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Dkt. Cainan Kiswaga aliwata watoto hao kuhakikisha kuwa wanasafisha maeneo yanayowazunguka ili kuondoa mazalia ya mbu.
“Hakikisheni kwamba nyasi zilizozunguka katika maeneo yenu zinafyekwa na msiruhusu maji kutuama kwani mazingira hayo yanaongeza mazalia ya mbu” alielekeza Dkt. Cainan
Akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya Malaria kwenye Wilaya ya Same, Mratibu wa udhibiti wa Malaria Wilaya ya Same Bi.Anusiata Mgumba alisema maambukizi yamepungua kutoka asilimia 1.5 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 0.8 mwaka 2023.
“Tunaendelea na jitihada za kupunguza maambukizi ili kufikia lengo la kitaifa la zero Malaria ifikapo 2030” alisema Anusiata.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.