Waziri wa Maliasili ya Utalii Balozi, Dk. Pindi Chana, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Tamasha la “Same Utalii Festival Season2, litakalofanyika Desemba 21 mwaka huu katika viwanja vya Standi Kuu ya Same Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mheshimiwa Kasilda amesema, baada ya Uzinduzi Waziri Chana ataongozana na watalii kuelekea hifadhi ya Mkomazi.
Alisema Same Utalii Festival Season2 itajumuisha kutembelea vivutio vya utalii vingine ikiwemo mlima kidenge, lengo likiwa ni kuibua vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Wilaya hiyo.
Mheshimiwa Kasilda amesema mtalii anapo ukwea mlima Kidenge, anaweza kuona mawio na machweo ya jua vizuri anapokuwa juu ya kilele hicho, hayo.
Watalii watapata nafasi ya kutembelea Hifadhi Asilia ya Chome (Mlima Shengena) ambapo watajionea uoto mzuri wa asili na kujionea vyura ambao hawapatikani maeneo mengine.
Vile vile amesema usiku wa Desemba 22, kutakuwa na tamasha la wanamziki mbalimbali akiwemo mwanamuziki wa Singeli Jay Combat, Msanii wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan maarufu (Tunda Man) pamoja na wasanii wengine wa ndani kutoka wilaya ya Same, ambapo pia kutakuwa na nyama choma Festival.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.