Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi Wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru ambao Kitaifa utafanyika April 2,2024 Moshi,Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu amesema Uzinduzi Wa Mbio za Mwenge utafanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
"Kwa mara ya Kwanza wakati nchi yetu inapata Uhuru mwaka 1961 Mwenge ulipandishwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro,hivyo mwaka huu tunasema Mwenge umerudi nyumbani"alisema Mheshimiwa Babu.
Amesema baada ya Uzinduzi Mwenge Wa Uhuru utakimbizwa kwenye Wilaya Sita zenye halmashauri Saba kwenye Mkoa wa Kilimanjaro.
Kaulimbiu ya Mwenge Wa Uhuru mwaka Huu inasema "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.