Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amezindua zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura Julai 20,2024 mkoani Kigoma ambapo amewataka wananchi wote wenye sifa za kushiriki uchaguzi wajitokeze kuboresha taarifa zao ili wawe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi zinazotarajiwa kufanyika hapa nchini.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura umeanza rasmi Julai 20,2024 kwenye mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora ambapo zoezi hilo litafanyika kwa siku saba kabla ya kuendelea kwenye mikoa mingine.
Akizungumzia maandalizi ya zoezi hilo kwenye Wilaya ya Same,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya WIlaya Bw. Jimson Mhagama alisema ili kufanikisha zoezi hilo Wilaya imeshaandaa vituo 263 ambavyo vitatumika kwaajili ya zoezi la uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
“Vituo hivi vipo kwenye Kata zetu 34 ambazo zina vijiji 100,ni maeneo ambayo yanafikika kwa kila mwananchi,hivyo niwahimize wananchi kuhakikisha kuwa wanafika kwenye vituo zoezi litakapoanza ili kuboresha taarifa zao” alisema Mhagama
Alisema kuwa kupiga kura ni haki ya msingi kabisa ya kidemokrasia kwa kila raia mwenye sifa ya kupiga kura hivyo ni vyema wananchi wakajitokeza kuhakikisha kuwa wanahakiki taarifa zao ili wawe na sifa ya kupiga kura.
Aidha amehimiza wananchi wenye sifa wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za Mtaa na Vijiji ili kuendelea kuimarisha demokrasia hapa nchini.
Nafasi zinazotarajiwa kugombewa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji ,wenyeviti wa vitongoji na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na kwa upande wa Mitaa watakakaochaguliwa ni mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe wa Mtaa.
Wananchi wenye umri kuanzia miaka 18 wanatakiwa kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la kudumu la Wapiga Kura wakati wa zoezi hilo ambapo wananchi wenye umri kuanzia miaka 21 na kuendelea wanaweza kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.