Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea na kujionea Maendeleo ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA kinachojengwa kwenye Kata ya Makanya Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro..
Waziri Mkuu ameonyesha kuridhishwa na ujenzi huo ambao upo kwenye hatua ya umaliziaji awamu ya kwanza
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu pia alitembelea na kukagua Ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani -Mkonazi yenye urefu wa kilomita 37 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami.
Dkt. Nchemba amewakumbusha watumishi wote wa umma nchini Tanzania kuhakikisha wanawajibika ipasavyo katika kusimamia miradi na kuwatumikia wananchi.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu alipata fursa ya kuzungumza na wananchi kwenye viwanja vya Ndugu na Makanya ambapo aliwasikiliza na kutatua kero mbambali.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.