Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mhe:Angellah Kairuki amekutana na Madiwani wa Same Mashariki Jan 11,2023 na kufanya nao mazungumzo mjini Dodoma.
Madiwani hao wakiwa wameongozwa na Mbunge wa Same Mashariki,Mhe:Anne Kilango Malecela walipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha huduma za Jamii Wilayani Same.
Baada ya kikao hicho Madiwani hao wamemshukuru Mhe:Kairuki kwa kutenga muda wa kuzungumzia nao lakini pia wamemshukuru Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Same fedha za Miradi ya Maendeleo katika sekta za Afya,Maji , Elimu na ukarabati wa miundombinu ya Barabara.
https://www.instagram.com/p/CnRqDqUNJk3/?igshid=MDJmNzVkMjY=
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.