Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Angellah Kairuki ameahidi kumsomesha kidato cha tano na cha sita Mwanafunzi Naomi Noah mwenye ulemavu wa miguu ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka huu 2023
Waziri Kairuki ametoa ahadi hiyo kwenye mahafali ya 17 ya kidato cha nne kwenye shule ya Sekondari Kibacha ambapo alikuwa Mgeni Rasmi.
"Naahidi kumsomesha binti huyu kidato cha tano na cha sita,lakini pia niwaombe wazazi wote wenye watoto walemavu wasiwafiche wawapeleke shule" alisema Mheshimiwa Kairuki.
Alisema wazazi wanaowakosesha elimu watoto wenye ulemavu ni kuwanyima haki yao ya msingi maana wanapopatiwa elimu wanaongeza uwezo wa kujitegemea.
Akizungumzia ahadi hiyo mwanafunzi Naomi Noah alimshukuru Waziri Kairuki na kuahidi kufanya vizuri kwenye mitihani yake.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.