Waziri wa Maliasili na Utaliii Mhe. Angellah Kairuki ameahidi kuchimba kisima cha maji katika shule ya Sekondari Kibacha iliyopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika shule hiyo.
Ahadi hiyo ya Mheshimiwa Kairuki aliitoa katika mahafali ya 17 ya kidato cha nne shuleni hapo kufuatia ombi la Wanafunzi wa shule hiyo wakati wakifanya igizo ambapo walieleza kukabiliana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji.
Mheshimiwa Kairuki ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika mahafali hayo alisema kisima cha maji atakachochimba pia itakua fursa ya kilimo cha mbogamboga ili kuimarisha lishe kwa wanafunzi shuleni hapo.
Mheshimiwa Kairuki alisema Serikali imefanya kazi nyingi katika uboreshaji wa elimu ikiwemo utekelezaji wa Miradi lipa kulingana na matokeo (EP4R) ambao kwa mwaka wa fedha 2022/23 umetoa Bil.7.5 kwaajili ya maendeleo ya shule mbalimbali za sekondari hapa nchini.
"Serikali yetu kupitia mradi wa EP4R umetoa fedha zaidi ya Bil.7.5 kwaajili ya ujenzi wa mabweni, matundu ya vyoo,vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali za kidato cha tano na sita na same pia imeweza kunufaika" amesema Mhe.Kairuki.
Huku Mradi wa SEQUIP umetoa shilingi billioni 48 kwaajili ya kujenga shule za wasichana za bweni ambapo wilayani Same ni miongoni mwa wilaya zilizo nufaika na mradi huo.
"Nipende kuwapongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa usimamizi mzuri wa Miradi,nimeona katika Shule Mpya ya Msingi Kisima ni shule nzuri imejengwa vizuri sana na Shule ya Chekechea ya mfano liyopo pale pia imejengwa vizuri,natamani Wilaya nyingine waje wajifunze hapa kwenu "alisema Kairuki.
Pia aliwaasa wahitimu hao wapatao 165 kutumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii kuongeza utiifu na nidhamu kuelekea mitihani ya Taifa.
Nae mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni ameishukuru serikali kwa kuikumbuka Wilaya ya Same na kutoa fedha za miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara pamoja na mradi wa maji wa Mwanga- Same- Korogwe ambao Mhe. Kasilda Mgeni amesema kufikia Juni 2024 mradi huo utakua umekamilika na kuwatua ndoo kichwani wakazi wa Same
Nae Mkurugenzi wa Wilaya ya Same Bi. Anastazia Tutuba alitoa salamu za shukrani kwa mhe.Angellah Kairuki kwa kusaidia fedha kwaajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo wakati alipokuwa Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI.
"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri maana kipindi ukiwa Waziri wa TAMISEMI Wilaya yetu kwa mwaka jana iliweza kupokea Bil.15 kwaajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa hospitali mpya ya Wilaya"alisema Tutuba.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.