Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewataka wawekezaji wa Madini ya Gypsum (Jasi) Makanya kuanzisha ushirika wao ambao utawasaidia kuweza kuwa na usimamizi mzuri ili uwekezaji wao uweze kuwa na tija kwao kwa wananchi na kwa Serikali.
Ameyasema hayo kwenye kikao na wawekezaji hao kilichofanyika Kata ya Makanya chenye lengo la kutafuta suluhu ya changamoto wanazokabiliana nazo wadau wa Jasi ambapo wakiwa na ushirika itakuwa rahisi kuzijadili na kuzipatia ufumbuzi.
"Ushirika umekua ukionesha mafanikio sehemu mbalimbali hivyo nanyi hakikisheni mnaunda ushirika wenu" alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha amewataka wawekezaji hao kuzingatia sheria ya utunzaji wa Mazingira baada ya kuchimba Madini ikiwemo kufukia mashimo na kupanda miti kwenye maeneo hayo ili kudhibiti athari za uharibufu wa mazingira.
Pia amesisitiza wawekezaji hao kuzingatia ulipaji wa kodi na ushuri mbalimbali wa Serikali kwa kama zinavyostahili.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.