Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Angellah Kairuki wakati akizindua Tamasha kubwa la Utalii Wilayani Same(Same Utalii Festival) Feb 23,2024.
Akizindua Tamasha hilo la siku tatu linalojulikana kama Same Utalii Festival Waziri Kairuki alisema ongezeko hilo la watalii limechangiwa na jitihada za Mhe.Rais Samia Suluhu kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour.
"Tutakua wachoyo wa fadhila iwapo hatutamshukuru Mheshimiwa Rais kusaidia ongezeko la watalii kupitia filamu ya Royal Tour"alisema Mhe.Kairuki.
Mheshimiwa Waziri amewataka pia wananchi wa Tanzania kushiriki kufanya Utalii katika maeneo mbalimbali ya utalii hapa nchini ili kuendelea kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini.
"Tusisubiri wazungu tu kuja kutembelea vivutio vyetu vya Utalii,tuanze sisi ili wazungu wafuate"alisema Mheshimiwa Waziri.
Aidha Waziri Kairuki alitoa wito kwa kampuni za Utalii na hoteli zinazopokea watalii kutoa huduma bora ili watalii hao waweze kuvutiwa na kutembelea tena Tanzania.
Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa nchi imetembelewa na watalii milioni tano ifikapo 2025.
Akizungumza katika Uzinduzi huo,Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Kasilda Mgeni alisema lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Wilayani Same ili kukuza uchumi wa wananchi na kuongeza pato la Serikali.
"Tamasha hili la Same Utalii Festival litakuwa linafanyika kila mwaka,tunaamini itasaidia sana kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika Wilaya hii"alisema Mheshimiwa Kasilda.
Katika Tamasha hilo wageni walifanikiwa kutembelea Hifadhi ya Taifa Mkomazi,Mlima Kidenge na Hifadhi ya Msitu wa asili Chome.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.