Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Same Mashariki na Same Magharibi Bw.Jimson Mhagama amewataka wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kuzingatia Kanuni na miongozo yote ya Uchaguzi wakati wa zoezi la kupiga kura Novemba 27 ,2024.
Amesema miongozo hiyo ni pamoja na kuhakikisha kuwa vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa 2 kamili asubuhi na kufungwa saa 10 kamili jioni siku ya Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Bw.Mhahama ameongeza kuwa wapiga kura wenye ulemavu, wakina mama wajawazito, wagonjwa na wazee wapewe kipaumbele katika zoezi la kupiga kura.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Same amewasisitiza wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kuzingatia sheria, taratibu ili kufikia malengo na makusudio ya Serikali katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
Jumla ya wapiga kura 182,618 wa Jimbo la Same Mashariki na Same Magharibi wanatarajia kupiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
Wilaya ya Same ina Jumla ya Vijiji 100 na Vitongoji 503 ambavyo vitachagua kiongozi Novemba 27 mwaka huu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.