Wilaya ya Same inakabiliwa na tatizo la uvamizi wa wanyamapori hatari na waharibifu hususani tembo na kiboko.Wanyamapori hawa wanavamia makazi ya wananchi na kuhatarisha usalama wa wananchi na mali zao.Maeneo mengi yameathiriwa ambapomazao mengi mashambani yameharibiwa kwa kuliwa na kukanyagwa vibaya na wananchi kujeruhiwa na wengine kuuawa.
Kata zilizoathirika zaidi na uvamizi wa tembo ni Njoro,Same,Kisima,Ruvu,Vumari,Kisiwani,Maore,Kalemawe na Mwembe.
Halmashauri ya Wilaya ya Same kupitia sekta ya wanyamapori imejitahidi kudhibiti wanyamapori hao wasilete madhara kwa wananchi.Pia wamekuwa wakishirikiana na wadau wa uhifadhi wa wanyamapori kama vile Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa(TANAPA),Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori(TAWA) na mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile WWF,TNRF na AWF.
Elimu ya namna ya kukabiliana nawanyamapori hao inatolewa na itazidi kutolewa katika maeneo yanayopata athari kwa kufundisha mbinu mbalimbali kama vile kupiga madebe au mabati,matofali ya pilipili,fensi ya vitambaa vyenye oil chafu,kumulika na tochi na kupiga honi(vuvuzela).
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.