Wananchi wa Wilaya ya Same wametakiwa kujitokeza kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na ushauri nasaha kwaajili ya kupima afya zao na kupata ushauri juu ya kujiepusha na ugonjwa hatari wa UKIMWI.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni wakati akizungumza na wananchi wa Same kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo hufanyika Desemba Mosi ya kila mwaka.
Lengo la maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ni kuwakumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa UKIMWI lakini kukumbushana njia sahihi za kuzingatia ili kuepuka maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Shughuli za maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani pia huenda sambamba na kukumbushana umuhimu wa kutumia dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (ARV’s) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.
Akizungumza na Wananchi kwenye uwanja wa kwasakwasa mjini Same Mkuu wa Wilaya aliwahimiza wananchi kwenda kupima afya zao ili kujua hali zao na waweze kuchukua hatua stahili kulingana na majibu watakayoyapata.
“Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha huduma za afya ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa dawa za ARV’s kwa watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI.
Katika Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Mkuu wa Wilaya ya Same pia alizindua Kampeni ya Mwezi wa Afya na Lishe kwa roundi ya Desemba itakayofanyika kuanzia tarehe 1-30 Desemba katika vituo vyote vya huduma za Afya Wilayani Same.
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yalikwenda sambamba na shughuli mbali mbali za lishe ikiwemo upimaji wa hali ya Lishe(Uzito, Urefu (BMI), MUAC kwa watoto chini ya miaka mitano, utoaji wa matone ya Vitamin A na dawa za minyoo kwa watoto wa chini ya miaka mitano.
Shunguli nyingine zilizofanyika ni maonyesho ya mapishi bora na utengenezajji wa juice na mapishi ya mbogamboga na matumizi ya viungo va vikolezo(Herbs and spices) ambavyo ni muhimu kiafya.
Siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka huu imebebwa na kaulimbiu isemayo Chagua njia sahihi,Tokomeza UKIMWI
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.