Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka ngumu Wilaya ya Same kimewataka wananchi Wilayani humo kuchangia kwa hiari ada ya uzoaji taka ili kukiwezesha kitengo hicho kuwahudumia vizuri.
Akitoa taarifa ya Utekelezaji kazi kwenye kitengo hicho Kaimu Mkuu wa Kitengo hicho Bi. Yuster Malisa alisema wapo baadhi ya wananchi ambao hawalipi ada ya uzoaji taka kwa wakati.
“Tunaendelea kuwahimiza wananchi kulipa ada ya uzoaji taka kwa wakati na iwapo watashindwa kufanya hivyo sharia itachukua mkondo wake” alisema Bi.Yuster.
Alisema kuwa kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka kitengo hicho kilifanikiwa kukagua kaya zaidi ya 15,000 ikiwa ni pamoja na sehemu za biashara.
Aidha alisema kuwa walifanikiwa kupima ubora wa maji na kugawa vidonge maalum vya kutibu maji ili kuhakikisha kwamba wananchi wanakunywa maji safi na salama.
“Katika robo ya nne sampuli 63 za maji kwenye kaya zilipimwa kwa lengo la kukinga na magonjwa ya mlipuko asilimia 98 ya maji yalionekana kuwa ni safi” alisema
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.