Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama amewashauri wananchi kuhakikisha kuwa wanakula mlo kamili ili kulilinda afya zao dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Akitoa ushauri huo wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe yaliyofanyika kwenye Kata ya Ruvu Wilayani hapa.
Mkurugenzi huyo alisema Kuna haja kubwa kwa wananchi kuzingatia ushauri wa wataalam wa lishe kwenye ulaji ili kuwa na afya bora,hasa kwa kinamama wajawazito na watoto.
"Wataalam wanatwambia tukila mlo kamili miili yetu inajenga kinga Imara hivyo inakuwa sio rahisi kushambuliwa na maradhi"alisema Bw.Mhagama.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake wa Hospitali ya Wilaya Same Dkt.Steven Temanyika alisisitiza kula mlo kamili kwa kinamama wajawazito na watoto.
Alisema wajawazito wanapokosa mlo kamili afya yao na ya mtoto aliye tumboni huathirika kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kuishiwa damu.
"Kwenye nchi zilizoendelea tatizo la upungufu wa damu kwa wajawazito ni asilimia 10 hadi 20 wakati kwenye nchi zatu zinazoendelea ni asilimia 40 hadi 80"alisema Dkt.Temanyika
Akitoa elimu ya lishe kwa wananchi Afisa Lishe wa Wilaya ya Same Bi.Jackline Kilenga alisema ni vyema kila mtu ahakikishe kuwa kwenye mlo wake kuna wanga,vitamin na protini.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.