Baada ya kukosa maji kwa zaidi ya miaka 20, hatimaye wakazi zaidi ya 300 wa Kitongoji cha Makei, Kijiji cha Bangalala Kata ya Bangalala Wilayani Same wameondokana na changamoto ya ukosefu wa maji baada ya Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kukabidhi mradi wa maji.
Akizundua Miradi huo Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amewataka wananchi hao kuhakikisha wanaendelea kuhifadhi mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti pembezoni mwa mradi huo ili kuhakikisha uoto wa asili haupotei.
"Mna wajibu mkubwa wa kulinda miundombinu ya Mradi huu, kila mmoja wenu awe mlinzi wa miundombinu hii ya maji kwa sababu kila mtu hapa anauhitaji wa maji, pia tuhakikishe tunalipa bili za maji kwa wakati ili pale miundombinu inapoharibika zile fedha za bili zitengeneze ili huduma iwe endelevu” Amesema Mhe. Kasilda.
Mhe. Kasilda Mgeni amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza sera ya “Kumtua Mama Ndoo Kichwani” ambayo imelenga kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma ya maji kwa karibu.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Same Mbayani Said amesema kuwa mradi wa maji Makei umegharimu milioni 63 za kitanzania na unahudumia kaya 90 zenye wakazi zaidi ya 360 wa Kitongoji cha Makei.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bangalala Kassim Mnyone amesema atashirikiana na wananchi wa Makei kuhakikisha kuwa miundombinu ya Mradi huo inatunzwa na kuwa wndelevu.
Nae Mwenyekiti wa Kijiji cha Bangalala Bw.Shaaban Kiambe amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dky.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha Utekelezaji wa Mradi huo kwani wananchi wa Kitongoji hicho walipata changamoto ya maji kwa muda mrefu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.