Wakazi wa Kata ya Hedaru, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mto Washi.
Ujenzi wa daraja hilo umemaliza changamoto sugu ya mafuriko yaliyokuwa yakisababisha vifo vya watu, uharibifu wa mali, mazao na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.
Wananchi hao wametoa shukrani zao kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni alipotembelea na kukagua ujenzi wa daraja hilo.
Mhe. Kasilda alieleza kuridhishwa na kazi iliyofanywa na TANROADS, huku akimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Ujenzi kwa dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha miundombinu ya barabara na kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili wananchi.
“Mradi huu umetumia fedha nyingi za Serikali zaidi ya shilingi bilioni 1.5 hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuutunza na kuilinda kwa wivu mkubwa.
Bw.Rajab Msheri Mkazi wa Hedaru anasema daraja hilo ni mkombozi mkubwa kwao kwani limeondoa hatari ya mafuriko yaliyokuwa yakisababisha vifo, uharibifu wa mali na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mhandisi Mkazi wa mradi huo, Mhandisi Benitho Mnzovela, amesema mradi umekamilika kwa asilimia 100.
Katibu wa CCM Uenezi Wilaya ya Same Ndg. Mohamed Ifanda, ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa daraja hilo pamoja na uongozi wa wilaya kwa usimamizi madhubuti wa mradi.
VIJANA WANUFAIKA NA PIKIPIKI ZA MKOPO USIO NA RIBA.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.