Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuipatia Wilaya hiyo gari la zimamoto.
Mheshimiwa Kasilda ametoa shukrani hizo wakati akikabidhiwa gari hilo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu ambapo alisema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuimarisha usalama wa wananchi.
Akikabidhi gari hilo Mkuu wa amkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Babu amewataka Viongozi wa Wilaya ya Same kuhakikisha kuwa gari hilo linatunzwa ili liweze kukabiliana na majanga ya moto kwa muda mrefu.
Kwa mwaka huu pekee Wilaya ya Same ilishuhudia ajali mbaya kabisa ya Moto baada ya magari mawili ya abiria kugongana na kuweka Moto ajali ambayo ilipoteza maisha ya watu zaidi ya 40 na ajali nyingine za Moto zilizotokea ni kuungua kwa mabweni ya Wanafunzi kwenye Shule za Sekondari Bemko na Makanya.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.