Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Same Bw.Charles Anatoly ametoa Elimu kwa Vijana wa Kata ya Maore juu ya taratibu za kufuata ili kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.
Mikopo hiyo ambayo hutolewa kwa Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu inatokana na asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri na haina riba.
Amesema hatua muhimu za kufuata ili kupata mikopo ni kama ifuatavyo:-
Kuanziasha kikundi cha watu wasiopungua watano (wanaoaminiana).
Kutengeneza Katiba ya Kikundi.
Kusajili Kikundi wenye tovuti ya Wezesha Portal.
Kufungua Akaunti Benki.
Amesema baada ya kufuata hatua hizo Kikundi kitathibitishwa na baada ya kuthibitishwa wataweza kuomba Mkopo.
Afisa Maendeleo huyo alisema Mafunzo hayo ni sehemu ya Mafunzo ambayo hutolewa mara kwa mara kwa wananchi ili kuwawezesha kunufaika na Mkopo huo.
Sambamba na elimu ya mikopo pia vijana hao walielezwa kuhusu umuhimu wa kuilinda amani na kujiepusha na vitendo vya kihalifu.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.