Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba amewataka wakuu wa Shule kushirikiana na viongozi wa Kata na vijiji Wilayani humo kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata mlo wa mchana shuleni.
Mkurugenzi Tutuba ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha walimu wa Shule za Sekondari Wilayani humo ambapo alisema suala la lishe kwa watoto lazima lizingatiwe.
"Suala la lishe bora na watoto kupata mlo wa mchana shuleni ni agenda ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hivyo lazima litekelezwe ili tuwe Na watoto wenye Afya bora"alisemq Mkurugenzi
Alisema watoto wanapopata mlo kamili hata viwango vyao vya uelewa huongozeka hivyo hata ufaulu unaweza kuongezeka.
Akizungumza katika kikao hicho ambacho kinalenga kuweka mikakati ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Same Bi.Neema Lemunge alisema kwasasa Zaidi ya asilimia 86 ya wanafunzi wanapata mlo wa mchana shuleni.
Alisema wapo wazazi wachache ambao bado ni wasumbufu katika kuchangia chakula kwaajili ya watoto wao shuleni lakini Sheria itatumika kuwabana ili waweze kuchangia.
Wilaya ya Same tayari imepitisha Sheria ndogo ya kuhakikisha kuwa wazazi wanawezesha chakula kwaajili ya watoto wao shuleni.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.