Jumla ya wanafunzi 6151 wanatarajia kufanya mitihani ya kuhitimu darasa la Saba Wilayani Same ambapo kati yao wanafunzi 3012 ni wavulana na wasichana ni 3139, takwimu hizo zinajumuisha wanafunzi wenye uoni hafifu ambao ni 5 kati yao wavulana ni 4 na Msichana ni 1.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama amesema Halmashauri imeshafanya maandalizi yote muhimu kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanafanya Mitihani yao Jumatano Septemba 11 na 12, 2024 kama ilivyo kwenye ratiba ya Serikali.
Halmashauri ya Wilaya ya Same ina jumla ya Shule za Msingi 206 ambapo shule 188 ni za Serikali na 18 ni za binafsi, ambapo shule zenye watahiniwa wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ni 196 .
Akizungumzia maandalizi ya Mitihani hiyo Afisa Elimu Awali na Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw. Marclaud Mero alisema shule hizo 186 ni za Mfumo wa Kiswahili na 10 ni za Mfumo wa Kiingereza (English Medium Schools) zinazomilikiwa na Taasisi Binafsi.
Bw.Mero alisema wanafunzi wanaofanya mtihani wa Taifa mwaka huu waliandikishwa darasa la kwanza mwaka 2018 wakiwa wanafunzi 6243 ambapo kati yao wavulana walikuwa 3066 na wasichana ni 3177.
“Idadi ya wanaomaliza imepungua kidogo kutokana na baadhi ya wanafunzi kuhama Wilaya” alisema
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.