Wizara ya Maliasili na Utalii umetoa kifuta jasho cha Shilingi milioni 217 kwa wahenga wa madhara yatokanayo na wanyama waharibifu kwenye Wilaya ya Same,mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia kifuta jasho hichoMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Bw.Jimson Mhagama alisema kifuta jasho hicho kimetolewa kwa wahanga 1,515.
"Tunashukuru sana Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kulipa kifuta jasho kwa wahanga katika Wilaya yetu kwani imesaidia kupunguza malalamiko"alisema Bw.Mhagama.
Kwa upande wake Afisa Wanyamapori Wilaya ya Same, Bw. Thomas Katunzi alisema kifuta jasho kimetolewa kwa familia za watu 06 waliopoteza maisha baada ya kuuliwa na wanyama.
Alisema wahanga wengine waliolipwa ni wahanga wawili waliopata majeruhi baada ya kuathiriwa na wanyama.
"Wengine waliolipwa ni wafugaji ambao mifugo yao 13 iliuawa na wanyama wakali ambapo pia wakulima walilipwa fidia kutokana na mazao yao ekari 2,396"alifafanua Bw.Katunzi
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.