Ni uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano ambapo mpango huo ulizinduliwa na Ndg Sospeter Magonera ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya akiwa amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Same.Ndg Sospeter Magonera alisema uzinduzi wa mpango huo unaenda kuleta mabadiliko makubwa katika usajili na utambuzi wa watoto wa Halmashauri yetu.
Ndg Magonera alisema ni haki ya mtoto kutambuliwa na kupewa uthibitisho na kwamba cheti cha kuzaliwa kina matumizi mengi ambapo hutumika katika kuandikisha watoto wanaoanza elimu ya sekondari,kupata nafasi za elimu ya juu na kupata mikopo,kupata kadi ya kura,kitambulisho cha taifa na hutumika kubainisha mahusiano kati ya wanafamilia.
Vilevile Ndg Magonera alisisitiza kuwa usajili wa vizazi ni huduma muhimu sana kwa wananchi na Serikali ambayo hupata takwimu sahihi za idadi ya watu kwa ajili ya mipango ya maendeleo na kuepuka matumizi ya takwimu za makisio.
Hapo chini ni baadhi ya wazazi wababa na wamama waliotunukiwa vyeti vya kuzaliwa vya watoto na mgeni rasmi
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kukubali mwaliko na kushiriki katika uzinduzi huo ambapo anasema mpango huo umebuniwa na Serikali kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA),ambapo mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano utaleta maboresho ya watoto wote wa umri chini ya miaka mitano watapata vyeti bure vilevile huduma zinasogezwa na kupatikana karibu na maeneo ya wananchi.
"Kila mtoto wa Halmashauri ya Same anastahili cheti cha kuzaliwa,tumpe haki yake"
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.