Ni chuo kikuu kinachojengwa kwa kushirikiana kati ya Chuo kikuu cha Califonia kilichopo Marekani na taasisi ya Mbesese iliyopo wilaya ya Same.
Wanafunzi 13 toka Califonia pamoja na walimu wao 5wakaa wiki mbili Same wakishuhudia mwanzo wa ujenzi huo.
Wasema waungana na mpango wa Wilaya wa kutumia eneo la tambarare kuwa taasisi za elimu na viwanda baada ya kuonekana ni kame kwa kilimo.
Wakiri kuifanya Same eneo lao la pili kwa makazi baada ya Califonia(Same to be there second home)
Washiriki kazi za mikono-kuchanganya zege baada ya mixer kuharibika.
Wananchi wanaozunguka eneo hilo wapokea mradi kwa furaha,waomba kupewa ajira.Mradi wachangia ujenzi wa choo shule ya Mighareni sekondari.
Wanafunzi wa chuo cha Calfonia wamkabidhi DC Same mchoro wa mapendekezo ya Round About ya Same.Warejea maneno ya DC Mhe.Rosemary Senyamule ya 2017 kutaka mchoro wa round about nzuri Tanzania.DC Same Mhe.Rosemary Senyamule afurahia ubunifu huo.Aahidi kushirikisha wadau kuona namna ya kutumia ubunifu huo mzuri.
DC awakumbusha kufuata taratibu zinazotakiwa.Awakaribisha kutembelea na kutangaza utalii wa Same na maeneo mengine ya Tanzania."Kwa kuwa mmekuwa wa kwanza kuanza ujenzi wa chuo kikuu Same,hakikisheni mnakuwa pia wa kwanza kupokea wanafunzi,kwani sisi bado tunatangaza uwepo wa maeneo ya vyuo,asije mwingine akajenga na kuanza kabla yenu mkapoteza sifa ya kuwa wa kwanza"Alisema DC hiyo.
Akiwashukuru Afisa tarafa Bi.Eva Laurian aliahidi kuwapa ushirikiano ili kukamilisha dhamira yao njema.
Hakika neno linasema"Na mataifa watawatumikia"Chuo kitaitwa Same Polytechnical University.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.