Wilaya ya Same yapeleka ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa lita 30 kwa mkamuo mmoja kwenye maonesho ya nane nane yanayofanyika kwenye viwanja vya Themi, Njiro mkoani Arusha.
Mshauri wa Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw. Zawadi Msambaa alisema Wilaya imeamua kuwapeleka ng’ombe hao kwenye maonesho ili wafugaji wengine waweze kujifunza ufugaji ulio bora.
“Umefika wakati kwa wafugaji kuachana na ufugaji wa kizamani wafuge ufugaji wa kisasa ambao unaweza kuleta tija kwenye maisha yao,ufugaji wa kibiashara” alisema
Bw.Zawadi alisema Wilaya imekuja na teknolojia nyingi kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji kufuga kisasa ambapo wafugaji wanapatiwa huduma ya uhamilishaji wa ng’ombe wa maziwa kupitia program ya mbegu za ruzuku kutoka Serikali kuu.
“Ufugaji wa kisasa unapunguza migogoro ya ardhi kwani mfugaji ana uwezo wa kufuga mifugo michache na ikamuwezesha kujimudu kimaisha” alisema
Mfugaji wa Ng’ombe hao kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Lameck Mbise alisema ng’ombe anaowafuga wote wana uwezo wa kuzalisha maziwa lita 25 hadi 30 kwa mkamuo mmoja” alisema
Bw.Lameck ameishukuru Serikali kwa kufanyia mifugo yake uhamilishaji hivyo kuweza kuzalisha ng’ombe walio bora ambao wanamsaidia kukidhi mahitaji ya familia.
“Ng’ombe wana wana faida kubwa kama kupata maziwa, mbolea na ngozi” alisema na kuongeza kuwa ufugsji wa ng’ombe umemsaidia kuongeza pato la familia na kuweza kuhudumia vyema familia.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.