Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Rais wa kwanza wa Tanzania zamani ikijulikana kama Tanganyika, alizaliwa Mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Baba wa Taifa alifariki Dunia Oktoba 14 mwaka 1999 akipatiwa matibabu Jijini London Uingereza.
Ifikapo Oktoba 14 ya kila mwaka Tanzania huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania.
Watanzania tunamkumbuka Baba wa Taifa kwa mambo mengi ikiwemo kuipatia Uhuru nchi ya Tanzania tena bila kumwaga damu mwaka 1961.
Baba wa Taifa ndiye aliyeasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 kwa kushirikiana na aliyekuwa Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume.
Baba wa Taifa alijenga umoja imara wa Kitaifa kupitia uanzishwaji wa Vijiji vya Ujamaa na kuimarisha lugha ya Kiswahili.
Kitaifa Maadhimisho hayo huambatana na sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo kwa mwaka 2024 yanafanyika jijini Mwanza.
Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro inaadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa kwa kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali ili kutunza mazingira.
Endelea kupumzika kwa amani Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.