Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amewataka wananchi wa Wilaya ya Same kutunza na kulinda miradi mbalimbali inayowekezwa na Serikali kwenye maeneo yao ili iweze kudumu na kunufaisha kizazi cha sasa na kijacho.e
Amesema Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga na kuboresha Miradi Msingi hivyo ni vyema wananchi wakahakikisha wanailinda.
Ametoa wito huo akizungumza na wakazi wa Kata ya Suji wilayani Same, mara baada ya ziara ya kukagua na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi miwili ambayo ni mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Suji pamoja na Zahanati ya Malindi – Suji ambapo amesema uwekezaji huo umesogeza huduma karibu na wananchi.
Zahanati ya Malindi-Suji kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya wilaya ya Same pamoja na Ubalozi wa Japani kwa gharama ya Shilingi milioni 470.
Waziri wa Afya ameridhia maombi ya wakazi wa Suji kuipandisha hadhi Zahanati hiyo iwe kituo cha Afya ili huduma zote muhimu ziweze kutolewa lengo ikiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma na kupunguza vifo vya mama na mtoto.
* Tunalo jukumu la kupunguza vifo vya akina mama wanaojifungua na watoto,hivyo tutaleta fedha hapa milioni 600 ili kupandisha hadhi Zahanati hii kwa mwaka wa fedha 2024/25"Amesema Waziri Mhagama.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni alisema kuwa miradi inyotekelezwa Wilayani humo itaendelea kutunzwa na kusimamiwa ipasavyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kutoa huduma kama iliyokusudiwa na kuleta tija kwa wananchi.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.