Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Alhaji Rajabu Kundya ameongoza maelfu ya wananchi wa Same katika zoezi la kupokea Mwenge Maalum wa Uhuru leo Juni 05 ,2021 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Steven Kagaigai chini ya uangalizi wa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa LT Josephine Paul Mwambashi.Mapokezi ya Mwenge wa uhuru yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi chekereni vilivyopo ndani ya kata ya Mabilioni.
Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mwenge wa Uhuru 2021 umetembelea jumla ya miradi saba yenye thamani ya Shil.2,466,981,782/=.Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa kituo cha waathirika wa madawa ya kulevya uliopo kata ya Mabilioni uliogharimu Shil.800,000,000/=, mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu kata ya Hedaru uliogharimu Shil.132,803,454/=.,mradi wa upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya maji Kasapo kata ya Makanya uliogharimu Shil.636,136,875/=,mradi wa Zahanati ya Kasapo uliopo kata ya Makanya uliogharimu Shil.163,609,067/= , mradi wa ujenzi wa soko la barabarani uliopo kata ya Bangalala uliogharimu Shil.254,931,386/=,mradi wa barabara ya Bomani uliopo kata ya Stesheni uliogharimu Shil.429,501,000/= na mradi wa vijana wajasiriamali uliopo kata ya Same uliogharimu Shil.50,000,000/=
Akizungumza wakati alipotembelea mradi wa kituo cha waathirika wa madawa ya kulevya kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa LT Josephine Paul Mwambashi amekiri kuwa mradi huo ni mzuri na kwa kuwa utahudumia waathirika wa madawa ya kulevya katika kata ya Mabilioni na kupunguza idadi kubwa ya waathika wa madawa ya kulevya kwa wakazi wa kata ya Mabilioni.
Sambamba na hayo Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 umetembele mabanda mbalimbali ya takukuru,TRA,Malaria pamoja na UKIMWI ambayo yameelezea shuguli mbalimbali zinazofanywa katika mabanda hayo zikihusisha vifaa na mifumo ya TEHAMA.
Akizungumza wakati wa hotuba yake kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 LT Josephine Paul Mwambashi amewaasa wana Same kwamba miradi iliyotembelewa na kuzinduliwa kukamilishwa na kutekeleza maelekezo yaliyotolewa ili kuleta tija katika jamii husika bila kusahau matumizi sahihi ya TEHAMA ili kuwa na Taifa endelevu.
Mwenge wa Uhuru Hoyeeeeeee!!!!
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.