Waziri wa Ardhi Mheshimiwa Jerry Slaa amewaruhusu wananchi wa Kata ya Ruvu ambao wanaoishi kwenye eneo la Pori Tengefu kuendelea kulima mazao yanayokomaa muda mfupi wakati Serikali ikilitafutia ufumbuzi suala lao.
Akizungumza alipofanya ziara kwenye Kata ya Ruvu Mheshimiwa Slaa aliwataka wananchi hao kufuata maelekezo ya Serikali yanayowazuia kufanya maendelezo yoyote katika eneo hilo hadi pale Serikali itakapokuja na maelekezo rasmi.
“Hili eneo ni pori Tengefu na Serikali imeshatoa maelekezo mbalimbali hapa hasa zuio la kufanya maendele ya kudumu ikiwemo kujenga nyumba za kudumu,ni vema maelekezo ya Derikali yakafuatwa ila suala la kulima mimi nawaruhusu mlime mazao ya muda mfupi” alise Waziri Slaa
Waziri Slaa alisema maamuzi kuhusu eneo hilo yanapaswa kuamuliwa na Mawaziri kutoka sekta nane na Mwenyekiti wa kikao hicho ni Wariri wa Ardhi hivyo ameahidi kuitisha kikao cha Mawaziri hao mapema mwezi February 2024 na baada ya kikao hicho atawasilisha majibu rasmi kwa Wananchi wa Ruvu.
“Mama Samia aliponiteua alinielekeza kuwa jambo asilolitaka ni kusababisha taharuki kwa wananchi,hivyo niwaombe mkae kwa amani na utulivu na mtambue kuwa Serikali ya mama Samia haiwezi kufanya maamuzi ya kuwamiza wananchi” alisema Waziri.
Awali akitoa taarifa ya Wilaya ya Same Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Kasilda Mgeni alimuomba Waziri kulipatia ufumbuzi suala la Kata ya Ruvu ambayo vijiji vyake vyote vine vipo kwenye Pori Tengefu hivyo wananchi wamezuiwa kufanya uendelezaji katika eneo hilo.
“Mheshimiwa Waziri tuna changamoto ya wananchi wetu wa Kata ya Ruvu kuishi kwenye pori Tengefu, Wizara ya Maliasili na Utalii ilituarifu kwamba Kata ya Ruvu ni Pori Tengefu lakini Kata hii ina Wananchi elfu kumi na tisa na vijiji vyote vimesajiliwa,hapa kuna shule na kituo cha afya,tunaomba Serikali itusaidie kupata ufumbuzi wa mapema” alisema Mheshimiwa Kasilda.
Mbunge wa Jimbi la Same Magharibi Mheshimiwa David Mathayo aliwaambia wananchi hao kuwa amelazimika kumuomba Waziri wa Ardhi kufika kwenye Kata ya Ruvu ili aweze kusikia kilio cha wananchi hao cha kuzuiwa kufanya maendeleo yoyote katika Kata hiyo hadi Serikali itakapotoa maamuzi.
“Nikuombe tuu Mheshimiwa Waziri haya majibu yaje mapema ili wananchi hawa waache kuishi kwa hofu”alisema Mathayo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.