Wilaya ya Same inatarajiwa kuwa mwenyeji Kimkoa wa maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.
Mkuu wa Wilaya ya Same,Mhe:Kasilda Mgeni amesema maandalizi yote kwaajili ya kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo yapo tayari.
Alisema katika kuelekea kilele Cha siku ya wanawake Machi 8 wanawake Wilayani humo wamekuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya kupinga ukatili mashuleni.
"Tumekuwa na wiki nzima ya shughuli mbalimbali za kijamii katika kuadhimisha wiki ya wanawake ambayo kilele chake ni Machi 8"alisema Mgeni
Alisema Elimu ya kujilinda dhidi ya ukatili imetolewa katika Shule za msingi na Sekondari pia kumefanyika zoezi la kuotesha miti 100 katika Shule ya Sekondari Mighareni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Anastazia Tutuba amesema shughuli nyingine zilizofanyika ni pamoja na kutoa elimu ya kuzuia ukatili,Elimu ya Lishe na maelekezo ya namna ya kunufaika na mkopo wa Halmashauri kwa wafanyabiashara katika soko Kuu la Kwasakwasa.
Alisema wanawake Wilayani humo pia watatoa misaada mbalimbali ya kijamii katika vituo vya watoto yatima na jioni ya Machi 8 kutakuwa na hafla fupi ya usiku wa familia ambao utafanyika Mkomazi Stop Over.
"Tumefarijika Sana maadhimisho haya kufanyika kimkoa katika Wilaya yetu na tumejiandaa vema kuwapokea wageni"alisema Tutuba.
Maadhimisho ya Kilele Cha siku ya wanawake Mkoa wa Kilimanjaro yatafanyika katika viwanja vya Stendi kuu ya mabasi Same na yatajumuisha na maonyesho ya biashara mbalimbali za wanawake.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.