Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Same yafana ambapo yamefanyika ndani ya kata ya Njoro katika kijiji cha Njoro katika shule ya sekondari Njoro huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Senyamule.
Sherehe hizo zimepambwa na burudani mbalimbali kama vile maigizo,ngonjera na nyimbo zenye jumbe mbalimbali kuhusu changamoto ,uwezo ,thamani na umuhimu wa mtoto kutoka kwa watoto wa shule mbalimbali ndani ya Wilaya ya Same.
Wadau wa mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kama NAFGEM(Network Against Female Genital Mutilation),Compasion,World Vision na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali washiriki katika kufanikisha siku ya mtoto wa Afrika Wilayani Same.
Akizungumza wakati wa mkutano mgeni rasmi Mhe.Rosemary Senyamule amewakumbusha wazazi na walezi kuwa karibu na watoto na kuwalea katika malezi bora yenye muongozo wa kumjenga mtoto vizuri kwa maisha yake ya baadae.
Akigusia kauli mbiu ya siku hii mwaka 2018 nchini Tanzania isemayo “Kuelekea uchumi wa viwanda tusimuache mtoto nyuma“Mhe.mgeni rasmi ameongelea umuhimu wa elimu katika kufanikisha hilo.
“Kumuandaa mtoto ili kukabiliana na uchumi wa viwanda ,elimu lazima ihusike”Amesisitiza Mhe.Senyamule.
Mhe. Senyamule amewataka wazazi kujiepusha na mifarakano ya kifamilia kitu ambacho huvuruga muelekeo wa watoto wengi katika jamii na ndicho chanzo cha watoto kuingia mitaani na kutafuta maisha mengine wanayofikiri ni sahihi ,hali hii hupelekea kuwa na ongezeko la watoto wa mitaani.
Mhe.Senyamule amewataka wazazi kutambua wajibu wao katika kuwatimizia watoto mahitaji yao ya msingi ili waweze kusoma vizuri na kuepuka vishawishi kama vile bodaboda na chipsi hasa hasa kwa watoto wa kike vitakavyoweza kuwarudisha nyuma kielimu.
Ikumbukwe kwamba siku ya mtoto wa Afrika huazimishwa kila mwaka Juni 16 ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watoto zaidi ya 176 waliouwawa kikatili kwa kupigwa risasi za moto na wengine zaidi ya elfu ishirini (20) kujeruhiwa walipokuwa katika maandamano ya amani kudai haki zao kwa uongozi wa makaburu, tarehe 16 Juni 1976 mjini Soweto nchini Afrika ya kusini.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.