Divisheni ya Elimu Sekondari katika Wilaya ya Same imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufundisha vema somo la Kiingereza (English Orientation Course) walimu 47 wa somo hilo kutoka katika Shule mbalimbali Wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa mbinu walimu hao ili waweze kufundisha vema somo la Kiingereza kwa wahitimu wa darasa la Saba.
"Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI aliagiza Wanafunzi wote waliohitimu elimu ya Msingi wapatiwe kozi ya Kiingereza katika Shule za Sekondari zilizo jirani na maeneo yao wakati wakisubiri kujiunga na kidato cha kwanza, hivyo tumeona nivema kuwapa mafunzo walimu wanaokwenda kuwafundisha"alisema Bi.Tutuba
Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Wilaya ya Same,Bi. Neema Lemunge amesema Mafunzo hayo yametolewa na Walimu kutoka Shule zinazofanya vizuri katika somo la Kiingereza Wilayani Moshi na yalijumuisha pia Maafisa Elimu kutoka Kata zote 34 za Wilaya ya Same na walimu 4 toka Shule binafsi.
Bi.Lemunge amesema tayari Shule zote za Sekondari zimeshapokea Wanafunzi waliohitimu darasa la Saba na mafunzo ya Kiingereza yataendelea hadi Desemba 2023.
"Lengo letu ni kuongeza umahiri wa ufundishaji na lugha ya kiingereza kwa walimu wetu ili waweze kufundisha Wanafunzi kuandika,kusoma,kuongea kusikiliza na kuelewa lugha ya Kiingereza vizuri"alisema Bi.Lemunge.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.