Same imekuwa Wilaya ya kwanza kutengeneza mpango mkakati wa mazingira na utalii 2018-2023 ambapo uzinduzi huo umefanyika katika kilele cha mlima Shengena kwenye hifadhi ya msitu wa Chome umbali wa kilometa 2462 toka usawa wa bahari.Watu 160 wamepewa vyeti vya kufika kileleni.
Fataki zapigwa kama ishara ya uzinduzi
Mpango wa mazingira utaunganisha mbuga ya Mkomazi,msitu wa Chome,kilele cha Shengena na utalii wa asili.Kutengeneza kifurushi(package) cha utalii na kuipa jina maalumu(brand).
Utekelezaji wa mpango kuifanya Same kuwa kivutio cha pekee na kuongeza idadi ya watalii.
Mpango wa mazingira kutumika kuunganisha wadau kuibadilisha Wilaya ya Same.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha Waziri,pamoja na kupongeza juhudi za Wilaya ya Same,aahidi kushirikiana na Wilaya kutekeleze mipango hiyo kwani kitu wanachofanya ni kati ya vipaumbele vya serikali kwa kuimarisha utalii katika maeneo mengi ili yaweze kujitegemea.
Naye CEO wa TFS Prof.Silayo aeleza adhima ya kuimarisha utalii wa ikolojia ya msitu huo ili uweze kuongeza kipato kwa wananchi kushirikiana na seriikali
Mkurugenzi wa TANAPA aahidi kushirikiana na TFS kutangaza utalii wa mkomazi na shengena ili kuvutia zaidi watalii
Makamu mkuu wa chuo cha mipango Dodoma Prof.Israel Katega aahidi kushirikiana na kuhakikisha mpango huo unatekelezwa.
Mwandishi wa UNDP aahidi kusaidia utekelezaji wa mpango
Naye Mwakilishi wa RC Kilimanjaro Mh.Kippi Warioba asema jambo hili ni la kuigwa na wilaya nyingine. Apongeza aahadi kutangaza utalii ya shengena.
"Shukrani yetu kwa wliotengeneza mipango hii na mliohudhuria leo ni kuhakikisha mipango hii haikai kabatini,tutaitekeleza na kuhakikisha inachangia maendeleo ya harakati za wilaya ya same. Asanteni mno" hayo yalisemwa na DC Same Mh Rosemary Senyamule
Shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na DC Siha,Mkt CCM W,DAS Hai ,Wiz,TAMISEMI,Mazingira,utalii,NEMIC,wawakilishi wa mkoa,Mkomazi,NGO,Benki wanasame walio nje ya same,na viongozi ngazi zote za wilaya ambao kwa umoja wao waliahidi kutekeleza mpango.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.