Halmashauri ya Wilaya ya Same,imekabidhi mkopo wa Shilingi Milioni 110 kwa vikundi 25 vya Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu.
Mkopo huu unafanya jumla ya mikopo iliyotolewa na Halmashauri kwa vikundi maalum kwa mwaka huu wa fedha kufikia Shilingi milioni 310 ambazo zimetolewa kwa vikundi 77.
Akikabidhi mkopo huo,Mkuu wa Wilaya ya Same,Mhe Kasilda Mgeni amewataka wanufaika hao kuhakikisha kuwa wanarejesha mkopo kwa wakati.
"Hii ni mikopo isiyo na riba ambayo Mheshimiwa Rais ameagiza itolewe kwa makundi haya maalum ili iwasaidie kuwakomboa kiuchumi,hivyo mnaporejesha kwa wakati inawezesha kukopeshwa watu wengine"amesema Kasilda
Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa kuzingatia kutenga asilimia 10 ya mapato yake na kuwakopesha wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Awali akitoa taarifa ya utoaji wa mikopo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Anastazia Tutuba amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ililenga kukopesha Mil 186 ambayo ni asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.
"Tukiwa tumebakiza robo moja kumaliza mwaka wa fedha 2022/23 tayari tumeshatoa mikopo ya Shilingi Mil 174 inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani na mil 136 inatokana na marejesho ya vikundi,hivyo kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kuwa Milioni 310"anasema Anastazia
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Same, Benedict Missani anasema hali ya marejesho ni nzuri kwani kwa mwaka huu wa fedha tayari Shilingi Milioni 153 zimeweza kurejeshwa.
Salma Khan ni mwanamama kutoka kikundi Cha Ushonaji cha Amazing Grace ambaye anasema mikopo hiyo isiyo na riba imewawezesha kujikwamua kiuchumi kwa kuongeza Vitendea kazi na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.
"Mwaka Jana tulilipa milioni tatu na tumeweza kurejesha mwaka huu tumepata mil 10 na tuna uhakika wa kurejesha,tunamsgukuru Sana Rais Samia"anasema Salma
Mwisho.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.