Maafisa Afya Wilayani Same wakiongozwa na Afisa Afya Wilaya Bi.Yuster Malisa wakiwa wanatoa Elimu ya tahadhari juu ya Ugonjwa wa homa ya Mpox katika Shule mbalimbali ili kuwawezesha wanafunzi kujilinda dhidi ya ugonjwa huo na kufikisha Elimu kwa wengine.
Akizungumza kuhusu tahadhari za kujilinda na ugonjwa huo Bi.Yuster alisema wananchi wanapaswa kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka,kuepuka kushikana mikono na kukumbatiana,kuepuka kugusa majimaji yatokayo kwa mgonjwa wa Mpox.
Amesema tahadhari nyingine ni kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko,kusafisha mara kwa mara vitu vinavyoguswa.
Mpox ni ugonjwa wa mlipuko unaosababishwa na kirusi kinachojulikana kama Monkeypox ambapo dalili zake ni pamoja na Upele,malengelenge au vidonda mwilini.
Dalili nyingine ni kupata homa,vidonda vya koo,maumivu ya kichwa, mgongo,misuli, uchovu wa mwili na kuvimba mitoki ya mwili.
"Ugonjwa wa Mpox hauna tiba maalum hivyo mgonjwa hutibiwa kulingana na dalili zinazoambatana na ugonjwa huo"Alisema Bi.Yuster.
@wizarayaafyatz
@maelezonews
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.