Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw. Jimson Mhagama amewapongeza washiriki wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) kutoka Wilaya ya Same kwa kushinda vikombe sita na kushika nafasi ya tatu ngazi ya Mkoa.
"Tuliitamani sana nafasi ya kwanza lakini hata nafasi mliyoshika sio mbaya ila mwakani ongezeni bidiii"alisema BW.Jimson
Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Same Mwl Marclaud Mero alisema Wilaya ilijipanga vizuri na lengo likiwa ni kurudi na vikombe vya kutosha katika mashindano hayo.
"Lengo letu halikuwa kushiriki Tu mashindano bali lengo lilikua kushinda na kama mnavyoona tumerudi na vikombe vya kutosha kabisa na tumetoka wanafunzi 50 kuunda timu za mkoa"alisema Mwl.Mero.
Naye Mratibu wa UMITASHUMTA Wilaya ya Same Mwl.Nathaniel Msangi alisema vijana wake wamepambana Sana na wamefanikiwa kupata nafasi ya tatu kati ya Halmashauri Saba zilizoshiriki.
"Tupo nafasi nzuri kimkoa lakini lengo letu ni kushika nafasi ya kwanza,mwakani tutapambania nafasi ya kwanza ambayo mwaka huu imechukuliwa na Manispaa ya Moshi ikifuatiwa na Moshi Vijijini"alisema Msangi.
Timu zilizoshinda vikombe kwa kushika nafasi ya kwanza ni Riadha wasichana na wavulana,Mpira wa wavu wavulana na wasichana,Mpira wa kikapu wasichana na wavulana.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.