Halmashauri ya Wilaya ya Same ni miongoni mwa Halmashauri zinazoshiriki maonyesho ya 30 ya Kilimo na Sherehe za Nanenane mwaka 2024 yanayofanyika Kanda ya Kaskazini katika Viwanja vya Themi Njoro Mkoani Arusha.
Katika maonesho hayo Halmashauri ya Wilaya ya Same imeshiriki kuonesha shughuli mbalimbali za Kilimo, Mifugo na Uvivu ili kuwawezesha wananchi kufanya vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw. Jimson Mhagama amesema lengo la kushiriki maonesho hayo ni kuwakutanisha wakulima, wafugaji na wavuvi na wenzao ili waweze kuongeza ujuzi katika kile wanachokifanya.
Alisema Maonesho ya Nane nane ya Kilimo yanasaidia wafugaji,wakulima na wavuvi kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuongeza thamani ya kile wanachokifanya.
Wilaya ya Same ni wazalishaji wa Tangawizi,Mpunga,Kahawa,Mkonge ,Mahindi pamoja na mazao ya mbogamboga kama nyanya ,vitunguu na mazao ya mikunde kama maharage na fiwi ambayo huuzwa ndani na nje ya nchi.
“Tunao wataalam wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi kwenye Halmashauri yetu ambao hutoa elimu ya mara kwa mara kwa watu wetu lakini tunaamini wanaposhiriki maonesho haya wanapata ujuzi zaidi” amesema Bw.Mhagama
Mratibu wa maonyesho ya Nanenane Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi. Yulia Joel alisema baada ya maonesho ya Nanenane wakulima huwa wanajitahidi kuboresha uzalishaji kwa kuzingatia walichojifunza Nanenane.
Maonesho ya Nanenane ya Kilimo ,Mifungo na Uvuvi hufanyika kila mwaka hapa nchini kuanzia Agosti mosi na kufikia kilele chake Agosti 08 ambapo kwa mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo “Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwaajili ya Maendeleo endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi”
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.