Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu ameipongeza Wilaya ya Same kwa Matumizi mazuri ya shilingi bilioni 2 zilizotolewa na Serikali kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
"Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya hongera sana Kwa usimamizi mzuri,kutumia bilioni mbili kujenga majengo yote haya sio Jambo jepesi,niwape hongera sana"alipongeza Mhe.Babu
Akiwa katika ziara ya kukagua Miradi Wilayani Same Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alieleza kuridhishwa na matumizi sahihi ya fedha za Miradi.
Fedha hizo zimetumika kujenga majengo nane likiwemo jengo la wagonjwa wa nje,jengo la baba,mama na mtoto,jengo la Utawala,jengo la kuhifadhi Dawa,jengo la kufulia na jengo la mionzi.
Akitoa taarifa ya Ujenzi huo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same DK.Alex Alexander alisema majengo matatu yamebakia hatua ya umaliziaji na tayari Wilaya imeomba kuongezewa Shilingi milioni 400 ili kukamilisha majengo hayo.
Pamoja na fedha hizo pia Wilaya ilipokea milioni 500 kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba hospitalini hapo na tayari vifaa hivyo vimeshanunuliwa na huduma zimeanza kutolewa kwa wagonjwa wa nje (OPD).
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.