Halmashauri ya Wilaya ya Same imepokea Shilingi Mil.554.2 kutoka Mradi wa Kuboresha Ujifunzaji na Ufundishaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akizungumzia matumizi ya fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama alisema fedha hizo zitatumika kujenga matundu 42 ya vyoo na madarasa 15 kwenye shule za Msingi saba.
“Fedha hizi tayari zilishapokelewa kwenye akaunti za shule husika na tayari hatua za awali za ujenzi zimeshaanza, tunatarajia baada ya miezi miwili kuanzia sasa ujenzi huu utakua umekamilika” alisema Bw. Mhagama.
Alizitaja shule zilizonufaika na mgawo huo kuwa ni shule za Mokande,Mferejini na Majevu ambazo kila moja imepata Shilingi milioni 88.6 kwaajili ya ujenzi wa madarasa matatu na matundu sita ya choo, nyingine ni Kirongwe, Karamba na Kizerui ambazo kila moja imepata shilingi milioni 65.6 kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu suta ya vyoo,na Shule ya Msingi Boda iliyopokea shilingi Milioni 91.6.
Wilaya ya Same pia imepokea fedha Shilingi milioni 96.8 kutoka Mradi Endelevu wa Usambazaji Maji na Usafi wa mazingira Vijijini(Sustainable Rural Water Supply and Sanitation) ambapo fedha hizo zimegawanywa kwenye shule mbili za Mhezi ambayo imepokea shilingi Mil. 48.3 na shule ya Ishinde imepokea milioni 48.5 ambazo zote zitatumika kujenga matundu 17 ya vyoo kwa kila shule.
Nae Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Same Bw.Marclaud Mero alisema mwaka juzi Wilaya ya Same ilipokea kiasi cha shilingi Bil 8 kutoka Mradi wa BOOST fedha ambazo zilitumika kujenga shule mpya mbili za kisasa za Msingi za Kisima na Anna Kilango, pia zilijenga madarasa 39 na matundu ya vyoo.
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutoa fedha za kuboresha miundombinu mbalimbali kwenye shule za msingi nchini kupitia Miradi mbalimbali ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.