Halmashauri ya Wilaya ya Same imepokea jumla ya shilingi Bil 1.8 kutoka Mradi wa kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za Awali na Msingi (BOOST)ambazo zitatekeleza miradi mbalimbali katika shule 10 za Msingi.
Akitoa taarifa katika kikao cha Baraza la Madiwani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Anastazia Tutuba amesema fedha hizo tayari zimeshaingia katika Akaunti za shule kwaajili ya kuanza utekelezaji.
Alizitaja shule zinazonufaika na Mradi wa BOOST Wilayani Same kuwa ni Shule ya Msingi Kisima ambapo patajengwa shule mpya((446,500,000/-),Shule ya Msingi Mgandu ambapo patajengwa pia shule mpya(348,500,000/-).
Shule nyingine ni Mpirani,Turiani na Kwesasu ambazo kila moja imepatiwa shilingi 131,300,000/-kwaajili ya ujenzi wa madarasa matano kila moja huku shule ya Msingi Mbono na Ndolwa ambazo kila moja imepatiwa shilingi 181,300,000/- kwaajili ya ujenzi wa madarasa saba kila shule..
“Shule ya Msingi Kikwete imepokea Shilingi 162,600,000/-kwaajili ya ujenzi wa madarasa sita na Dimbwi wamepokea shilingi 81,300,000/- kwaajili ya ujenzi wa madarasa matatu huku shule ya Msingi Mbuyuni ikipokea Shilingi 69,100,000/- kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya kisasa ya Awali ”amesema Tutuba.
Mkurugenzi ameishukuru Serikali kwa fedha hizo ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa madarasa katika shule za Msingi Wilayani humo na pia kusaidia ongezeko la shule kwa kujenga shule mpya.
Akipokea taarifa hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Yusto Mapande pia aliishukuru serikali kwa kuipatiwa Wilaya hiyo fedha hizo ambapo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri na timu yake kuhakikisha kuwa Miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaostahili.
“Sina mashaka na wewe Mkurugenzi nina imani hii miradi utaisismamia vema ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora kama unavyosimamia miradi mingine inayotekelezwa katika Wilaya yetu”alisema Mhe.Mapande
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.