Mkuu wa wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni amempongeza Rais wa Awamu ya Sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya hiyo kiasi cha shilingi 554,200,000/- ili kutekeleza miradi ya BOOST inayolenga kuboresha miundombinu kwenye shule za msingi.
“Wilaya ya Same tumenufaika kwa kiasi kikubwa na Mradi wa BOOST utakaosaidia kutatua changamoto za miundombinu kwenye elimu ya msingi” alisema
Same ina majimbo mawili ya uchaguzi na katika mgawo huu majimbo yote yamenufaika na mgawo wa fedha za BOOST kwaajili ya kujenga madarasa mapya na matundu ya vyoo.
Alisema kwa mwaka jana Wilaya hiyo ilipata zaidi ya shilingi bilioni 8 za kutekeleza mradi wa BOOST ambazo zilijenga shule mpya mbili ,madarasa arobaini na matundu ya vyoo Zaidi ya 20.
Akizungumzia mapokezi ya fedha za BOOST, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mpirani Bi.Ester Mlay alisema shule hiyo ilipokea shilingi mili 131.3 kwaajili ya ujenzi wa madarasa matano na ujenzi wake umeshakamilika.
Mwl. Mlay pia ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuipatia shule hiyo mgawo wa fedha za BOOST ambao umewezesha kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
Naye Mhe.Rashid Juma Diwani Kata ya Maore amemshukuru Mhe. Rais kwa kuiwezesha Kata hiyo kupata Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa mapya 30.
Diwani Rashid alisema Kata yake imepokea takribani shilingi bilioni moja na milioni mia tano ishirini na nane kwaajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali.
“Miradi yote hii imetekelezwa wakati huu wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwakweli Maore tunamshukuru Rais kwa miradi hii.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.