Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni ameongoza wananchi wa Kijiji cha Ishinde Kata ya Njoro Wilayani humo kwenye zoezi la upandaji miti kando kando ya barabara kuu ya Moshi - Dar es Salaam kama sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu kupanda miti pembezoni mwa barabara.
"Wilaya ya Same baada ya kupokea maelekezo hayo tumeungana na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo mpaka sasa tumepanda zaidi ya miti elfu kumi na sita kando kando ya barabara kuu, na kwenye Kata ya Njoro pekee tumepanda miti elfu tatu" Alisema Mhe.Kasilda.
Amesema lengo ni kurejesha Same ya kijani kama ilivyokua miaka ya nyuma kabla ya uharibifu wa Mazingira.
Mkuu huyo wa Wilaya amewaelekeza wananchi wote wa Same kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu kuungamkono jitihada za Serikali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda miti angalau mitano kwenye eneo la makazi yake lakini pia kando ya mashamba yao.
Nae Diwani wa Kata ya Njoro Mhe.Abdallah Omar aliishukuru TFS kwa kuwapatia miche ya miti waliyootesha.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.