Wilaya ya Same leo imeungana na Wilaya nyingine nchini kufanya maombi maalum ya kuombea Muungano uendelee kudumu na kuwaombea Viongozi waweze kuongoza vema Taifa la Tanzania.
Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Same katika maombi hayo yaliyofanyika April 22 ,Katibu Tawala wa Wilaya ya Same Bi.Upendo Wella amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeweza kutimiza miaka 60 kutokana na Uongozi Imara wa Viongozi wa Tanzania.
Akizungumza kabla ya kuongoza maombi hayo Katibu wa Makanisa ya Pentekoste Mkoa wa Kilimanjaro Mch.Daudi Kiula alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza maombi yafanyike nchi nzima kuombea Taifa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Kiongozi wetu wa nchi amepata maono mazuri sana na nina imani kwasababu muongozo huu umeanzia kwa kiongozi Mkuu wa nchi Mungu hatoacha kutusikiliza na kututendea kama tunavyoomba,Mungu amlinde sana Rais wetu” alisema Mch.Kiula
Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26,1964 ambapo waliokuwa Marais wa nchi hizo Hayati Julius Kambarage Nyerere akiwa Rais wa Tanganyika na mwenzie Abeid Amani Karume akiwa Rais wa Zanzibar walichanganya udongo wa nchi hizi mbili ambapo ilizaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.